*SEHEMU YA KUMI NA MOJA*
Walikubaliana na kuanza mchakato wao, Husna alikuwa mzuri sana kwa kuigiza,ni ngumu kujua kama ni mtu mbaya, walipambana kwa miezi kadhaa, mpaka wakamnasa Naseer, upande wangu niliweka sawa na familia yangu, na nikawa binti bora sana, nikarudi chuo kuendelea na masomo, niliomba mda Naeer asiniguse kwanza nimalize masomo, alikataa na kusema naweza kusoma na huku nahudumia ndoa, nilikuwa naogopa sana mimba, akaniomba nitumie uzazi wa mpango, yeye hawezi kujizuia...
Niliamua tu kufanya hivyo, sikutaka ukaribu na yeyote niliewahi kumhudumia, nilikuwa nawakatia, nilisemwa sana, ila nikajikaza nakuendelea na maisha, nilianza kuishi na Elham mtoto wa Najma, nilimlea vizuri na kuwa nae makini sana, alitokea kunipenda, na kuniita mama, alikuwa na miaka 7 sasa....
Nilikuwa namsaidia home work, alikuwa smart sana kama mtu mzima, siku moja Naseer alirudi nyumbani akiwa anaogopa alipiga magoti na kuniomba nimsamehe kafanya kosa lakini hakudhamilia, nilishangaa na kumuuliza kabla sijamsamee kafanya kosa gani, alisema kampa mwanamke mimba na ni yatma anajihisi hatia anaomba ruhusa amuone, kuepusha hio dhambi, nilichoka nikahisi mwili wote umekufa ganzi...
Nilijikuta nalia tu nakumjibu sawa, alinisogelea ili kunimbembeleza lakini sikutaka mazoea, nilianza kumuona Naseer kama mwanaume wa ajabu sana, nilimchukukia mno, nikaamua kuangalia, ataoa wangapi, huenda anampango wakuoa dunia nzima, nilijikuta nasahau ata mafundisho ya dini, mapenzi yanauma jamani, kumbe kina Najma walivyoona kumpata kawaida inakuwa ngumu walimuendea kwa mganga, na wakafanikiwa make mimi sikuwa mtu wa ibada kivile nilikuwa kawaida tu, naswali kawaida tu sio kivile....
Hivyo ilikuwa lahisi tu kwao kufanya ubaya na wakafanikiwa, walianza kucheza na akili yake,kwa madawa, akawa hanijali tena mimi, anaweza maliza mwezi hajaja kwangu, yuko kwa Husna, na ndoa hata sijui ilipitaje, sikutaka kufatilia, na nilipuuza na kuona ndivyo alivyo, kumbe ndio maana Najma alikuwa anachit, huenda ndio tabia yake, na nikiunganisha na story na watu kuhusu ndoa nikaamini kumbe ndo tabia zao tu, sikushtuka kabisa kama kuba nguvu za ziada zinatumika...
Mimi niliendelea kupambana kivyangu uzuri ada nililipiwa ya miaka mitatu yote, hivyo ni mahitaji tu ndo yalikuwa changamoto, nikaamua kufanya biashara ya urembo apo apo chuoni, Najma na Husna walianza kulala na Naseer chumba kimoja na hata Naseer hakukataa, alikuwa anatembea nao wote kwa pamoja, analala hoi, mpaka kazini akaanza kuyumba, kampuni zikaanza kuyumba mno, ilibidi mama ake aniombe nisimamie, anahisi mwanae hayuko sawa...
Nilikuwa nauzoefu kiasi, ilibidi nianze kusimamia na kublock baadhi ya acount za pesa ili asitoe apo alikuwa anesahau kabisa kuhusu kazi nimezi minne hajakanyaga kwenye kampuni yake, alivyokosa pesa ya kula bata na wake zake akaja, alimkuta mama ake na mimi, ilibidi mimi na mama ake ndio tusimamie, mimi nilitoka nikawaacha mtu na mama ake wanazozana, mama ake alisema kachukua kampuni yake na riba ya hio kampuni ya vitambaa hivyo kampuni zote ziko chini yake kuanzia leo Naseer sio CEO, Naseer alipanic nakusema haiwezekani, aliondoka akaenda kwenye kampuni yake nyingine ya maji, aliamua kuitumia hio kwa sababu mama ake alikuwa haijui...
*SEHEMU YA KUMI NA MBILI*
Alianza kulandama hio, akawa anatoka na wake. zake, wanamzimisha, wanachukua pesa wanaenda kufanya yao wakimaliza wanarudi na kumdanganya, mimi n mama mkwe tulianza kupata mashaka sana, tulihisi kuna tatizo, tulianza kuomba dua, tulifunga, tulipambana kufanya dua, ilifika hatua tukaanza kukata tamaa kabisa, lakini tunajikaza tu, niliogopa kusema kwa mama mkwe nimekata tamaa, kwa sababu ataniona mkwe mchovu nikawa najikaza, Dua ilijibu aiseee...
Naseer alikuja nyumbani kachoka, hajielewi, nilimuekea maji akaoga nikampa chakula akala, akalala, alilala, siku nzima, simu yake si ikaaanza kuita kucheki mpigaji imeandikwa bi mdogo, nikaachana nayo ilivyokata si ndo nikaona picha juu ya profile ya simu, ni Husna na Najma, nilishtuka ikabidi nianze kuikagua simu, nikakutana na picha za ajabu nyingi, aisee nilichoka nilichukua picha zenye angalau nikahamishia kwangu nikamuomba mama angu mzazi aje kwangu, alikuja....
Nikamuonesha picha na kumsimulia kila kitu, mama alichoka akaniuliza Thuraya, unapitia yote haya huniambi, unaakili kweli wewe mtoto?, mimi ndio msiri wako, hakuna mtu atakae kuelewa zaidi yangu, mama mkwe wako anaweza kukugeuka lakini mimi mama ako siwezi, unatatizo niambie mapema tujue cha kufanya...
Mama alisema tuzidishe dua, na nisiswali kwa kubip natakiwa kila siku niswali kwa ajili ya ndoa yangu, nimombee mme wangu, wavurugaji nje ni wengi, wakimshindwa kawaida wanakuja kivingine, watatia ata madawa kwenye macho,mme wako akiwaona tu ananasa, kama humuombei Dua mmeo, ndio anaenda hivyo, hasara kwako...
Nilimtizama tu mama, alinyamaza kwa muda na kusema huyu Husna kuna kitu anakitafuta kwenye familia yangu sio bure, sasa acha tushirikiane karma itampa anachokitafuta, naomba usije ukawaza kwenda kwa waganga, tulia kabisa, Dua inanguvu mno itasimama na wewe,niliongea vingi na mama kisha akaondoka muda wote huo. Naseer alikuwa hajaamka, nilimtafuta shehe akaja nikampa maelezo kiasi aliandaa maji akayafanyia dua, tukasoma na kisomo, kisha nikamuamsha, mengine nikampa akanywa, mengine akaoga....
Alianza kulia, akasema haelewi nini kinaendelea kwenye maisha yake, nilimtuliza nakumwambia asijali tufanye ibada kila kitu kutakuwa sawa, alikuwa hakumbuki mambo mengi mno, ilibidi tu nimsimulie mwanzo mwisho wa kile ninachokijua, alishtuka, akachukua simu yake, akawasha na kuangalia adi video za ajabu ajabu aisee, aliwaza mno, alinitizama nakusema kwa hapa alipofikia mali zake hapaswi kuwa nazo...
Alilazimisha, kuniandikisha mimi kila kitu ili lolote likitokea mtoto wake na mimi tusipitie wakati mgumu, awa sio watu wa kawaida, alikuwa na kiwanda cha mabati, shule vyote aliniandikisha mimi, hata mama ake hakumshirikisha akaomba hivi anavyovijua mama ake ataongea nae pia viwe chini ya jina langu,nilibaki tu namshangaa, nilianza kupata nguvu na kuongeza bidii kwenye Dua...
Kumbe ata mimba alidanganywa Husna hana hata uwezo wa kuibeba hio mimba, walianza kumtafuta make aliwaaacha hotelini na wanadaiwa uko, hawana pesa, imebidi wafanye ufuska wao ndio wakalipia wakarudi kwenye nyumba aliyomjengea Najma, wakakubaliana wauze afu watajua cha kumjibu Naseer...
Hawakujua hati zote zinasoma mimi, kila kitu, walimtafuta ili wapauze aje kusain, akawa hapatikani, alivyowasha tu simu wakamvagaa, hakuwapokelea, wakajua tayari kuna shida, wakaamua kurudi kwa mtaalam wao, wamefika Ilikuwa ni kijijibi ndani ndani humo....
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments