Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

BEKI TATU ANAMTAKA MUME WANGU Sehemu ya Kwanza

26th Aug, 2025 Views 29


Jina langu ni Vicky, mke wa mwanaume ninayempenda kuliko nafsi yangu. Nimeolewa na Kelvin kwa miaka mitano sasa. Maisha yetu yalikuwa ya kawaida, si tajiri kupindukia, lakini tulikuwa na furaha yetu. Niliamini ndoa yetu ilikuwa imara… hadi siku nilipoamua kuajiri mfanyakazi wa ndani mpya.

Nilikuwa nimechoka kufanya kila kitu peke yangu. Ofisini nachelewa, nikifika nyumbani nashughulika na chakula, kufua, na usafi. Kelvin alikuwa akinishauri mara nyingi:

“Mke wangu, tafuta mtu wa kusaidia kazi za ndani… sio lazima uchoke hivi kila siku.”

Mwisho wa wiki ile nilipoamua, nilipigiwa simu na jirani yangu akisema anajua msichana mzuri, mpole, na mwenye heshima anayehitaji kazi. Nilipomwona kwa mara ya kwanza, nilipigwa butwaa.

Alikuwa msichana wa miaka ishirini hivi, mrembo kuliko nilivyotarajia. Ngozi yake ilikuwa nyororo na nyepesi , midomo laini iliyopendeza, na macho makubwa ya miale yaliyoonyesha mvuto . Umbo lake halikuwa kubwa, lakini mwili wake ulikuwa na mvuto wa ajabu ule mvuto wa kimya unaoweza kumchanganya mwanaume yeyote.

“Shikamoo dada,” alisema kwa sauti nyororo iliyojaa heshima.
“Marahaba, unaitwa nani?” niliuliza.
“Na… Nasra dada,” alijibu huku akishusha macho kwa aibu.

Sikujua kwamba Nasra ndiye angekuwa mwanzo wa balaa katika ndoa yangu.

Wiki za kwanza zilienda vizuri. Alikuwa mchapakazi kweli, hakuwa na maneno mengi, na Kelvin hakumjali sana. Lakini kadri siku zilivyopita, nilianza kuona alama ndogo ndogo ambazo nilizipuuzia, nikidhani najua kila kitu.

Kwanza, Kelvin alianza kujitolea kusaidia jikoni. Mume wangu ambaye hakuwa hata na tabia ya kushika sufuria sasa alikuwa karibu na Nasra mara nyingi. Nilipoingia jikoni ghafla, niliwakuta wakicheka kuhusu jambo fulani.
“Eeh, mnaongea nini humu?” niliuliza.
“Ah, mke wangu, Nasra ananifundisha jinsi ya kupika ugali wa Kisukuma,” Kelvin alijibu kwa tabasamu lisilo la kawaida.

Mara nyingine, nilianza kushuhudia tabasamu za siri. Kelvin akirudi kazini, Nasra anamkaribisha kwa heshima kubwa, na macho yake yakimwangalia mume wangu kwa namna ambayo haikunipendeza. Nilijikaza kimya, nikijifariji kwamba labda nawaza sana.

Lakini dalili ziliendelea kuongezeka.
Nilianza kushuhudia Kelvin akionekana safi kupita kawaida wakati wa wikiendi, akivaa nguo nzuri hata bila sababu. Simu zake zilianza kuwa na siri zaidi, mara nyingi akibeba simu hadi bafuni. Na mara moja usiku, niliposhtuka usingizini, nilimkuta akichat kwa tabasamu lililoniambia kila kitu.

Siku moja nilichelewa kurudi kutoka kazini yeye mume wangu aliwahi kurudi haraka haraka alipita na kuingia ndani huku akimuita nasra lakini hakuwa anasikia Nasra alikuwa chumbani kwake kalala. Mume wangu alipiga hatu hadi chumbani kwa Nasra
Alipofungua mlango alimkuta nasra kalala bila kitu mapa na kitu viko wazi

Jasho lilimtiririka ........
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

BEKI TATU ANAMTAKA MUME WANGU Sehemu ya Kwanza  >>> https://gonga94.com/semajambo/beki-tatu-anamtaka-mume-wangu-sehemu-ya-kwanza

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
never give up harmonize
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest