Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

BAMTU MR SASAMPA UTAM WANGU MWENYEWEEEE AAAASSSSHH🥵💘07

3rd Aug, 2025 Views 60



Kabla Bryan hajaanza kuongea Maria alianza kujitetea.
" Lakini ulinielewa vibaya Mimi sikuwa na maana uliyofikiria...... Jordan valifika walipokuwa wamesimama
" Bryan Kuna Nini?
" Hakuna kitu unaweza ukaenda.
" Huyu dada anahitajika ndani kwenda kuhudumia watu.
" Na Mimi Nina maongezi nae.
" Kumbuka hapa ameajiriwa usiniharibie kibarua chake ingekuwa vizuri Kama ungemtafuta baada ya kazi. Dada unaweza kwenda kuendelea na kazi yako. Maria aliondoka huku akimshukuru
"Asante Mungu wangu kwakuniletea huyu malaika la sivyo sijui Lile jitu lingenifabya Nini Mimi.

Kabla ya sherehe haijaisha Bryan aliamua kuondoka . Kesho take alipofika kazini alimuita zakia ofisini kwake.
" Nataka ufanye kitu, fanya uwezavyo nahitaji kupafahamu anapoishi Maria.
" Sawa boss. Alijibu zakia alafu akaendelea kusimama, Bryan akaendelea kufanya kazi zake alipogeuka akamuona zakia bado kasimama.
" Vipi mbona umenisimamia umekuwa bodyguard?
" Hapana nilijua bado unataka kuongea.
" Nenda kafanye kazi niliyokutuma ikiwezekana jioni nipate majibu.
" Lakini napafahamu nyumbani kwao. Bryan aliacha kazi aliyokuwa anafanya akazima loptop alafu akazunguka kwenye kiti chake na kumgeukia zakia huku alimtolea tabasamu la mbali.
" Safi Sana , Sasa ongoza njia twende"
" Lakini sijamalizia Ile kazi uliyonipatia.
" Utamalizia badae. Aliongea Bryan huku alinyanyuka kutoka kwenye kiti chake na kutoka nje ya ofisi take huku zakia akiwa anamfuata huku akikimbia maana Bryan alikuwa anatembea mwendo wa haraka. Walienda mpaka kwenye gari la Bryan dereva alienda haraka na kumfungulia mlango na zakia akafungua mlango wa nyuma akapanda.
" Zakia unatakiwa kumpa maelekezo dereva ya sehemu tunayokwenda
" Sawa boss. Dereva aliendesha gari na kutoka nje ya geti ya jengo kubwa la hotel. Zakia alianza kumpa maelekezo mpaka sehemu walivyokuwa wanaishi wakina Maria . Hatimae walifika.
" Boss nyumba yao Ile pale.
" Shuka nenda kamuangalie
Zakia alishuka kwenye gari akaenda mpaka karibu na mlango na kuanza kugonga. Aligonga kwa muda bila kujibiwa na palikuwa kimnya Sana .alipoona muda unaenda akaamua kuondoka kabla hajafika lililosimama gari alimuona Dada mmoja anapita alimsimamisha na kumsalimia
Habari dada
" Salama
" Samahani naomba kuuliza. Wewe Ni mwenyeji kwenye huu mtaa?
" Ndio nakaa hapo jirani.
" Nilikuwa na shida na Maria lakini kwasasa nahisi hayupo huwa anakuwepo muda gani?
" Mbona Maria hayupo hapa muda mrefu alihama na hiyo nyumba iliuzwa.
" Ooo unaweza ikawa unapafahamu anapoishi kwa Sasa?
" Hapana Ila Kuna rafiki Yake anaishi hapo mtaa wa Pili alikuwa anaishi hapo.
" Unaweza kunielekeza?
" Sawa. Unafuata hii barabara nenda mpaka pale kwenye transformer alafu ingia barabara ya kushoto Anza kuhesabu nyumba ya kwanza kuanzia pale kwenye Kona ,nyumba ya Pili ,nyumba ya tatu Ina geti lenye rangi nyeusi hapo hapo ndipo anapopatikana Maria.
" Asante Sana . Zakia alirudi kwenye gari na kumueleza Bryan sehemu alipo Maria. Bryan aliniamuru dereva awashe gari na zakia alikuwa akitoa maelekezo.

Walipofika zakia alishuka kwenye gari na kwenda kugonga kwenye nyumba aliyoelekezwa. Alifunguliwa na Liya
" Habari
" Salama
" Samahani naitwa zakia niliku namuulizia Maria. Liya alimuangalia zakia alafu akataka kujibu Ila kabla hajafanya hivyo Bryan alifika na kusimama pembeni ya zakia. Liya akawa anamuangalia Bryan.
" Aaaa huyu ni boss wetu Mr Bryan.
" Nashukuru kwa kunitambulisha mbona Sasa afananii na tabia yake. Liya alisema na Bryan alivua miwani na kumuangalia
" Unamaana gani kusema hivyo,Ina maana unanifahamu Sana au?
" Kaka usiniletee ujeuri wako ipo kwetu hapa alafu Leo Sina mood ya kuongea kabisa. Dada huyo mtu mliekuja kumuuliza hayupo hapa aliondoka siku nyingi na Mimi sijui alipo kwaherini. Liya aliongea moja kwa moja kwa moja bila kuwapa nafasi ya kuongea chochote alipomaliza akafungua geti. Zakia alimuangalia boss wake kwa jicho kuibia. Bryan hakuongea kitu aliondoka na zakia akamfuata nyuma wakapanda kwenye gari wakaondoka . Wakiwa njiani Bryan alikuwa mbali Sana kimawaza. Baada ya ukimnya wa muda mrefu Bryan aligeuka nyuma akamwambia zakia
" Unahisi Nini kuhusu Yale majibu tuliyyopewa na Yule msichana?
" Nahisi jatuficha kitu.
" Inamaana Maria anaishi mule ndani.
" Hivyo ndivyo nilivyoelekezwa.
" Sawa Ila siwezi kukata tamaa bado Nina shauku ya kukutana na Maria, unatakiwa kufuatilia .
" Sawa boss.

Kesho yake Liya alienda kumtembelea Maria walipiga story mbili tatu Liya akamwambia
" Nisije nikasahau unajua Jana Kuna watu walikuja kukutafuta....
" Wakina Nani walikuja kunitafuta nyumbani kwenu?
" Mdada mmoja hivi na Yule boss wako jeuri.
" Nani , Bryan?
" Huyo huyo
" Khaaa hivi Yule Kaka ananitafutia Nini Mimi jamani mbona sijamlia chake?
" Inawezekana hujamlia chake Ila anataka kujifunza adabu kwa kumjibu vibaya.
" Acha ujinga kwani siku Ile nilimjibu vibaya wewe mwenyewe shahidi yeye ndio alinitukana.
" Sasa tuseme anakutafutia Nini, au anakutaka?
" Unaongea ujinga gani hakuna kitu Kama hicho.
" Wewe unasema hivyo hujui moyo wake......
" Wewe nyamaza Kama umemchoka kupiga story lala hapo. Maria alikaa anafikiria Sana jinsi ya kutatua matatizo yake na Bryan.
" Vipi mbona unawaza Sana unamfikiria Bryan?
" Liya unajua Mimi napenda Sana amani nataka kutatua hili tatizo ili niwe huru na maisha yangu.
" Wewe nae unafikiriaga ujinga Sasa huku atakupatia wapi?
" Unafikiri kule kwenu alipajuaje? Yule akitaka Jambo lake atafanya awezavyo ili litimie.
" Kwahiyo unataka kufanya Nini?
" Kesho nitavunja shuhuri zangu nitamfuata aniambie kwanini ananitafutia. Liya alikuwa kajilaza kitandani alinyanyuka haraka
" Wewe hivi unajielewa Yani unanipeleka mwenyewe kwenye mdomo wa mamba.
" Acha nijipeleke nijie moja Kama ataamua kunitafuna haya na Kama ataamua kuniacha salama na maisha yangu nitashukuru maana nitakuwa na amani

KWETU morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

BAMTU MR SASAMPA UTAM WANGU MWENYEWEEEE AAAASSSSHH🥵💘07  >>> https://gonga94.com/semajambo/bamtu-mr-sasampa-utam-wangu-mwenyeweeee-aaaasssshh-07
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 10

majario rewards 100 Comments 0
 

BLOOD MOON EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest