Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

BAMTU MR SASAMPA UTAM WANGU MWENYEWEEEE AAAASSSSHH๐Ÿฅต๐Ÿ’˜14

11th Aug, 2025 Views 41



Bryan alipigiwa na usingizi akiwa amekaa, Maria aliendelea kuuchapa usingizi mpaka kulipokucha, alifumbua macho akajikuta kalala kwenye mapaja ya Bryan Tena akiwa kafunikwa vizuri na Bryan alikuwa bado kalala. Maria alijijnyanyua taratibu kutoka kwenye mapaja ya Bryan akakaa na kumuangalia usoni akiwa bado kafumba macho.
" Kweli Ni kijana anaevutia Sana hawezi kukataliwa na mwanamke yoyote yule atakayemueleza anampenda lakini Mimi sio wa hadhi yake, siendani nae kabisa. Bryan alijitingisha Kama anataka kuamka, Maria alinyanyuka haraka akatoka nje akanjinyoosha viungo vya mwili wake na kuangalia juu. Jua ndio kwanza lilikuwa kinachomoza na ndege walikuwa wanaruka angani na wengine walikuwa wakiruka ruka juu ya miti huku wakilia kwa sauti zao nzuri. Alifurahia yake mazingira alipoangalia pembeni aliwaona wakina Jordan wakiwa wanamuangalia huku wakiwa na nyuso za tabasamu kwa mbali. Maria alijishitukia akahisi wanamuangalia vile kwasababu alilala hema moja na Bryan.
" Hii imeshakuwa shida nyingine kwaajili yao watakuwa wanajua nimelala na Bryan na siwezi kuongea kitu wakanielewa acha niuchune. Maria alijikausa akawafuata walipo.
" Habari za asubuhi.
" Salama. Wote kwapamoja waliitikia
" Bryan Yuko wapi? Derick aliuliza
" Mmmh bado kalala. Maria alimjibu Vivian akadakia
" Unamuachaje mpenzi wako akiwa kalala mlitakiwa kuamka pamoja .
" Unajua hivyo unavyofikiria sio kabisa Jana usi...... Kabla Maria hajamaliza kujitetea Bryan alitoka kwenye hema akawa anajinyoosha huku anapiga kelele. Wote waligeuka kumuangalia. Bryan aliwafuata walipo huku akiwa kashika kiuno. Jordan na Derick waliangaliana wakacheka na kugonganisha viganja vya mikono yao
" mbona unatembea hivyo umepatwa na tatizo gani?
" Kiuno kinaniuma?
" Umefanya kazi gani mpaka uumwe na kiuno ushindwe hata kutembea vizuri. Bryan alimuangalia Maria ambae alikuwa anaona aibu.
" Acheni ujinga. Maria aliondoka na kwenda kusimama pembezoni ya mto.
" Jamani naomba tusiharibiane mwenzenu ndio nabembekeza hapa alafu Maria ana aibu Sana.
" Tumekuelewa Kaka, vipi hicho kiuno umepatwa na Nini?
" Nilikuwa nautafuta ushujaa usiku nimelala nikiwa nimekaa nilikuwa namlinda mpenzi. Wenzake walimcheka .

Bryan aliondoka akamfuata Maria akamkuta kakaa kwenye jiwe akiwa ananawa uso, akaenda kuchuchumaa pembeni yake.
" Umeamkaje?
" Salama, unaumwa kiuno kwaajili yangu?
" Hapana , huwa Nina hili tatizo nikirudi mjini nitaenda kumuona daktari.
" Lakini unaweza kutumia dawa za maumivu itasaidia kupunguza maumivu.
" Ni kweli Ila hapa sina dawa yoyote ya kupunguza maumivu.
" Ninayo nitakupatia.
" Sawa. Kimnya kilitawala takribani dakika 3 ,Maria akavunja ukimnya kwa kusema
" Nisamehe kwa kilichotokea Jana usiku.....
" Hakuna haja ya kusamehewa kila kitu kilikuwa sawa.
Bryan alichota maji kwa viganja vyake viwili akaanza kunawa uso alipomaliza alisimama akamwambia Maria
" Twende tukapate kifungua kinywa pamoja. Maria alitaka kusimama Bryan akampa mkono ili amsaidie kusimama. Maria hakusita alimpa mkono wake akapewa msaada wakaongizana mpaka walipowenzao wakapata kifungua kinywa pamoja.
Bryan alikuwa anamjali Sana Maria alimpa huduma ambayo alihisi anahitaji. Taratibu moyo wa Maria ulianza kumkubali Bryan akahisi kuwa ameshasnza kumpenda Lakini Kuna wakati alihisi kuwa hakuwa sahihi Ni ngumu Sana yeye binti wa kimasikini mwenye maisha ya tabu kuwa na mahusiano na kijana billionea. Bryan hakuchoka aliendelea kumvuta Maria upande wake alipoona Maria ana wasiwasi akaamua kuongea nae ili ajue shida iko wapi .
" Maria tunaweza kutembea kidogo?
" Sawa. Maria alikubali wakaanza kutembea msituni Bryan akaanza kuongea.
" Maria kwanini hutaki kuniekewa kuhusu ombi nililokuomba Jana usiku? Maria alinyamaza na Bryan akauliza swali lingine.
" Au tayari una mpenzi?
" Hapana sijawahi kupendwa Wala kuwa na mpenzi na Wala sijui chochote kuhusu mapenzi. Jibu la Maria lilimpa matumaini makubwa Bryan.
" Basi naomba niwe mwanaume wa kwanza kupenda tuwe pamoja katika safari ya mapenzi. Bryan aliongea huku akiwa amesimama mbele ya Maria wakawa wanaangaliana mapigo ya moyo wa Maria yalikuwa yanaenda Kasi .
" Lakini Mimi siend...... Bryan aliweka kidole chake mdomoni kwa Maria ili kumzuia asiongee.
" Shiiii sipendi kusikia hiyo kauli,wewe ndio mwanamke ambae nakufikiria Sana kwenye maisha yangu. Nipe nafasi tuweze kufurahia mapenzi tukiwa pamoja. Maria alinyanyuka macho akamuangalia huku akitabasamu alafu akaangalia pembeni kwa aibu. Bryan akajua biashara ya kumbembeleza imeishia hapo alimsogeza karibu yake na kumkumbatia nae Maria alinyanyuka mikono wakakumbatiana
KWETU morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

BAMTU MR SASAMPA UTAM WANGU MWENYEWEEEE AAAASSSSHH๐Ÿฅต๐Ÿ’˜14  >>> https://gonga94.com/semajambo/bamtu-mr-sasampa-utam-wangu-mwenyeweeee-aaaasssshh-14
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

never give up harmonize
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest