ANIPHA ππ.
Sehemu ya 8.
"Na wewe kulikoni, mbona uko hivyo unaumwa ama ni nini"
"hapana Mainda niko poa, kichwa tu Ndio kinaniuma ila nitakuwa sawa tu ngoja ninywe dawa"
"sawa kunywa dawa upumzike sasa, me ngoja niende kazini sawa badae, nitakuwa nakupigia simu sawa"
"Sawa Mainda, asante"
Mainda aliondoka na kwenda kazini na mimi nikanywa dawa nikarudi kulala. Niliamka mchana na kukuta meseji kibao na missed calls nyingi kutoka kwa Brown, nikampigia simu sasa.
"Hello, Brown"
"Anipha nini shida mama mbona hupokei simu zangu, nimetuma meseji kibao hujibu kwa nini Anipha???"
"Brown, nisamehe sana sijafanya makusudi kabisa, sijiskii vizuri Ndio maan hata dukani sijafungua"
"daah pole sana jamani sikuwa najua chochote, nisamehe sana, naweza kuja kukisalimia"
"usijali niko sawa kabisa, tutaonana kesho dukani"
"sawa Anipha, uwe unapokea basi simu yangu"
"sawa hamna shida"
Baada ya Brown kukata simu, nilitoka hadi jikoni kwenda kutafuta chakula maana nilikuwa na njaa sana jamani. Nikiwa busy napika Mainda akapiga simu sasa mmbea mwenzangu ππ.
"We mwanamke vipi, unaendeleaje, maana nimepiga simu nambiwa unatumika"
"si ache yani, ni Brown Ndio alikuwa amepiga kama kawaida yake yani kulalamika tu"
"ππNdio, si anakupenda jaman Ndio maana ana lalamika tu jamani"
"aaah Mainda bwana embu Acha hizo mimi sina hata mpango na Brown jamani"
"Aya, shauri yako Anipha, kwa hiyo unaendeleaje sasa hivi"
"aah nipo sawa sasa hivi, na kesho nitaenda dukani"
"Sawa kipenzi wacha me niendelee na kazi badae"
"Sawa mama asante"
Baada ya hapo nikala chakula changu na kurudi chumbani kwangu nikaoga kisha nikalala tena mpka jioni, muda ambao Mainda Ndio alikuwa anatoka kazini kwake.
"Kipenzi, nimerudi ngoja nibadilishe nguo alafu nije nikupikie chakula sawa mwaya"
"sawa kipenzi asante"
Mainda alibadilisha nguo na kuja kupika chakula cha usiku, tukala na kuanza kupiga story, Mainda akanisimulia kuhusu mpenzi wake kuwa wamegombana na anampango wa kuachana nae.
"jamani Mainda kwa nini sasa muachane kisa nini na wewe khaa"
"Bwana wewe me sina muda wa kubembelezana na mtu mimi, yani mtu ana dharau sana we humjui Ndio maana"
"jamani aya sawa, maamuzi ni yako mama"
"na vipi kuhusu wewe"
"mimi tena kuhusu nini sasa"
"si kuhusu Allen na wewe"
"kuhusu Allen me siwezi kuwa na mpenzi wingine wakati mimi na Allen bado hatijamalizana"
"mmalizane nini tena jamani wakati yeye mwenyewe Allen alikwambia muachane, embu sikiliza inaonekana kuwa Brown anakupenda sana hivyo we kuwa nae basi"
"Mainda, asante kwa ushauri lakini mimi bado nampenda sana Allen"
"Mmh aya mama mwenye upendo wake wa agape ππ"
"Nyoo umeanza na wewe"
Baada ya story kila mtu aliingia chumbani kwake na kulala, kesho yake Asubuhi niliwai kuamka nikapike chai, tukanywa kisha tukaelekea kazini.
Nimefika tu dukani bado nafanya usafi Brown huyu hapa na maua mkononi utadhani mimi ni nyuki khaa πππ. Ikabidi nijifanye tu nimeyapenda ili asianze kulalamika hapa kama kawaida yake.
"asante sana Brown kwa kuja"
"usijali anipha, ngoja mimi niwai kazini, nitarudi badae kukupa hi"
"sawa hamna shida"
Miezi sita sasa inapita nikiwa Arusha na muda hua Brown na Mainda Ndio marafiki zangu wakubwa sana, japo Brown alisha nitongoza ila nilimwambia kuwa anipe muda kwanza, hakuwa na neno kaka wa watu alikubali kabisa na Maisha yakaendelea na mimi sasa hapo sivai tena vile vijora vyangu labda nikiwa nyumbani tu ila dukani nilikuwa navaa nguo nzuri nzuri kabisa zile za kidada zaidi ππ
Itandelea.....
Full 1000
Whatsp 0784468229.