Dokta Temba alishangaa sana na kubaki akijiuliza usiku huo aliona nini mpaka aogope kusema akihofia mdogo wake kufa, ila mimi na wewe msomaji tunajua kabisa kuwa aliwaona wachawi japo anaogopa sana kusema akihofia uhai wa mdogo wake. Basi walirudi nyumbani na kumkuta mama yao akiwa amemaliza kuwaandalia chakula, walikula na wakatambulishana kwa kina, ila dokta Temba akawashtaki akina Dorini eti wamempatia life story yao ya kusikitisha ila ikaishia njiani, palepale mama akaomba na yeye ahadithiwe kisa-mkasa hicho mwanzo mpaka mwisho. Dorini akaanza kusimulia yote ila akakomea kubakwa, habari za wachawi hakuthubutu kabisa hata kudokeza.
Mama yake alishtuka kisha akasema
“We Dorini unasemaje”
“Mama nilipoteza usichana wangu kwa kubakwa na mtu mmoja anaitwa Emma”
“Mungu wangu ulibakwa na mtu wa miaka mingapi au hukujua hata umri wake?”
“Aliniambia ana miaka kumi na sita”
Yalikuwa maongezi ya mama na mtoto wake na hapo dokta Temba akadakia
“Hapo inatakiwa usiku uu huu nikufanyie vipimo nitambue hali yako isije ikawa umeambukizwa magojwa ili nikupatie matibatu stahiki mapema”
“Nashukuru sana kwa unavyozidi kunijali baba”
Alisema Dorini huku akimuangalia dokta Temba kwa macho ya upole sana.
Dokta Temba hakutaka kuendelea kuongea zaidi, alimchukua Dorini na kumpeleka kwenye maabara yake ya nyumbani, baada kama dk kadhaa majibu yaliletwa na kuonesha kuwa Dorini hakuwa na matatizo yoyote wala hakuathirika kwa ukatili aliofanyiwa na huyo Emma...Baada ya vipimo na chakula kumalizika wote waliondoka na kwenda kulala kuingoja kesho ili waendelee na maisha yao kama kawaida…
Basi kesho yake dokta Temba aliwaandikisha shule na siyo hizi za kina “pangupakavu” wala za serikali bali aliwaweka kwenye shule za praiveti mashuhuri ndani ya Tanzania, ambazo aghalabu wanaosoma ni watoto wa zile familia za mboga saba. Wakaanza masomo kila mmoja akiwa na ndoto zake, Dorini yeye alikuwa akipigana siku moja awe mfanya bishara mkubwa duniani hivyo akawaza kuja kuchukua shahada ya uchumi. Upande wa Frank yeye aliwaza kuwa mwanasheria mkubwa ili aweze kupata fursa ya kukemea vikali hii tabia ya wazazi kuwatelekeza watoto, hivyo akawaza kusomea sheria.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.