Ingia

Music News

Lifestyle

Mfalme Mswati adaiwa kumpa Joseph Kabila uraia wa Eswatini kinyume cha Sheria.

18th Dec, 2025

Mfalme Mswati adaiwa kumpa Joseph Kabila uraia wa Eswatini kinyume cha Sheria.


Katika kile kinachotajwa kama mzozo mpya wa kidiplomasia na utawala wa kifalme, Mfalme Mswati III wa Eswatini anadaiwa kumpatia uraia wa taifa hilo aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Joseph Kabila, kinyume na sheria na taratibu za uraia wa nchi hiyo.


Kwa mujibu wa uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti la Swaziland News, Kabila alipewa uraia na hata kupatiwa pasipoti ya kidiplomasia ya Eswatini baada ya agizo la moja kwa moja kutoka kwa Mfalme Mswati kwa Bodi ya Uraia.


“Nyaraka rasmi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani zinaonyesha kuwa Joseph Kabila alipewa uraia kwa agizo maalum la kifalme, bila kupitia mchakato wa kisheria wa uraia kwa wageni,” limeandika Gazeti hilo.


Hatua hiyo imezua sintofahamu, hasa ikizingatiwa kuwa Kabila alihukumiwa na Mahakama ya Kijeshi ya DRC adhabu ya kifo kwa makosa ya uhaini, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, akihusishwa na kundi la Waasi la M23.


Taarifa zaidi zinaeleza kuwa mnamo Jumamosi, Novemba 29, 2025, Kabila aliondoka nchini Eswatini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Mswati, akiwa na pasipoti ya kidiplomasia ya Eswatini, na hiyo ilikuwa safari yake ya kwanza kutumia hati hiyo mpya ya kusafiria.


“Mfumo wa Uhamiaji wa Eswatini unaonyesha kuwa hiyo ndiyo ilikuwa safari yake ya kwanza kutumia pasipoti mpya, lakini kwa sababu za kiusalama, hatuwezi kuweka wazi namba ya pasipoti hiyo,” limeeleza Swaziland News.


Mpaka sasa, Serikali ya Eswatini haijatoa tamko lolote rasmi kuhusu suala hili, huku Wachambuzi wa masuala ya sheria na haki za binadamu wakisema hatua hiyo inaweza kuvuruga taswira ya Eswatini kimataifa.


Hili linaendelea kuwa moja ya matukio ya kushangaza barani Afrika, likifungua mjadala kuhusu ushawishi wa watawala na uhusiano wao na Wanasiasa waliopoteza mamlaka katika nchi zao.


Toa maoni yako 

#MvanoHabari

#MvanoMtangazaji

#Mv34

.

Tangazo - nitakusemea kwa baba unaniumiza
nitakusemea kwa baba unaniumiza