Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94

ANIPHA πŸ˜‚πŸ˜‚. Mtunzi... Sehemu ya 9.

19th Jul, 2025 Views 14

ANIPHA πŸ˜‚πŸ˜‚.
Mtunzi...
Sehemu ya 9.

Maisha yalikuwa mazuri mno yani weekend tunaenda kuenjoy mimi, Brown na Mainda, siku hiyo tulikuwa kwenye hotel moja nzuri sana tunakula, Mainda akasema kuwa kuna kaka yake anakuja week hii kumsalimia hivyo tutakuwa nae kwa siku chache pale nyumbani.

"Sawa hamna shida, kipenzi tutakuwa wengi nyumabni"

"yeah, sasa Brown Sisi ngoja twende nyumbani maan muda umeenda sana"

"Hamna neno, twende niwapeleke then me nitaelekea kwangu"

Brown alitufikisha nyumbani na yeye akaelekea kwake.

"Eeh best embu niambie vizuri huyo kaka yako ni nani"

"Mmmh ona huyu jamani πŸ˜‚πŸ˜‚hapo tu ushaanza kumuwaza kaka yangu jamani"

"Hapana bwana sio hivyo, nataka tu kujua"

"Sawa anaitwa Allen, ni mdogo wangu, me naanza anafuata yeye"

"Allen, mmh sawa"

"unadhani atakuwa Allen wako πŸ˜‚πŸ˜‚, ila wewe aya bwana wacha me nikalale"

"Sawa usiku mwema"

Kila mtu aliingia chumbani kwake kulala huku mimi nikiwaza huyu Allen ni nani au Ndio Allen mpenzi wangu mimi jamani sasa itakuwaje, eeh Mungu naomba tu asiwe Allen ninaemjua mimi jamani sjui hata nitafanyaje. Niliwaza sana mwisho nikapitiwa na usingizi mpka asubuhi.

Asubuhi hiyo tukajiandaa na Baada ya hapo tukaenda kila mtu kazini kwake hapo mshahara wangu natunza tu maan nilikuwa sinunui chochote wala kulipia chochote, kila kitu alifanya Mainda basi.

Siku hua azigandi hatimae siku ya mdogo wake Mainda kuja ikafika, tukafanya usafi Nyumba nzima mpka chumba cha wageni Baada ya usafi tukapika chakula tukaandaa vizuri sasa, tukakaa sasa kumsubiri mgeni na siku hiyo hatukwenda kazini wote mimi na Mainda.

Muda ya mchana Ndio mgeni sasa akawa amefika stendi hivyo Mainda akaondoka na gari yake kwenda kumchukua huyo mgeni stendi mimi nikabaki nyumbani naanda mazingira ya kumpokea mgeni sasa.

Baada ya muda Mainda akarudi sasa na huyu mgeni, kwanza akaanza kishuka mdada kwenye gari kisha Mainda hapo mimi namsubiria tu huyo Allen πŸ˜‚πŸ˜‚hao wengine sina shida nao hata kidogo, baada sasa ya hao wengine kishuka kwenye gari Ndio akashuka sasa huyo Allen, Mungu wangu ni Allen mpenzi wangu Ndio mdogo wake na Mainda yani niishiwa nguvu kabisa, na hata yeye aliponiona alijifanya kama hanijui kabisa.

"Karibu sana mdogo wangu, naona umeniletea na Wifi kabisa"

"asante dada Mainda, na huyu anaitwa Tanasha, ni mke wangu mtarajiwa Ndio nimemleta ili umuone dada mkubwa"

"waooh jamani, karibu sana Tanasha hapa Ndio kwangu karibu sana"

"Asante sana wifi"

"Na huyu anaitwa Anipha, ni rafiki yangu sana piah anafanya kazi kwenye duka langu "

"oooh sawa basi tuingie ndani sasa dada"

Muda huo wote mimi sielewe chochote, yani mimi nimekaa siku zote hizo namuwaza Allen kumbe yeye alisha nisahau kabisa kweli jamani πŸ₯ΉπŸ₯ΉπŸ₯Ή. Tuliingia ndani mimi nikapitiliza moja kwa moja hadi chumbani kwangu nikafunga mlango nikaingia bafuni, nikafungulia maji nikiwa na nguo hivyo hivyo, nililia sana mpaka nikahisi kufa yani. Nilikuwa nahisi kama kuna kitu kinaninyiga shingoni yani jamani nyie acheni tu 😭😭😭😭yani mimi leo sina ujanja kabisa daah.

Itaendelea......
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

ANIPHA πŸ˜‚πŸ˜‚. Mtunzi... Sehemu ya 9.  >>> https://gonga94.com/semajambo/anipha-mtunzi-sehemu-ya-9
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
karibu msagala furniture
karibu msagala furniture

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MKEKA 03

majario rewards 100 Comments 0
 

.BABAMKWE epsd 19.

majario rewards 100 Comments 0
 

ALINIINGIA BILA IDHINI

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE..17..18

msagala rewards 100 Comments 0
 

bei sawa na bule

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 16

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest