jira ya saa sita usiku Dorini hakuwa amefanikiwa kupata usingizi kabisa, badala yake alijilaza tu, kwa hofu na mashaka aliyo kuwa nayo akajifunika shuka tu ili mdogo wake asije tambua kama hakulala.
Usiku huo wa saa sita alicho kiona Dorini kilimfanya jasho limtoke, mwili ukafa ganzi akakosa kabisa hata nguvu za kuinua ulimi wake kupiga kelele akatamani angepata usingizi ila kwa wakati huo haukupatikana kabisa, basi akabaki kuangalia tu filamu ya kichawi iliyo kuwa live yaani mbashara mbele ya macho yake. Ni baada ya kuwaona watu walio kuwa wamevaa vitambaa vyekundu, huku kichwani wakiwa wamejifunga vilemba vyeupe, walikuwa wanaume wawili walio kuwa wamevifunga viunoni vitambaa hivyo vyekundu huku wakiwa vifua wazi kabisa, upande wa wanawake walikuwa wanne, wao walivaa vitambaa hivyo toka chini miguuni mpaka juu ya matiti yao, na wote kwa pamoja walivifunga vyema vilemba vyeupe vichwani mwao. Mithili ya wanakwaya kanisani walikuwa wakiimba kwa pamoja huku wakitikisa viuno vyao na kuruka hatua kadhaa nyuma na kwenda hatua moja ndefu mbele. Aliwaangalia watu hao walivyokuwa wakitambika pale huku akiogopa na kuepuka kutikisa mwili akihofia wakibaini uwepo wake na kutambua kama anawaona huenda wangemteketeza na hatoweza tena kumlea mdogo wake. Baada ya muda mara kiongozi alitoa amri kuwa waende wakalete viti kwa ajili ya kukaa, mara ileile wakapotea wote na kiongozi wao akabaki pale akiwangoja. Baada ya kama dakika moja hivi wote walirudi wakiwa na mtu mmoja mmoja. Mara tu baada ya wao kufika ghafla kuna kiti kimoja kilionekana kung’aa eneo lile walipokuwepo, ambapo kiongozi yule alikaa juu ya kiti kile. Wale watu walio letwa walionekana kuwa bado wamelala, waliinamishwa migongo yao na ndiyo waliofanywa kuwa viti kwa ajili ya wachawi wale.
Basi baada ya kila mmoja kukaa kwenye mgongo wa mtu aliye mleta wakaanza kikao chao. Mambo yote hayo Dorini aliyaona mbele ya macho yake.
“Ony’ake be’ kaseembee’ lemeleh kase dil manjie’ kame” (“Nawasalimieni na karibuni kilingeni wageni mjisikie mpo nyumbani”)
Alisema kiongozi wao huku akinyosha mikono yake mbele kuonyesha ishara kuwa amewakaribisha, na wote kwa pamoja wakasema
“Kans’e” (“Asante”)
Pale pale kiongozi akasema huku akionekana kuwa na furaha sana
“Kasembee’ kasembee’ Manjie’ dole kase” (“karibuni karibuni wageni mnaweza kuja sasa kiringeni”)
Mara waliongezeka mabinti wanne wazuri sana wao walivaa vitambaa vyeusi na kichwani kujifunga vitambaa vyekundu, mmoja alionekana kuwa na asili ya kihindi na wengine walionekana kuwa waafrika kama hususan watanzania. Baada ya mabinti hao kukaa chini naposema chini simaanishi kwenye ardhi hapana bali ni kwenye migongo ya watu, wale ambao mnalala bila kuomba mjue usiku mnaenda wapi, mtu anaamka mgongo unauma anajihisi kachoka sana anabaki kusema eti kalala vibaya, chefu, hakuna cha kulala vibaya hapo, yawezekana kabisa usiku wote wewe ulikuwa ndiyo kiti kwa ajili ya wachawi hivyo kuwa makini sana, kabla ya kulala omba sana ili Mungu akulinde usiku mzima mpaka kuna kucha maana waswahili walisema “Usiku mwaka”.
Yote hayo Dorini aliyaona vyema yaani alikuwa akiona sasa kifo kipo karibu naye, Ndipo akapata wazo la kumwamsha mdogo wake ili watoke kwenye hilo dampo usiku uo huo maana alihofia kuonekana. Basi akamwamsha. Frank alipoamka akaanza kulia akilalama baridi kuwa kali. Mara wale wachawi wakawasikia na wote kuwageukia, Dorini akatambua kuwa kimenuka hapo, kifo kipo karibu yao na muda wowote wanaweza kukikabili kifo.
Mwili wa Dorini ulitetemeka mithili ya jenereta bovu huku kijasho chembamba kikimtoka baada ya wachawi hao kuwaona kuwa walikuwa karibu yao. Mara yule binti mwenye asili ya kihindi aliwafuata na kuwapeleka kwa kiongozi wao, Frank alikuwa wa kulia tu maana watu hao kimwonekano walitisha sana. Huku akiwaangalia watoto hao kwa umakini sana yule kiongozi wa wachawi hao akasema
“Chade kofine’ roise manje” (“nadhani hakuna haja ya kuwadhuru hawa watoto”)
Akapumua kidogo kiongozi huyo kisha akaendelea kuongea
“Sose’ manje I’ pida~ kose magine seen” (“tena mtoto huyu tumpatie ubize ili asipate nafasi ya kutangaza haya aliyo yaona”)
Baada ya kusema hayo akanyoosha mkono wake na mara mkononi kukatokea mionzi fulani kama radi hivi ambayo ilimpata sawia Frank na wao wakapotea palepale na kumuacha Frank akiweweseka kwa maumivu. Baada ya wao kupotea tu mara Frank akanyamaza na kuonekana hana shida yoyote wakawa wamerudi tena palepale na kuendelea kulala. Hapohapo Dorini akapata usingizi mzito akifuatiwa na Frank, wakalala kama wafu mpaka kulipo pambazuka.
Follow page yangu Story za Riwaya Tanzania.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.