Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

CEO NISAMEHE SIRUDII TENA SEHEMU YA KUMI NA NNE*

14th Sep, 2025 Views 36



Upande wa Naseer alienda kuongea na mama ake kuhusu wazo lake la kuniandikisha mimi mali zake, mama ake aliwaka akaanza kugomba amekuroga na yeye eeh? Yani mtu hana hata mtoto unataka kumpa mali zako unaakili kweli wewe? Ugomvi uliibuka ikabidi Naseer aondoke tu kimya kimya, mimi huku sikuwa najua chochote, jioni mama mkwe anakuja kafula, namsalimia haitikii, akaanza kunitukana, nataka kumuua mwanae, ili nirithi mali za mwanae mtu mwenyewe sijui mgumbaa, aliniporomoshea mbona nilijuta.... yaani

Nilijaribu kumuelewesha lakini hakunielewa. kabisa, akaanza kusema alijua tu make nimekaa kijanja janja, nilibaki tu nalia, nikiwa nalia alitoka mwanangu Elham, alimsalimia bibi yake, akamuuliza, Bibi mbona unamsingizia mama? Mama mkwe alimsogelea mjukuu wake akaanza kumwambia, "mjukuu wangu huyu sio mama ako, huyu anatuchezea akili anataka mali za baba ako, ndio maana anajifanya anakupenda na kukulea vizuri...

Bibi bwana unauzamani sana, na mashaka mashaka utazani ulishawai kufanya hivyo au ulishawahi kufanyiwa? Mama mkwe alishtuka, mpaka tukashangaa, akaanza kulia nakusema namfundisha mtoto kumtukana, nilishangaa na kukana mama mimi siwezi kufanya ivyo unayoniwazia mimi sivyo nilivyo...

Hakujibu chochote akaondoka tu, uku anagomba nilichoka, Naseer alirudi alinikuta nimenywea lakini sikusema chochote, aliwaza akaamua kwenda kumuuliza mwanae, oya dogo mama ako kulikoni nimefanya kosa gani mbona sielewi? Elham alimcheka baba ake, kisha akamwambia tu bibi alikuja kumtuhum wala hujamkosea huenda anamawazo tu siunajua mambo ya wanawake, yani kanavyoongea kama mtu mzima....

"Kwani wamekosana nini? Wala hawajakosama bibi tu na kupenda kwake mali kuliko utu, anahisi mama anataka kukuibia mali, "ila bibi yako jau, hana shukrani kabisa hajui mke wangu kapambana kiasi gani, ata kunivumilia tu, hawezi kuwa na tamaa ya mali, angekuwa na tamaa angeshajulikana tu, nimemwambia bibi lakini haelewi mpaka anamuita mama mgumba, mzee weka sawa ili jambo lisijekufika mbali, mama ni mwanamke poa sana ukimpoteza utakuwa umejiharibia mno...

Walielewana na mwanae, akaingia kulala, kakuta mimi nishalala kitambo sana, sikuwa nataka kuongea chochote kwa leo, kulikucha nilimuandaa kama kawaida, akaondoka, upande wa mama mkwe, alipigiwa simu na mama Najma, akampanga mpaka akaingia kwenye mfumo, kwa ajili ya mali alisema atapambana mpaka Najma arudi kwake, akuna cha talaka, alipewa ahadi ya kupewa kiwanda cha sukari, apo mama tamaa ikamuingia....

Pale pale akafunga safari kwenda kwa mwanae, akaenda kumsihi asimuache mke wake, kwa sababu hata dada ake alikuwa na tabia mbaya, lakini hajatengwa kasaidiwa, na huyu anaweza kuwa bora zaidi, asaidiwe tu, Naseer aligoma mama ake akatumia ubabe kumlazimisha kama. mama nakumtishia laana,mambi yalianza kuwa magumu, tulianza kuishi kwa mawazo mno...

Apo nilikuwa mwaka wa mwisho, nikawa napiga tu Dua usiku na mchana, nilimaliza mitihani yangu, nikaanza kufanya biashara zangu uku nasimamia kwa siri sana zile za Naseer aliniomba nifanye hivyo...

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

CEO NISAMEHE SIRUDII TENA SEHEMU YA KUMI NA NNE*  >>> https://gonga94.com/semajambo/ceo-nisamehe-sirudii-tena-sehemu-ya-kumi-na-nne

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest