Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

BILLIONEA CHOMOA IMEZIDI PLEASE❀ 3--4

14th Sep, 2025 Views 83


Chapter 3

Nilitaka kuchukua simu akazuia, niliamua kutulia, akanitizama nilivyonuna akaendelea kucheza game kwenye simu yake, nikaona na mimi nimkomeshe, nikamnyakua nakuizima, afu nikaitia kwenye kifua, alinitizama tu, ata hakugomba yani nilichukia nilijua atagomba alalamike lakini ata hakujisumbua ndo kwanza akaamua kulala, nilimminya kwenye kidonda ainuke, alipiga kelele ya maumivu akainiuliza unashida gani, simu si nimekuachia? Nikamuuliza kwa nini haulizi au kugomba kama nimechukua simu udai simu yako, alinitizama bila kusema kitu adi nikaona aibu, alijikaza akajisogeza atoe simu yake kifuani, nilishtuka nikamwambia wewe unafanya nini?" Nataka kuchukua simu yangu si ndo unachotaka?...

na Niligoma nakumwambia atachukuaje iko mbali, "naweza kuchukua usijali, weee koma nilimzuia akanitizama kwa muda akatikisa kichwa na kurudi kulala, nilishusha pumzi na kumshukuru Mungu make mmh, tulifika kwanza huo mjengo ni umejaa Camera, vioo yani ni mzuri ila umekaa mkao wa ulinzi mno, nilimchamba kumwambia mjengo utazani zinaishi Dhahabu ndani, hakujibu chochote aliomba nimshike hawezi kutembea bila msaada, nilimhurumia, na jeraha lilikuwa linatoa damu, nilikumbuka ni mimi ndo nimemtonesha, nikaamua kumsaidia, uku ananielekeza, io milango haifunguki bila yeye, yani nilianza kujionea mauza uza, chumba chake sasa dah! Nikama nyumba nzima ya mtu, kwanza kulivyopangiliwa kunavyonukia na kuvutia adi raha...

Nilijikuta tu nimepasifia, nikasahau kama nina mgonjwa natakiwa kumsafisha, "Sweet, niwekee dawa kwanza, afu utazunguka uikague nyumba vizuri kama umeipenda unaweza kuhamia hapa hakuna shida, niligeuka nikamtizama kwanza, nikaamua kupotezea, nikaanza kumtoa shart nimwekee bandej mpya, nilimsafisha nakumfunga vizuri jeraha lake, kulikuwa na jiko umo umo kwenye hiki chumba, nikaona nimpikie mgonjwa, nilimuuliza nipike nini make sina uenyeji na pia sijui nini anapendelea, alinambia nimchagulie chochote nikipika mimi atakula, kasoro bamia na mchicha ndo hatumii, nilipika nikamtemgea akadai hawezi kula nimlishe, kwa jinsi nilivyokuwa nimechoka na nina usingizi, nilijikuta napitiwa usingizi nikiwa namlisha...

Nililala kwa pembeni yake, hakutaka kunisumbua, alisogea ili nilale vizuri, nilimkumbatia, bila kujua nikalala kabisa...

Itaendelea..

Chapter 4

Nakuja kuamka, nakuta nimefunikwa kabisa na shuka afu niko kwenye kifua cha mgonjwa, nikiwa kwenye kutahamaki nashangaa, Frank akaingia bila hodi, alivyotuona alitoka mbio, uku anasema sijaona kitu, niliona aibu, nikajitoa taratibu kabla mgonjwa hajaamka, lakini kumbe hakuwa amelala, aliniambia nitulie nisimsumbue anahitaji joto langu, niliona aibu, nikaanza kujitetea, sijakuomba ujitetee wala sijakutuhumu, na kingine samahani nimechukua simu yangu bika ridhaa yako...

Nilishtuka kachukua chukuaje na ilikuwa kwenye kifua, nilimgeukia na umenichunguria? Hakujibu kumuuliza nilichomuuliza badala yake akasema nimuache apumzike kachoka,nilitulia ila kwa shida sana, nilivumilia halafu akapitiwa usingizi, amekuja kuamka mimi nishatoka niko nacheza game, nikiwa pale Frank alirudi tena akabisha hodi nilimuitikia uku naona aibu, alifika nakudai wenzake walikuja kunitafuta, ameshawaekeza, afu akaja na mzigo akadai kaagizwa na kaka ake, akiamka nimpe, kumbe alikuwa kashaamka, alimuita mdogo wake, Frank alisogea alivyoagizwa, wakaanza kupiga story... akatia

Frank akamtizama kaka ake akaacha na maelekezo ya dawa zingine,akaniuliza mahitaji ambayo hayapo jikoni akalete, Ethan akamwambia, "hupaswi kumuuliza wewe aisee, nikashangaa, Frank akacheka nakusema hatauliza tena tuulizane wenyewe, nilibaki nawashangaa tu...

Ethan aliniuliza nahitaji nini uko jikoni, niliingia nikaandika ninavyoitaji nikampa Ethan, Ethan alitabasamu nakusema uko smart sana, sikujibu chochote nilikaa tu kimya, make siwaelewi kabisa, Ethan alipitia akakuta nimeandika na pipi, alicheka akatoa ule mfuko aliokuja nao Frank akanipatia nilifungua na kukuta mfuko wa pipi, nilifurahi mno, nikamshukuru kama sina akili vizuri....

Wote walicheka jinsi nilivyofurahi na kushukuru kisa pipi, nikioga na kuvaa nguo zililetwa, nikaingia kupika chakula cha mchana, nilipika tukala, kisha Frank akaaga anaingia kulala, na mimi nikauliza room yangu nilale, Ethan hakujibu akakaa tu kimya, nilovyomuuliza tena akanambia "kwani kitanda hiki hakitoshi?...

Nilimtizama nakumwambia wewe ni mwanaume hatuwezi kulala chumba kimoja, alijibu, "ni mwanaume lakini saiv anaumwa hawezi kufanya chochote, hivyo nilale tu kama mwanzo yeye hana shida kabisa, nilichoka, nikaona uyu analake jambo ngoja...

Itaendelea...

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

BILLIONEA CHOMOA IMEZIDI PLEASE❀ 3--4  >>> https://gonga94.com/semajambo/billionea-chomoa-imezidi-please-3-4

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest