Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

BINTI WA MTUNZA BUSTANI😍 Sehemu ya 4

23rd Aug, 2025 Views 20



Ibra akiangalia Ile picha Kisha akamuangalia Tena Munira na kumuuliza
" Bado unataka kuangalia? Munira alitingisha kichwa kwa kukataa Ibra aliirudisha Ile picha ilipokaa Kisha akachukua laptop yake na kuondoka alipofika mlangoni Munira alitoka kwa mwendo wa kasi na kumgonga Ibra
"Hey wewe vip unashida gani? Munira hakugeuka alienda moja kwa moja chumbani kwa bibi
" Haaa huyu binti yupo sawa kweli Yani amenigonga na Wala hajali. Munira alifika chumbani kwa Bibi hukubwakiwa na wasiwasi alijua Ibra anamfuata
" Bibi Mr tattoo nimkali?
" Nimesha kwambia acha kumuita hivyo muite Ibra
" Sawa
" Kwani mmemkorofisha
" Akaaaa nimeuliza tu.
" Hana shida na mtu ambae hajamkorofisha
" Leo sikai mpaka jioni nataka kuwahi nyumbani.
" Kuna Nini mpaka uwahi
" Mimewakumbuka marafiki zangu naenda kuwatembelea. Munira alimfuata baba yake akamuaga wakati anaondoka Ibra allimuona akamuita
" Hey Munira niletee maji yakunywa. Munira aliingia ndani akatoka na maji akamtengea na kuondoka alipiga hatua mbili Ibra akamuita
" Mbona una haraka unaenda wapi?
" Nawahi nyumbani
" Kuna Nini mbona Leo mapema
" Nimepanga kwenda kuonana na marafiki
" Kumbe na wewe una marafiki? Munira alirudi akakaa
" Mr tattoo unamuonaje kwani unahisi siwezi kuwa na marafiki.
" Mr tattoo ni Nani? Munira alizuga Kama vile hajasikia alivyoulizwa
" Marafiki ninao Tena wengi Sana na hivi ninavyoshinda huku watakuwa wamenimiss Sana leo nimewaahidi tutakuwa pamoja tutabadilishana mawazo tutafurahi na kucheka Ibra alinogewa na maongezi ya Munira akaacha kazi alivyokuwa anafanya na kumsikiliza muda ilizidi kwenda Munira alishituka
" Ina nimejisahau muda umeenda mpaka nipate usafiri si nitafika usiku Mimi naenda. Aliongea Munira huku akisimama
" Hebu subiri nitakupeleka.
" Oooh afadhali maana ningezidi kuchelewa wanganilaumu Sana. Ibra alinyanyuka akaenda chumbani kwake akabadilisha nguo akavaa nguo za mazoezi maana alikuwa anaelekea gym alipotoka wakapanda kwenye gari Ibra akafungulia redio Kuna mziki ulikuwa unaimba
" Huo mziki nakupenda Sana ongeza sauti kidogo. Ibra aliongeza Munira aliomba kwa kuufwatisha ule mwimbo Tena aliomba kwa hisia huku akifumba macho Ibra alimkata jicho huku akiendelea kuendesha gari.
" Usisahau kumuelekeza unaposhukia.
" Kwani si unanipeleka mpaka nyumbani? Ibra hakujibu alimuangalia Munira akaona aibu
" Kama utapenda lakini . Walipofika mbele kidogo Ibra alimuuliza napita kulia au kushoto.
" Kulia, kulia. Walipofika mbele kidogo alimuomba Ibra amshushe hapo
" Nishushe hapa wakina Samira wale pale wanakula mihongo. Ibra alisimamisha gari Munira akashuka Asante Mr t... Kabla hajamaliza Ibra alimkata jicho ikabidi anyamaze Ibra akawasha gari na kuondoka.
" Mmmh sijui ndio kakasirika aah atajua mwenyewe. Mashoga walimuona wakamuita aliwafuata na kuwakumbatia.
" Jamani Munira unatabia mbaya kwanini tumekusubiria kwenu mpaka tukachoka tukaamua kija kupata mihogo na viudambu udambu.
" Poleni lakini msijali ndio nimeshafika.
" Hebu tueleze Ile gari iliyokuleta ni yanani?
"Nyie nae wambea kumbe mmeniona mwenzangu ningari ya Mr tattoo mtoto wa boss kanichelewesha ndio kaamua kunileta.
" Mmm sio mpenzi wako kweli
" We nae umbea umekuzidi muone na komwe lake hebu twendeni nikale kachori
" Kwani kuuliza dhambi
" Samira usinichimbe ukataka kuujua undani .
" Sio Samira hata Mimi nataka kujua pengine mwenzetu umeopoa mabosi huko ndio maana hushindi mtaani. Furaha alimwambia
" Hamna lolote shoga zanguni watu wenye pesa wanapendana wenyewe kwa wenyewe Mimi kapuku mtoto wa kijakazi ataniweka wapi Mimi nitapata wauswahilini mwenzangu Basi .
" Lakini mapenzi hayachagui yawezekama siku moja zali likakuangukia.
" Sema Mr tattoo ni mzuri jamani ukimuangalia hutamani kuacha kwanza akiwa anakuja inaanza kusikia harufu ya marashi alafu yeye ndio anafuata waliongea mpaka kigiza kilipoingia Kila mtu alienda kwao

Zilipita siku mbili Munira hakwenda nyumbani kwa kina ibra. Siku ya kwanza Ibra alipotoka kazini alienda chumbani kwa Bibi yake na kumkuta kajilaza alimsalimia Kisha akauliza
" Huyu mcharuko Yuko wapi?
" Leo hajaja Yani mimepooza mwenyewe huwa ananichangamsha na maneno yake mengi huku akinikanda miguu yangu.
" Kesho anaweza akaja. Siku ya pili yake pia hakuja Ibra alitamani kumuuliza mzee mvungi akaona Haina haja wakati anaenda gym alienda mpaka pale alipomshusha akapaki gari lake pembeni.
" Hapa hamna hata dalili ya kumuona sijui namuuliza Nani na sikuile nikifanya makosa sikumuuliza nyumbani kwao ni wapi. Mara alipita Dada mmoja alimsimamisha akamsalimia
" Samahani nilikuwa mamuulizia Dada mmoja anaitwa Munira anaongea Sana.
" Munira mdogo wake Sara.
" Sijui Kama anandugu anaitwa Sara Ila yeye ni muongeaji sana
" Itakuwa ni huyohuyo hapa mtaani Munira niyeye tu Sasa nenda mpaka pale mbele kwenye Ile nyumba yenye duka nyumba inayofuata ndio kwao.
" Ok Asante Sana Dada. Ibra alipanda kwenye gari akaendesha mpaka alipoelekezwa alipofika alimkuta Munira kakaa kwenye mkeka na marafiki zake akabisha hodi.
" Karibu. Aliitikia Munira Kisha akageuka kuangalia anaebisha hodi alipomuona Ibra alishangaa
" Haaa Mr tattoo

Ofaaaaa full 1000
Whatsapp 0755090082.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

BINTI WA MTUNZA BUSTANI😍 Sehemu ya 4  >>> https://gonga94.com/semajambo/binti-wa-mtunza-bustani-sehemu-ya-4

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest