Mtu anielekeze kwa upole kabisa na mniwie radhi kama nitakuwa βNahamisha Madaβ hivi ule msimu wakati Benki ya CRDB inaingia kudhamini michuano ya Kombe la Shirikisho walianzia hatua ya Mtoano wakati awali ilikuwa inatambulika kama Azam Sports Federation Cup, ambapo Azam ndie alikuwa Mdhamini Mkuu, tunakubaliana?
Sasa Mkataba wa Azam kama Mdhamini ukatakamatika halafu CRDB akachukua kama Mdhamini Mkuu halafu Azam akabaki kuwa Broadcaster (Mrusha Matangazo) hapa si tunakubaliana? Je tulipewa status ya Azam baada ya kutamatisha mkataba wake? Maana Premier League yupo NBC anatoa hela na yupo Azam kama Broadcaster anatoa fedha tena nyingi saaana ambazo zote zinafahamika.
Sasa kwa faida ya sisi Wakulima na Back Bencher mtuelekeze mnaofahamu kwa lugha rahisi tu, Azam kama Mrusha matangazo na CRDB kama Mdhamini Mkuu maana yake thamani ya kombe la FA imepanda, sasa kiufundi hapo nilikuwa nataka kujua Azam anatoa kiasi gani (kwa nia njema tu ya kujifunza) na CRDB inafahamika anachotoa, hivyo jumla hapo mzigo ni kiasi gani kwenye michuano ya FA?
Kwa sauti ya upole tu na taratibu, kama Azam alikuwepo na amebaki kama Broadcaster, sasa yupo CRDB tunaweza kuambizana thamani ya michuano ipoje na bingwa sasa hivi anachukua kiasi gani huko? Nikiri hili silifahamu ningependa Instagram kitengo cha Taarifa mnisaidie Wakuu.
Na kwa Watu wa Masoko hivi Mdhamini anapoongeza zawadi za Mshindi na bakshishi za Washiriki zinabaki zile zile? Nauliza tu maana hizi ni taarifa nzuri ambazo ni nzuri kufahamishana, kama mikataba inaingiliana kote kote basi tunaambizana kwa sauti ya upole, lengo ni kujifunza tu.
.
.
AMEANDIKA FARHAN JR..