Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

Bibie Sara alikuwa demu mrembo lakini mwili wake ndo ulikuwa unaingiza chenga. Alikuwa mnene haswa, hadi mtaa ukawa umempa jina Kitimoto

17th Sep, 2025 Views 2

. Hakuna aliyemshika mkono, hakuna aliyemtongoza, wala kumsifia hata siku moja. Kila mtu alimuona kama kichekesho.

Yeye mwenyewe alishazoea kuitwa majina ya ajabu, lakini moyoni kwake kulikuwa na maumivu ya kisirisiri. Aliwaza, Mbona mimi pia ni binadamu, mbona wao wanafurahia maisha yao na mapenzi yao, mimi nikibaki tu kama kipande cha sofa? Duh.

Siku moja, demu akajikaza kiume, akasema apate presha ya maisha. Akajitosa kwenda kuogelea kwenye swimming pool ya mtaa wa mabazu, akijua pengine maji yangeosha maumivu yake.

Lakini mbona? Balaa lilimkuta. Kundi la madada wa kisela, wenye roho za shetani, wakamnyemelea. Wakaanza kumrekodi live huku wakimcheka, kumshusha, wakimwambia hafai, wakimwita Titanic iliyojaa maji.

Cha ajabu zaidi, walimchukulia nguo zake zote. Yaani demu kabaki mtupu katikati ya umati, na video tayari ipo TikTok, watu wanacomment bila huruma.

Sara alijikuta anazidi kuvunjika moyo, lakini kilichowashangaza wengi, kulikuwa na jamaa mmoja pembeni, alishuhudia yote. Jamaa huyo hakucheka kama wengine. Alimuangalia Sara kwa jicho la tofauti, kama vile alikuwa anaona almasi kwenye vumbi..

Baada ya lile tukio la pool, Sara alitoroka fasta kwa taulo moja tu alilokuwa kapewa na mlinzi wa eneo. Huku machozi yakimtoka, alijisemea:
Mbona watu wana roho za paka? Mimi nimewakosea nini hadi wanifanyie hivi?”.

Akafika home, akajifungia ndani kama wiki nzima. Hakutaka kuongea na mtu, hata wazazi wake waliona kabisa mtoto wao anadidimia kisaikolojia. Lakini usiku mmoja, akatumiwa meseji isiyo na jina,
Nimeona yote. Usijione uko peke yako. Kuna mtu anakutazama tofauti.

Sara akaanza kuchanganyikiwa. Moyo ukamdanganya kuwa labda kuna jamaa kavutiwa na uchungu wake, lakini akajikaza: “Haya mambo ya mapenzi kwa mtu kama mimi ni kama kutamani mwezi.

Siku ya pili, akiwa anatoka kidogo kwenda duka la jirani, yule jamaa akajitokeza. Jamaa alikuwa mpole, anavyoongea haongei kama wanaume wasiwo wa mtaa.:
“Mimi naitwa Max, na tangu siku ile nakuona, sijakupoteza akilini. Hawa wanaokucheka hawajui dhahabu wanayotupa.”

Sara akashtuka lakini moyo ukamshtua. Kwa mara ya kwanza akaona kuna mtu anamwangalia bila huruma wala dharau. Wakaanza kuonana mara kwa mara, na polepole Sara akaanza kurudi kwenye furaha.

Sara akiwa hajui kinachoendelea, bado alikuwa anaamini Max ni msaada pekee alioumbiwa na Mungu. Jamaa alimpa faraja, akamrekebishia hata self-esteem iliyokuwa imesambaratika kama kioo kilichodondoshwa.

Follow channel zetu watssap
https://whatsapp.com/channel/0029VbAynWb7IUYY5Bfgwj2j.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Bibie Sara alikuwa demu mrembo lakini mwili wake ndo ulikuwa unaingiza chenga. Alikuwa mnene haswa, hadi mtaa ukawa umempa jina Kitimoto  >>> https://gonga94.com/semajambo/bibie-sara-alikuwa-demu-mrembo-lakini-mwili-wake-ndo-ulikuwa-unaingiza-chenga-alikuwa-mnene-haswa-ha

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest