Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

BAMTU MR SASAMPA UTAM WANGU MWENYEWEEEE AAAASSSSHH🥵💘20

22nd Aug, 2025 Views 24


Maria alienda alimuacha Hayden na Bibi yake akaenda sebleni kuonana na baba Yake.
" Baba nimesikia unataka kuondoka.
" Ndio mwanangu.
" Unaenda wapi Sasa? Maana Bryan aliniambia haikuwa sehemu salama. Baba Maria alitabasamu
" Naenda sehemu salama naenda kwenye nyumba yetu.
" Nyumba yetu ipi?
" Niliyoiuza
" Lakini uliiuza
" Mwanangu Bryan aliturudishia nyumba yetu, Ile Ni urithi wako Sasa. Maria alishangaa
" Inawezekana je , na mbona hakuwahi kuniambia?
" Ipo siku atakwambia . Ukiwa sawa njoo nyumbani iuone nyumba iliyokulia
Sawa baba. Waliagana baba Maria akaondoka.maria alimuangalia hakuamini Kama baba Yake amebadilika na kuwa baba mzuri.
" Huyu ndio baba yangu Sasa, Yule shetani aliempotosha akafie mbali. Mara alisikia Diana anamuita.
" Mama Hayden unapigiwa simu na baba Hayden. Maria alitabasamu akamfuata Diana akachukua simu yake. Kabla hajapokea mama mkwe wake alimuita (mama mlezi wa Bryan).
" Abeeee mama.
" Mtafutie Hayden nguo . Hayden alikuwa anaogeshwa na Bibi yake. Bryan alipoona simu take haipokekewi alipiga Tena.
" Oooh jamani hii Ni Mara ya tano anapiga na ndio kwanza asubuhi. Mama Jordan alitabasamu
" Hallow
" Mbona mtoto wangu analia hivyo? Bryan aliuliza baada ya kusikia sauti ya Hayden akilia
" Anaoga.
" Sawa , natumai hamjambo.
" Ndio tupo sawa.
" Sawa , nitakupigia baadae,kuwa makini pamoja na mtoto.
" Sawa
" Nakupenda
" Nakupenda pia.
" Mwaaa! Hili busu ni Kwaajili ya Hayden .
" Sawa nitambusu.baada ya kukata simu mama Jordan akasema
"Bryan anajali Sana.
" Hii Ni Mara ya tano anapiga simu. "Usimlaumu hayo ndio mapenzi. Hata hivyo nashukuru Sana ujio wako kwenye maisha ya Bryan imekuwa Ni baraka amekuwa kijana mzuri na mwenye furaha.
" Hata kwangu pia amekuwa mwanaume Bora Sana.
" Hii inapendeza Sana, mchukue mtoto umnyonyeshe.
Hatimae miaka ilienda Hayden akatimiza miaka miwili.
" Maria mtoto wetu ameshakuwa Sasa nilikuwa nahitaji mtoto mwingine tumpate tukiwa ndani ya ndoa.
" Unamaanisha unataka tufunge ndoa?
" Ndio nataka uwe mke wangu rasmi. Maria alifurahi kwasababu alitamani iwe hivyo.
" Nijambo hema nimefurahi kwakweli.

Baada ya kukubaliana Bryan alianza utaratibu wa kumtolea mahali na mwishowe mipango ya ndoa ilianza maramoja . Baada ya miezi mitatu walifunga ndoa . Siku hiyo ilikuwa Ni siku kubwa Sana kwao walipendeza mno kwa kuvalia nguo na vito vya thamani kubwa . Harusi yao ilikuwa gumzo mji mzima.
Macho ya Bryan hayakubanduka kwa Maria waliangaliana na kutabasamu.
" Hakika nimeweza Nina mke mke mrembo . Hayden alikuwa anamsumbua Bibi yake
" Bibi nataka kwenda kwa mama na baba.
" Hayden Baki na Mimi mjukuu wangu utaonana nao badae.
" Nataka kwenda kuwaambia kitu niruhusu niende.
" Sawa alafu urudi sawa.
" Sawa. Hayden alijipenyeza kwa watu akawakimbilia wazazi wake waliokuwa wamekaa mbele ya ukumbi. Wazazi wake walipomuona walitabasamu. Bryan alimnyanyua
" Niambie Simba wangu.
" Baba umependeza. Bryan aliishika pua ya Hayden
" Oooh Asante Sana , hata wewe umependeza.
" Hata mama yangu ni mrembo zaidi anaonekana Kama sindelela.
" Ndio mama yako Ni sindelela wangu. Hayden alicheka
" Na wewe ni mwana mfalme.
" Ndio.
" Haya nishushe nataka kurudi kwa Bibi nilimuahidi baada ya kuongea na nyie nitarudi kwake.
" Sawa mtoto mzuri. Hayden alimbusu baba yake Kisha akambusu mama yake. Bryan alimshusha Hayden akaenda kwa Bibi yake.

Baada ya sherehe kuisha maharusi waliondoka wakaenda Honeymoon kwa siku kadhaa.

Baada ya mwaka mmoja kupita Maria alianza kujihisi tofauti kwenye mwili wake, alipoenda hospital akagundulika Ni mjamzito. Bryan na Maria walifurahia Sana kwani ndio Jambo alipokuwa anataka Bryan.

Siku moja asubuhi Maria na Bryan walikuwa bado wamelala Hayden alienda chumbani kwao akapanda kitandani na kutaka kulala Katikati
" Sogeeni huko nataka nafasi hapa. Baba, mama amkeni Sasa kumekucha.
" Sasa hivi bado mapema Sana Rudi chumbani kwako. Hayden hakuekewa aliendelea kuwasumbua
" Baba kumbuka Leo Ni jumapili uliniambia tutaenda kutembea asubuhi ya leo.
" Sawa lakini nimechoka
" Lazima utimize ahadi.
" Bryan ondoka na mtoto wako mnanisumbua alafu nakumbuka ulimuahidi Sasa timiza ahadi.
" Sawa,sawa nenda najiandae uvae tracksuit nakuja.
" Yeeeeeeee. Hayden alisimama na kurukaruka kitandani huku alipiga kelele.
" Hayden toka usinipigie kelele. Maria alifika
" Samahani mama. Baba, mama nawapenda mwaaaa. Aliwabusu alafu akaondoka kwa furaha. Bryan alimsogelea Maria akambusu
" Habari za asubuhi mke wangu!
" Salama.
" Sawa ngoja nimtoe huyu bwana mdogo.
Siku iliyofuata asubuhi Maria na Bryan walienda hospital kuangalia maendeleo ya ujauzito. Baada ya vipimo doctor akamwambia Bryan
" Naona unazidi kuongeza idadi.
" Una maana gani William?
" Maria ana mapacha . Ilikuwa Ni furaha kwa wote wawili.

Siku moja Maria alikuwa anamuamsha Hayden ili aende shule lakini hakutaka kuamka mpaka alipokuwa Bryan.
" Hey hebu amka uende shule. Hayden alinyanyuka akakaa
" Lakini mnanini mbona mmenikatisha kutoka kwenye ndoto yangu ya ajabu.
" Ndoto gani ya ajabu?
" Nimeitoa nimepata dada wawili niwarembo Kama mama yangu, haya baba nibebe niende nikaoge niwahi shule.
" Hahaha wewe mtoto wa ajabu Sana.
" Baba natamani hii ndoto iwe kweli nataka kuwa Kaka.
" Itakuwa kweli na utakuwa Kaka mkubwa mwanangu. Bryan akimbeba na kumpeleka bafuni akaanza kummwagia maji.

Baada ya miezi kwenda Maria alijifungua salama mapacha wake wakike Caroline na careen. Walikuwa na watoto watatu ilikuwa Ni furaha kubwa Sana kwenye familia ya Bryan.
" Niliishi maisha yaliyokosa amani ,hasira na kisirani ndio walikuwa ndugu zangu licha ya kuwa na kila kitu, pesa pamoja na Mali lakini nilikisa kitu kikubwa na chenye umuhimu na yo Ni furaha. Nakushukuru Sana mke wangu kwa kubadilisha maisha yangu na Mimi Leo naonekana mtu mwenye furaha. Bryan akimkumbatia mke wake kwa upendo mkubwa Sana . Hayden aliwakuta
" Haiwezekani mkumbatiane wenyewe nata Mimi na wadogo zangu tunahitaji kumbatio la pamoja. Maria na Bryan wakacheka. Bryan akimbeba careen na Maria akambeba Carolyn.
" Hawya na wewe Hayden njoo. Hayden aliwagosea wakakumbatiana kwapamoja.

MWISHO

All the best.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

BAMTU MR SASAMPA UTAM WANGU MWENYEWEEEE AAAASSSSHH🥵💘20  >>> https://gonga94.com/semajambo/bamtu-mr-sasampa-utam-wangu-mwenyeweeee-aaaasssshh-20

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest