Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94

*BINTI MPELELEZI* SEHEMU YA... 19 Na

19th Jul, 2025 Views 13

*BINTI MPELELEZI*

SEHEMU YA... 19
Na
Mamuh Mohd
(0716730000)

Tulipoishia......

Wote walishangaa hata malkia na kijakazi wake walibaki pozi limewaisha jumba bovu limewaangukia......

SONGA NAYO......

"Hapana wewe umekuwaje? Mbona unaongea vitu ambavyo havipo kabisa kwani mwanzo tuliongea nini?"
Aliuliza malkia huku macho yamemtoka,
" Hapana malkia siwezi kusema uongo tafadhali".
Sultan alimtazama mkewe na kumuuliza,
" Bado una nafasi ya kunionesha hicho ulichotaka kunionesha mkewangu"
Malkia alibaki kimya asijue ajibu nini.
Sasa wakati huo Yenah na Kosho walianza kuondoka zao wapofika barabarani kosho akamshika mkono Yenah na kumwambia,
"Walinipiga na picha nikiwa mtupu kabisa na alipewa yule dereva sawa tumemaliza huku vipi kuhusi picha? "

" Picha una uhakika anazo yule?".

" Ndio alipewa na malkia"
" Sawa alipiga kwenye simu au camera?"
"Alikuwa na camera ndogo"
"Sawa cha kufanya hapa jitokeze wewe umzubaishe mimi nitatokea nyuma kumdhibiti".

" Sawa".
Basi walipokubaliana kosho akajitokeza akawa anakimbia ndipo Dereva yule kumuona akamkimbiza kwani alihisi ametoroka.
Kosho kuona anakimbizwa akajiangusha makusudi ili dereva yule amkamate ni mpango wao.
Basi kweli dereva yule alimkamata,
"Wewe unatoroka umewakimbia Sultan na malkia eti?"
"Nisamehe nakuomba".
Dereva yule akamshika kosho amrudishe kule ndipo aliogeuka nyuma alikutana na teke la usoni kutoka kwa Binti Yenah mpaka akaanguka chini damu zikimtoka mdomoni.
"Haaa!! Wewe ndio maana umekuwaje umemsaidia huyu au? ".
Yenah hakutaka kusubiri alianza kumshushia kipigo ngumi za kutosha mpaka akalegea ndipo Yenah akaanza kumpekua mfukoni kweli walipata camera ile.
Kosho alifurahi kweli aliona amepata mwanamke sio wa michezo haraka Yenah akamvuta dereva yule kutokana barabara mpaka msituni upande wa pili tofauti na ule waliopo Sultan.
Alipofika akamuamuru nae avue nguo dereva yule alilia kuomba msamaha lakini kosho akawa mstari wa kwanza umvua nguo kisha wakampiga picha za kutosha kisha Yenah akamwambia,
"Sasa nakuacha amua moja kuwa Upande Wangu au hizi picha na video zisambae kazi kwako sikukatazi ukiamua kusema sema ni mimi Yenah"
" Nakuomba usisambaze hizo picha nina mke na watoto".

Yenah hakujali taratibu walianza kuondoka wakiwa na Kosho tena kwa kupitia njia za msituni mdogo mdogo.

Malkia alikosa ushahidi wewe ndie yywakarudi nyumbani walimkuta dereva wao akiwa ameshavaa nguo zake ndie aliwarudisha nyumbani.
Kufika Sultan alikasirika sana lakini kabla hajaingia ndani mkewe alimshika mkono na kumwambia,
"Sultan Wangu najua hauniamini lakini upo ushahidi mwingine wa mwisho kukuonesha kuwa tulikuwa na kosho ndie alitwambia Ukweli utanisamehe japo ilinibidi nimpe adhabu ili aniambie ukweli".
Malkia akamgeukia dereva na kumwambia,
"Naomba ile video na picha za kosho nimuoneshe sultani".

Dereva yule alibaki anaangalia chini kwani amepigwa kaumia akatingishwa kichwa,
"Video gani unaongelea malkia mbona sina kitu chochote".

Malkia alizid kushangaa hakuamini macho yake Sultani hakutaka tena kusubiri aliingia zake ndani.
Malkia alimfuata dereva yule na kumwambia,
"Niambie umepatwa na nini hadi wewe kuna kitu si ndio?"
"Hapana hakuna kitu chochote malkia".

" Anhaaa sawa".
Malkia akaingia zake ndabi huku analia ndipo Dereva yule alimtazama hana jinsi kutokana na mkwala aliopewa na Yenah.

Basi kesho yake Asubuhi Sultan aliamuita gavana wake na Mkewe pamoja na Yenah na vijakazi wao.
"Nimewaita hapa mshuhudie maamuzi Yangu... mkewangu malkia amenidanganya akisema atanipa ushahidi lakini hajanipa anajua kila kitu siwezi kuweka hapa wazi lakini tulikubaliana kwamba alishindwa kunipa ushahidi nifanye vile navyotaka sasa naamua kwamba Nataka siku tatu hizi muandae harusi namuoa Yenah kama mke mdogo kwa kuwa ana ujauzito wangu".

Malkia zunaifah alishangaa,
" Hapana mmewangu usinifanyie hivyo nakuomba tafadhali huyu mwanamke ni nyoka niamini".

Alilia lakini haikusaidia Sultani hakutaka hata kumsikiliza tena hapo Maamuzi ni yake akubali au aachie ngazi kwa maana aachane na Sultan.
Hata Yenah hakuwa na nia ya kuolewa na Sultan sababu anajijua hana mimba lakini kwa ajili ya kumkomoa malkia anaemfuatilia nyanja zake alikubali na kupanga akutane na Kosho wajadili hilo.

Malkia alipata homa akawa sio wa kula wala kunywa ndipo kijakazi wake wa karibu enifa akamwambia,
"Malkia usilie huwezi kukata tamaa mapema kiasi hicho siku tatu ni nyingi kabla ya harusi kumthibitishia Sultan kuwa huyu mwanamke ni mbaya nina wazo"
" Wazo gani?"
" Haiwezekani wale vijana na Dereva wkaugeuke na kosho akawa hayupo huoni labda kuna namna Yenah kawadhibiti? Cha kufanya na wewe wadhibiti waseme ukweli....huyu dereva ana mke na watoto tuwateke watoto wake kisha mtishie atasema ukweli wote kama Yenah kweli kuna kitu amefanya au laa?".
Hata malkia alihisi kupona gafla baada ya kusikia mpango ule madhubuti......je watafanikiwa?

Tukutane Sehemu ya 20

*BINTI MPELELEZI*

SHEHEMU YA... 20
Na
Mamuh Mohd
(0716730000)

Tulipoishia.....

Hata malkia alihisi kupona gafla baada ya kusikia mpango ule madhubuti....

SONGA NAYO.....

"Enifa hakika haujawahi kuacha kuwa upande wangu hata siku moja nakuahidi tukitiki huu mpango tukahakikisha Yenah amefukuzwa hapa nitakupa zawadi nzuri sana kijakazi wangu mtiifu"

" Nimekula kiapo kukusaidia Katika shida na raha usijali tupo pamoja".
" Sawa naomba chakula walau nile maana nina njaa"
" Usijali malkia wangu vyovyote utakavyo".
Haraka enifa akaondoka na kwenda jikoni kuandaa chakula.

Wakati huo walifika wazee wawili ambao ni ukoo mmoja na Sultan yaaani mabibi zao wa zamani.
Wazee hao walikuwa wakiishi hapohapo katika himaya ya Sultan ANARUDI lakini kuna kinyumba kidogo kimejengwa pembezoni kabisa ndipo wanaishi wazee hao.
Walipokelewa na kijakazi wa ndani humo,
"Karibu sana wazee wetu"
"Asante tunahitaji kuonana na Yenah bi harusi"
Sawa kijakazi yule akawaelekeza mpaka chumbani kwa yenah na kumgongea.
Yenah akaenda kufungua mlango na kukutana na wageni hao.
"Habari yako Yenah sisi ni wageni wako tunahitaji kuongea na wewe kama hautojali".

Yenah alishangaa lakini akawakaribisha na kuwasikiliza wamasemaje.
" Sisi ni miongoni mwa wanafamilia hii ya Sultan na tumekuja hapa kukuandaa tumesikia kuwa ni bi harusi unaolewa hivi karibuni"
" Ohhh sawa karibuni".
Yenah alifurahi kusikia vile akajisemea moyoni,
" Hapa napaswa kuwa karibu na hawa wazee naweza kupata chochote Katika upelelezi wangu na kujua umiliki upo wapi".
Alijisemea Yenah na kutulia kuwasilikiza wazee wale ambao walikuja kumfanyia Maandalizi ya kuishi na mume yaaani kwa lugha ya kiswahili ni (kungwi) Mtu maalum wa kumuandaa bi harusi.

Wakati huo sasa mipango ya malkia ilikamilika ambapo kuna Walinzi wengine walienda mpaka nyumbni katika familia ya dereva samwel na kuwateka kuwatishia silaha kisha polepole wakawaamuru kutoka ndani na kuingia kwnye gari kifuatacho wakaenda kuwafungia sehemu ya mbali mama na wanae wawili.
Walipomaliza ndipo alipigiwa simu dereva yule na namba ya simu ngeni,
"Haloo Nani mwezangu?"
"Haina haja ya kujua unaeongea nae lakini familia Yako ipo matatizo na usipofanya hivi navyokwambia familia Yako itaangamia? "
" Ujasemaje wewe? Unaongea nini wewe?"
"Nisikilize nachokwambia wacha kuwa mkali sawa fuata vile navyokwambia nenda kamuambie sultan ukweli ambao umeuficha kaa sivyo labda familia yako inaangamia muda si mrefu utapokea taarifa mbaya na usimwambia mtu yoyote fuata maelekezo".
Kisha simu ile ilikatika.
Dereva samwel alishangaa sana hakuamini kile alichokisikia haraka akakimbia na kurudi nyumbani na alipofika kweli alikuta familia yake haipo zaidi kuna ujumbe ambao ulisomeka,
"Sema ukweli utukukomboe familia yako".
Dereva yule alilia na kupiga kelele hajujua aanzie wapi na amalizie wapi lakini alipotuliza lili akili aliweza kujua kuwa kwa vyovyote vile aliefanya haya yote ni Malkia kwanza akaona arudi akaonanae na malkia.

Wakati huo Malkia zunaifah habari zilimfikia kuwa kuna wageni wale wazee wamekuja kuzungumza na Yenah.
Malkia alijua wanachozungumza nae japo kilimkwaza sana.
"Nafahamu wale wazee hata mimi kipindi kaolewa walikuja na kunipa somo naelewa naumia sana inabidi harusi isikamilike ma Sheria ya hawa wazee wakimaliza kumfunda anatakiwa awaandalie chakula vipi ameshaandaa?"
" Hapana"
" Sawa nendeni jikoni mkaweke sumu kwenye viungo Chochote ambacho mnahisi Yenah atakitumia wekeni wale wazee wafe aanzie kulaumiwa hapo huku dereva akija kusema ukweli tuone yenah atasalimika wapi hapo".
Malkia alimpa maelekezo kijakazi wake na kumpatia Sumu akafanye Kazi yake.

Kweli wakati huo Yenah akiendelea kupewa mafunzo ya kuwa mke wa Sultan na walipomaliza wazee wale wakamwambia Yenah,
"Sheria yetu sisi tukishamaliza kukupa mafunzo utuandalie chakula walau ugali tu"
" Ohhh sawa msijali naandaa nahitaji kuwa karibu zaidi na nyie wazee wangu".
Basi Yenah akasimama na kwenda jikoni kuandaa chakula.

Wakati huo Dereva alifika kwa malkia Zunaifah kwani aliomba kuonana nae,
"Malkia una roho mbaya sana umefanya nini kwa familia yangu hauna hata huruma familia Yangu imekosea nini?".
Malkia alikasirika alimnasa kibao dereva yule kisha akawaita vijakazi wakiume wamkamate derava yule na kwenda kumfungia kwa otovu wa nidhamu kumpazia sauti malkia.
Samwel alianza kulia huku akiomba msaada kwa malkia amuachie yupo tayari kusema Ukweli lakini malkia Zunaifah aliona kwanza amuache apate shida ili iwe rahisi kusema ukweli.
Samwel alilia sana na wakati huo Yenah alikuwa jikoni akiandaa chakula lakini akasikia kelele zile ikabidi amuulize kiajkazi wake nae aliepewa awe nae karibu,
"Nani huyo?"
"Ni dereva wa malkia zunaifah sijui amefanya nini anapelekwa kufungwa inaonesha ametenda kosa".
Yenah Alishangaa kusikia vile alitamani akajue nini sababu lakini kwanza ilimbidi amalize kuandaa chakula.

Yenah aliivisha chakula na kuwapelekewa wazee wale kwa nidhamu zote hakujua kilichoendelea lakini wakati anapeleka malkia zunaifah na kijakazi wake enifa walikuwa wamejificha mahali wanamtazaka kuonesha kweli wameshaweka mpango wao walioupanga.
Yenah hajui hili wala lile aliwanawisha mikono wazee wale na kuwapa chakula kile nao wakaanza kula.
Walati huo Yenah aliwaaga kidogo anaenda kuwaletea matunda kumbe nia yake akafuatilie ajue derava yule amepatwa na nini hivyo akawaacha wageni wale wakiendelea kula chakula.
Walikula lakini mala gafla baada kama kama ya dakika 10 wakaanza kuhisi......

full 1000.
what'sapp no 0716730000.

Sijui itakuwaje?
Tukutane sehemu ya 21.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

*BINTI MPELELEZI* SEHEMU YA... 19 Na  >>> https://gonga94.com/semajambo/binti-mpelelezi-sehemu-ya-19-na
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
karibu msagala furniture
karibu msagala furniture

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MKEKA 03

majario rewards 100 Comments 0
 

.BABAMKWE epsd 19.

majario rewards 100 Comments 0
 

ALINIINGIA BILA IDHINI

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE..17..18

msagala rewards 100 Comments 0
 

bei sawa na bule

majario rewards 100 Comments 0
 

BABAMKWE epsd 16

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest