Tulipata taarifa, na mama Najma alitangaza vita na Mama mkwe na Naseer, ilibidi Naseer amtumie majibu yake na hali yake wakati yuko India kwenye matibabu kwa ajili ya Najma alimtumia na ujumbe niliugua miezi 6 Niko India kwa ajili ya binti yako ulitaka nirudiane nae tena nife ama lengo lako lilikuwa nini? Alituma pia kwa mama ake, mama mkwe hakujua kama mwanae aliambukizwa ugonjwa mkubwa vile yeye alijua tu ni mambo ya afya, imegoma, alichoka, ila tamaa ndio ilimjaa akawa hajazingatia hilo akaendelea na lawama, mama Najma alikaa kimya hakujibu chochote...
Najma yeye alivyoona ameshazagaa aliamua kuchukulia poa nakuamua kufanya sasa kama kazi kwanza akawa anajiamini pesa ya matibabu atakuwa nayo, hatapata shida, mama ake alimsihi aaache lakini aligoma, kabisa, ndo akazidi zaidi, hali ikabadilika, wazungu hawakumpeleka hosptal wakamtupa, aliokotwa kama bahati tu, mama ake alikuwa huko akatafutwa na kuelekezwa akaingia tena mfukoni kutibu, safarii hii kizazi ilibidi kitolewe. kabisa ili yeye apone, na akakutwa kaathirika...
Mama ake alilia mno, alijiuliza kakosea wapi aliamua kimpeleka India wamtibu na ubongo huenda ndiko shida ilipoanzia, kweli waligundua anatatizo pia kwenye ubongo ilibidi afanyiwe oparation mama wawatu alianza kuyumba. kiuchumi kwa ajili ya kumuuguza mwanae akaamua kuuza baadhi ya mali zake, alifanikiwa, operation ikapita vizuri, akaanza kufanyiwa ushauri, mama ake ilibidi arudi kupambana kutafuta hela na kumuacha mwanae hosptal anatibiwa akili, na ushauri, ilichukua mwaka. mzima, apo mimi nilikuwa tayari nimeshajifungua katoto kangu ka kike, aisee furaha iliongezeka...
Elham alifurahi kapata mdogo wake, alikuwa anatamba kila kitu ni mdogo wangu hawezi ongea maneno matatu.bila kumtaja mdogo wake, ilipita miaka 6 apo tumeshasahau kama tuna vita, na Najma alikuwa kapona kawa mtulivu ila alikuwa kaathirika, walitutafuta sana wakatupata na kuomba angalau tu tusimtenganishe na mwanae...
Tulimwambia tu awe na amani hakuna tatizo alikuja tukampokea vizuri japo hofu ilikuwepo, Elham alikuwa kawaida tu, nilianza kimshauli asimchukie mama ake hakuwa sawa, taratibu Elham alinielewa, akaanza kucheka na mama ake, baada ya muda akawa ameondoka, mwanangu alifunga mwaka nikajikuta nina mimba tena, ilibidi tutafute dada wa kazi make safari hii nilikuwa naumwa umwa kila kukicha, tulitafuta mdada tukapata, mama akanisisitiza niwe makini mno, hana imani kabisa na wadada, nilimwambia tu hawafanani awe na amani, alinielewa japo kishingo upande alionekana kabisa hajaelewa kitu...
Mdada alikuja alikuwa anaitwa chausiku, alikuwa mchapakazi, mcheshi yani nilijikuta nashukuru Mungu nimepata mtu sahihi, tulikaa nae miezi mitatu, akaanza kubadilika, ni anajipenda sio kama alivyokuwa, akaanza kuvaa vitu vya gharama, nikajua tu kapata bwana nikawa nampa siku moja kwa ajili ya mapumziko....
Alifurahi mno, na kila wiki lazima atatoka io siku ya off nakurudi jioni, sikutaka kumfatilia muhimu yangu yanaenda, nilikuwa tu makini na wanangu, nikawa sitaki mazoea yazidi ikaja kunikuta kama yangu, nikawa nawaombea wanandu Dua mno, Δ°lipita miezi nikajifungua, nilivyojifungua tu,mama alikuja nikashangaa chausiku anaacha kazi, alidai anamimba, sikumzuia uzuri nimeshashusha na mama kaja...
Itaendelea.....
Offer offer offer
Soma yote kwa sh 500
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments