Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

1--2 CAPTAIN MAVERICK NA MISSION YA MAPENZI ๐Ÿ’”๐Ÿ’”

11th Aug, 2025 Views 12


HURU MEDIA

SEHEMU : 1

Katika jumba moja kubwa la kifahari alionekana binti mmoja mrembo sana akiwa anakatia maua kwenye bustani. Iliyojaa maua mazuri na ya kupendeza na uso wakeulipambwa na tabasamu pana

" Madam Gabriella unaweza kuumia acha hiyo kazi anaweza kufanya kigo hiyo ndo kazi yake inayofanya analipwa kwenye hii nyumba"
aliongea mfanyakazi mmoja akionyesha kuwa na wasiwasi sana

"Zena acheni kuwa hivyo bhana nani kawaambi Mimi nimeumbwa na glass kwamba kitu kidogo tu nitavunjika acheni hizo basi " aliongea Gabriella huku anatabasamu

" Lakini madam utatupa wakati mgumu endapo ukiumia unamjua vizuri mume wako Mr Tristan alivyo "
aliongea mfanyakazi mwingine aliyeitwa Jema

" Sawa sawa basi nitaacha ..mmfurahi Sasa hamtaki nifanye kitu chochote ni mwaka Sasa umepita jamani lakini bado mnanifanya kama mgeni "
Gabriella aliweka mkasi wa kukatia maua chini

" Hapana madam sio kama tunakuona kama mgeni ila tunakupenda sana na Mr Tristan anakupenda sana pia ndomana hataki uguse kitu chochote kinachoweza kukuumiza au kusababisha madhara yoyote"

" Sawa nitakaa tu chumbani kwangu kama mnavyotaka "
Gabriella aliingia chumbani kwake akafunga mlango alianza kutabasamu akajitupa kitandani

" Leo ninafuraha Sana siamini kama tunatimi za miaka miwili ya ndoa yetu ...natakiwa kufanya kitu "
Gabriella alichukua simu yake aliingia mtandaoni alifanya booking ya meza kwenye hoteli moja ya kifahari

" Nimemaliza sasa ngoja nikajiandae "
Gabriella aliingia bafuni

Gabriella ni binti wa miaka 26 jina lake kamili ni Gabriella Alphonse ni mtoto wa kwanza kati ya watoto wawili wa Mr Alphonse na bi Carina Mr Alphonse ni mmiliki wa kampuni yake ya mambo ya usafirishaji iliyoitwa Nextinn mtoto wa pili ni mdogo wake Gladness mwanye miaka 20 na yupo chuo ,miaka miwili iliyopita Gabriella aliolewa na Tristan ambae ni CEO wa kampuni iliyoitwa Maxwell ndoa yao ilijengwa kwa upendo mzito Tristan alimjali sana Gabriella Kwa upande wa kampuni moja kubwa iliyoitwa Maxwell kwenye ofisi ya CEO alionekana mkaka mmoja handsome sana

" Tristan ni lini utaachana na huyo mwanamke wako ?" Aliuliza dada mmoja alionekana mrembo pia

"Babe nimekuahidi nitaachana nae muda sahihi ukifika kwanini unakuwa huana uvumilivu "
aliongea Tristan

" Uvumilivu ? Na vipi kuhusu mtoto wetu aliyepo tumboni kwangu yeye pia haumjali ,kama haumtaki huyu mtoto sema tu nitamlea mwenyewe sishindwi kufanya hivyo Tristan" Silvia alitaka kuondoka Tristan alimkimbilia na kumkumbatia

" Nawezaje kukuacha mpenzi wangu nakupenda sana wewe pamoja na mtoto wetu ajae nakuahidi nitaachana nae "
Tristan alimbembeleza Silvia

" Utaachana nae lini ?" Aliuliza Silvia

" Nitaachana nae Leo nataka kuongea na mwanasheria wangu kabisa "

" Asante sana hunny ndomana nakupendaga " Silvia alimkumbatia Tristan huku anatabasamu

Kwa upande wa Gabriella aliandaa kila kitu kwaajili ya kusherekea miaka yao miwili ya ndoa Kisha alimtumia Tristan message

" Mume wangu kipenzi ..Habibi wangu nataka kukutoa out leo mida ya saa moja ,makutano ni pale pale kwenye hoteli yetu pendwa "
Tristan aliisoma ile message akatupa simu yake pembeni alionekana wazi hamjali Tena mke wake Gabriella

Mida ya saa moja jioni Gabriella alifika green view hotel akiwa amependeza sana wanaume waliokuwepo pale hotelini hawakuacha kumsindikiza Kwa macho , meza ilikuwa imeandaliwa vizuri kama alivyoagiza

" Limepita lisaa limoja Sasa kwanini hakufika mpaka saizi mara zote Tristan ni mtu wa kwenda na muda imekuwaje Leo " Gabriella alipata wasiwasi alianza kumpigia Tristan lakini simu zake hazikupokelewa Gabriella aliendelea kusubiri bila kuchoka Saa tatu usiku ndipo Tristan alifika akiwa na bahasha ya kaki mkononi

" My hubby ulikuwa wapi unajua ulinipa wasiwasi sana "
Gabriella alienda kumkumbatia ,Tristan alimsukuma

"Kuna kitu cha muhimu sana nataka kukwambia " Tristan alivuta kiti akakaa

" Honey unaonaje tukakata Keki kwanza then utaniambia unachotaka kuniambia " aliongea Gabriella huku anatabasamu

"Sina muda mchafu wa kupoteza Kwa vitu vya kijinga kama hivyo nitaenda moja Kwa moja kwenye pointi hizi ni karatasi za taraka Saini " Tristan alimtupia Gabriella ile bahasha

" Tristan acha utani bhana mume wangu unanitisha mwenzio ujue "
Gabriella alicheka maana hakumzoea mume wake kuwa hivyo alidhani labda ni utani tu kwasababu ni mwanaume anaemjali sana

" Mimi sio mchekeshaji namaanisha ninachokisema Saini haraka nataka kuondoka "
Gabriella alitoa zile karatasi na ni kweli haukuwa utani zilikuwa ni karatasi za taraka

" Tristan kwanini ? Kwanini unanifanyia hivi nimefanya kosa gani mume wangu ?"

" Kosa ulilolifanya ni kukubali kuolewa na mtu tajiri Kwa maslahi ya familia yako"

" Lakini ulikubali kunioa Tristan na ulinipenda sana "
Gabriella alianza kulia

" Nilikuonea huruma tu na wala haukuwa upendo wa dhati ..Kwa Sasa umejua Sasa nataka Usaini hizi karatasi na kingine nimepata mwanamke ninaempenda sana na tunatarajia kupata mtoto hauna nafasi Tena kwenye moyo wangu "

" Tristan ulisema hauwezi kuniacha hata kama hatutopata mtoto kwanini saizi umekuwa hivi Tristan ni kitu gani kimekubadilisha mume wangu "

" Kulia hakuta saidia kitu nakupa siku mbili Saini hizi taraka "
Tristan aliondoka hakumjali Tena Gabriella

Gabriella alifuta machozi akaondoka alienda nyumbani Kwa rafiki yake Veronica

" Karibu kipenzi na mbona kama haupo sawa ?"
Veronica alimuangalia Gabriella usoni

" Ni kweli sipo sawa Vero "
Gabriella alianza kulia , Veronica alimkumbatia Kwa nguvu na kuanza kubembeleza

" Niambie kipenzi changu shida Nini sijakuzoea kua una Lia Lia nakujua wewe ni super woman machozi kwako ni mwiko " Veronica aliongea huku ameshika mikono ya Gabriella

" Ni Tristan ...ni Tristan " Gabriella alianza kulia Tena

" Amefanya nini Shem Tristan amepata ajali au Kuna Nini acha kunipa wasiwasi malizia sentensi yako basi"
Gabriella alishindwa kuongea alimkabidhi Veronica zile karatasi za taraka

" Sikuwahi kufikiria kuwa Tristan nae ni mbwa ..kwanini anamfanyia hivi binti mfalme wangu jamani usilie kipenzi "
Veronica alimbembeleza Gabriella mpaka Alinyamaza

" Kwanini anataka muachane ?"

" Amesema Kuna mwanamke wanapendana sana na wanakaribia kupata mtoto "

" Haina haja ya kumlilia mtu msaliti kama yeye Saini hizi karatasi na muimalize hii ndoa ya kipumbavu "
aliongea Veronica Kwa hasira

" Siwezi sio rahisi kama unavyofikilia Vero tumetoka mbali Mimi na Tristan na ninampenda Sana mume wangu na yeye ndo mwanaume wangu wa kwanza "

" Umevumilia mengi ...mengi Sana Gabriella familia yake wala hawakuwahi kukupenda kila siku masimango kutoka Kwa mama mkwe na mawifi ulipendwa tu na baba mkwe wako na Sasa yeye mwenyewe Tristan hakutaki achana nae na utue huu mzigo kwanza bado unalipa sana mtu akikuangalia anasema ndo kwanza una miaka 18 "
Veronica alimshawishi sana Gabriella mpaka akakubali kusaini zile karatasi za taraka

" Una uhakika nitakuwa sawa baada ya hii taraka Vero ?"
Gabriella alimuuliza Veronica

"Nina uhakika asilimia ๐Ÿ’ฏ hata usiwaze shoga angu utakuwa na furaha kama zamani hata zaidi "
Gabriella aliagana na Veronica akaondoka Alifika nyumbani kwake mida ya saa 5 usiku alimkuta Zena na jema wanamsubiri nje

" Madam ulikuwa wapi ?tulikuwa na wasiwasi sana sio kawaida yako kuchelewa kurudi nyumbani "
waliuliza Zena na jema

" Hata msiwe na wasiwasi bhana mimi ni mtu mzima sio mtoto nilienda kumtembelea rafiki yangu kipenzi " aliongea Gabriella huku anatabasamu

" Sawa madam ila Kuna kitu tunataka kukwambia... "
Zena alitaka kuongea jema alimkanyaga mguu kama kumzuia asiseme

" Kitu gani hicho Zena nawasikiliza niambieni " Gabriella aliwaangalia Zena na jema

" Madam Wala usimjali Zena hata hakuna Cha maana "
aliongea jema huku anacheka Cheka

" Hapana hii inaonekana ipo serious niambieni msinifiche "

" Madam utakuwa sawa kweli kusikia hii taarifa ?"
Aliuliza jema

" Niambienj ili nijue mkinificha haitasaidia kitu "

" Madam ni kuwa Mr Tristan amerudi na mwanamke mwingine na wanatumia chumba ulichokuwa unatumia na Mr Tristan "
Gabriella aliangusha pochi chini kwa mshtuko alilijua hili lazima litatokea lakini hakutegemea kama Tristan atamfanyia hivi kabla ya kuondoka machozi yalimtoka kwenye macho yake mazuri

" Madam usilie kila kitu kitakuwa sawa Nina uhakika mr Tristan atakuwa amerogwa haiwezekani akufanyie hivi ghafra na ilhali anakupenda sana na kukujali"

" Hata msijali najua mnanijali sana lakini hapa hapanifai tena shika hii bahasha akiamka kesho asubuhi mtamkabidhi na kwaherini "
Gabriella alianza kuondoka

" Madam unaenda wapi usiku huu "
Zena na jema walitaka kumzuia Gabriella asiondoke lakini hakutaka kuwasikiliza hata kidogo aliondoka usiku ule ule alienda nyumbani kwao

" Dada Gabby mbona usiku usiku kwema lakini ?"
Aliuliza Gladness mdogo wa Gabriella

" Niache nipumzike kwanza kesho nitawaelezea kula kitu wewe pamoja na baba na mama "
Gabriella aliingia chumba alichokuwa alitumia zamani kabla ya kuolewa na Tristan

" Sijui kapatwa na nini ? Ananipa wasiwasi sana " Gladness aliingia chumbani kwake pia

SEHEMU YA 2
Gabriella hakupata usingizi kabisa usiku huo alikumbuka mambo waliyofanya pamoja akiwa na Tristan hakuamini kabisa kama angebadirika namna ile alitamani iwe ni ndoto na aamke mara moja

Asubuhi mida ya saa 1 Mr Alphonse na mkewe bi Carina walikuwa mezani kupata kifungua kinywa Gabriella alienda kuungana nao

" Gabriella kwanini upo hapa na kwanini umekuja bila taarifa ? mkwe wangu Tristan Yuko wapi ?Umemuaga mume wako kweli ?"
Bi Carina aliuliza maswali mfurulizo huku aliangalia huku na huku kama atamuona Tristan

" Muache mtoto anywe chai kwanza hayo maswali yako atayajibu baadae "
alisema Mr Alphonse mana anamjua vizuri mke wake alivyo

" Asante daddy " Gabriella alivuta kiti akakaa bi Carina alimuangalia kwa jicho Kali
Baada ya kumaliza kula walienda sitting room

" Mmmh tuambie kilichokuleta hapa tena ukiwa peke yako mkwe wangu Yuko wapi ?" Aliuliza bi Carina

" Mke wangu taratibu acha tumsikilize maana binti yetu anaonekana anamengi sana ya kutuambia "
alisema Mr Alphonse

"Daddy ,mom ...mimi na Tristan tumetalikiana " aliongea Gabriella kwa ujasiri hakuogopa hata kidogo

" Unasemaje wewe mpuuzi ?"
Bi Carina alimuangalia Gabriella kwa jicho Kali

" Nimesema mimi na Tristan tumeachana na sio mke na mume tena " Gabriella alishtuka baada ya mama yake kumpiga kibao kizito Cha shavu

" Unafanya nini ?"
Mr Alphonse alienda kumzuia bi Carina asiendelee kumpiga Gabriella

"Niachie nimuweke akili yake sawa anaanzaje kuongeo huo ujinga mbele yetu hajui familia ya Mr Edward ilivyotusaidia sana na bado tunaitegemea " aliongea bi Carina kwa kupayuka

" Vipi kama mtoto wetu anateseka huko na sababu ya hiyo ndoa kuisha ni Tristan wewe hata hujali unajali pesa tu kama kawaida yako " alifoka Mr Alphonse

" Umesahau kila kitu si ndio umesahau walipotutoa, familia ya Mr Edward ndo inayotuweka mjini " alisema bi Carina

" Acha kuongea ujinga kama ulimuuza mtoto wetu kwa mara ya kwanza siwezi kukuacha umuumize tena kwa mara nyingine , Gabriella binti yangu nenda chumbani kapumzike na ukumbuke baba yupo upande wako kwasababu naamini unafanya kitu sahihi " alisema Mr Alphonse

" Thanks Dady " Gabriella alitabasamu aliondoka na kuelekea chumbani kwake

" Mume wangu nadhani umesahau kwamba kampuni yetu imekuwa kubwa na tunaishi jumba la kifahari kwasababu ya familia ya Mr Edward itakuwaje kama tukikubali waacheni kila kitu kita haribika "
aliongea bi Carina huku amekasirika sana

" Tutasimamia wenyewe kampuni na kila kitu kama zamani kwanza walituwezesha tu sio kama walitusaidia kila siku, nitakuwa safarini kwa mwezi mzima usichukulie kutokuwepo kwangu kama nafasi ya kumsumbua mtoto muache apumzike "
Mr Alphonse aliondoka

" Tutaona ni lazima warudiane sitaki kujua sababu ni nini "
bi Carina alitoa simu yake akampigia Mr Edward ,baba yake na Tristan

"Mr Edward samahani sana kwa usumbufu mzazi mwenzangu " bi Carina alijichekesha

" Bila samahani sisi ni familia "
alisema Mr Edward

" Nimefurahi sana kusikia hivyo ,kwa Sasa nina huzuni sana hivyo nimepiga simu kukushukuru kwa yote mliyoifanyia familia yetu " bi Carina alianza kujiliza

" Bi Carina mbona sikuelewi shida Iko wapi mbona unalia ?"
Aliuliza Mr Edward

" Ni watoto wetu .. Gabriella amerudi nyumbani Jana anasema wametalikiana na Tristan "

" Unasemaje ? Hii haiwezekani wanaanzaje kufanya kitu kikubwa kama hicho bila kumshirikiaha mtu yoyote ,usijali bi Carina nitalishughulikia na kila kitu kita kuwa sawa " Mr Edward na bi Carina waliagana

Bi Carina alitbasama aliamua kumfuata Gabriella chumbani kwake

Kwa upande mwingine lilionekana geti kubwa la kambi ya jeshi ๏ธmilio ya honi za asubuhi ilivunja ukimya wa kambi ya jeshi ya Ndundu na tayari askari walikuwa mstari kwa mstari, macho mbele, miili imenyooka kama fimbo ya mwarobaini ,Lakini mmoja tu aliyewafanya waogope kuliko adui, alikuwa bado hajafika.Captain Maverick flanklin al maarufu kama Kifaru wa Ndundu Maverick alikuwa ni mtu wa nidhamu na amri Si kwa sababu ya vyeo vyake tu, bali kwa sababu ya historia iliyomjengea heshima na ujasiri

Maverick ni kijana wa miaka 33, mwenye macho makali kama miale ya jua, sauti nzito inayoweza kuamsha askari waliolala usingizi mzito na tabia ya kutokusamehe uzembeMaverick ni mtoto wa pili katika familia ya Mr flanklin na bi Vanessa alikuwa na dada aliyeitwa Nicole baba yake Mr flanklin ni CEO wa kampuni kubwa iliyoitwa Purenex company

"Nimesikia captain Maverick anachukua likizo ya miezi mitatu " aliongea askari mmoja kwa sauti ya chini

" Wee sio kweli sidhani kama tutaondokana nae hata mara moja "
aliongea askari mwingine kwa kunong'ona

Dakika hizo hizo aliingia captain Maverick akiwa amevalia sare zake za jeshi Askari wote walitulia kama sanamu na alipofika mbele yao alisimama walimtolea saluti kama heshima aliwaangalia kwa sekunde kumi, kisha akasema kwa sauti ya amri:

"Kuanzia leo mtakuwa chini ya uangalizi wa captain mpya , captain Raymond na kama mlivyofundishwa hapo kabla nidhamu inahitajika kwa asilimia 100 na niwakumbushe tu captain Raymond Hana mchezo , Kama wewe ni askari wa kweli, utaishi. Kama wewe ni mzembe hautahitajika tena hapa nimemaliza niwatakie mafunzo mema "
maverick alimaliza kuongea akaondoka Captain Raymond alisogea mbele

" Haya vijana kama mlivyoambiwa mimi ni captain wenu mpya kwa siku ya Leo nitawapa offa ya kupumzika mimi sio mkali kama captain Maverick"
aliongea Raymond huku anatabasamu

" Woyoo ...." askali wote walishangilia

Captain maverick hakupoteza muda alipanda kwenye gari lake na kuondoka akiwa njiani alipokea simu kutoka kwa general Amel

" Captain maverick Kuna mission ya kufuatilia uuzaji wa madawa ya kulevya inayosimamiwa na Nadya unatakiwa kuungana nae " alisema general Amel

" Ndiyo mkuu ,lakini hii mission haikuwa ya kwangu "
alisema maverick

" Captain maverick najua upo likizo lakini unatakiwa kufanya hii mission kumsaidia Nadya hii kazi inatakiwa kukamilima mapema sana iwezekanavyo "

" Sawa mkuu "
maverick alibadirisha uelekeo hakuelekea nyumbani kwake tena alienda hotelini

Bi carina aliingia chumbani Kwa Gabriella bila kugonga mlango

" Mom ndo nini Sasa unaingia bila kugonga ona Sasa umenikuta navaa"
alilalamika Gabriella huku anajifunga taulo lake

" Wewe ni mtoto wangu Kuna kipi kipya ambacho sikijui kwenye mwili wako "
bi carina alienda kukaa kwenye kochi lilikuwepo chumbani Kwa Gabriella

"Hata kama mom lakini wakati mwingine uwe unagonga mlango "

" Embu acha kunifundisha Nini cha kufanya kaa hapa nataka kuongea na wewe Tena nataka unielewe sio yaingilie huku yatokeee huku "
bi carina alimshika Gabriella masikio

" Sawa nakusikiliza " Gabriella alimuangalia mama yake

" Nimeongea na baba yako mkwe ..."
Gabriella alimkatisha mama yake

" Baba mkwe Yupi uyo ?" Aliuliza Gabriella

" Kwani humjui baba mkwe wako Mr Edward au una baba wakwe wangapi mwenzetu ,Sasa sikiliza Kwa makini ni meongea nae na amesema wewe na Tristan hamuwezi kuachana kirahisi hivi atashughulikia kila kitu wewe na Tristan mbaki kama mume na mke "

aliongea bi carina huku anatabasamu

" Nope labda sio Gabriella Mimi ,siwezi kamwe kurudiana na Tristan amenionyesha upande wake mwingine ambao sikuwahi kuutegemea hata siku moja ,siwezi kurudi Tena kwenye ngome ya mbwa mwitu ikiwa Mimi ni kondoo ,hata nikipata mwanaume basi nataka wa kuendana nae kila kitu "
alisema Gabriella

" Kwahiyo unamaanisha hata kama akiwa ni mzoa taka ,kibaka wewe twende tu ?"
Aliuliza bi carina Kwa dharau

" Ndivyo hujakosea hata kidogo cha muhimu ni mapenzi ya kweli na nipo tayari kuvumilia shida nikiwa napata upendo wa dhati "
bi carina alimpiga Gabriella kibao cha shavu

" Kaa kimya mtoto mpumbavu Kwa uzuri uliobarikiwa ,elimu ...lakini bado unafikilia ujinga huko ni kutumia vibaya rasirimali ulizopewa na muumba wako nataka kukwambia hivi utarudiana na Tristan hata iweje liweke Hilo akilini mwako mfyuuu" bi carina aliondoka chumbani Kwa Gabriella

Gabriella alibaki ameshika shavu lake alilopigwa kibao

" Wewe ni mama wa aina gani mara zote unanichukulia Mimi kama kitega uchumi chako kwanini unanilazimisha nikuchukie mama " Gabriella alianza kulia alichukua simu yake iliyokuwa ikiita akapokea hakuwa mwingine alikuwa Mr Edward

" Shkamoo baba ..." Alisalimia Gabriella

" Marahaba binti yangu mzuri ,nisamehe sana Kwa kitendo alichokifanya Tristan yote ni makosa yangu sikumlea vizuri kijana wangu "
alisema Mr Edward ni wazi alimpenda sana Gabriella na alitaka aendelee kuwa mke wa mtoto wake

" Hata usijali baba hayakuwa makosa yako umefanya kazi kubwa sana kumfanya Tristan kuwa pale alipo Sasa mfanyabiashara maarufu na tajiri ,hata kama tumeachana na Tristan wewe utaendelea kuwa baba kwangu "

aliongea Gabriella huku anafuta machozi...

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

1--2 CAPTAIN MAVERICK NA MISSION YA MAPENZI ๐Ÿ’”๐Ÿ’”  >>> https://gonga94.com/semajambo/1-2-captain-maverick-na-mission-ya-mapenzi
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

never give up harmonize
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest