Klabu ya Fountain Gate inaingia dimbani saa 8 mchana huu ikiwa na wachezaji 13 TU waliosajiliwa na mfumo wa usajili kutokana na MATATIZO YA KIUFUNDI ambayo hayawahusu FOUNTAIN GATE kitu ambacho kina chembe chembe za UONEVU.
Fountain walikuwa na kesi na Amisi Tambwe kule FIFA wakafungiwa kusajili, lakini baada ya kumaliza tofauti zao na Tambwe na FIFA wakakubali kwa barua ya tarehe 1 Septemba 2025, kwamba jambo hilo limeisha wakaondoa hiyo ban, wakawaambia TFF pia kuondoa ban ya ndani pia.
Lakini bado Fountain Gate wameshindwa kusajili wachezaji wao kwenye mfumo wa usajili (FIFA CONNECT) jambo ambalo walilipoti TFF na TFF wakasaidia kuwaandikia FIFA ili Fountain waweze kusajili, lakini FIFA hawajajibu barua za Fountain wala za TFF. Fountain walichoambiwa na TFF kwamba kuna tatizo la kiufundi ambalo kimsingi si kosa la Fountain Gate.
Fountain Gate wakaandika barua TFF kuomba mechi yao ya leo ihairishwe ili jambo lao lishughulikiwe kwakuwa wana wachezaji 13 pekee na kosa si lao, majibu kutoka Mamlaka (Sekretarieti ya TFF) ni kwamba HAWAWEZI KUGHAIRISHA KWAKUWA RATIBA ISHAPANGWA. Bin Kazumari inajiuliza kama jambo hili lingekuwa Simba au Yanga, majibu haya si ndo yangeturudisha kule kwenye HATUCHEZI? Bado hatujajifunza tu au kwakuwa Fountain Gate HAWANA WATU? Tujifunze kuwasikiliza hata wadogo na tuwatendee haki bila kuangaliana sura, CHEO NI DHAMANA TU.
BIN KAZUMARI MTIPA (Voice of the voiceless).
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments