. Daktari wake alikuwa amesisitiza kwamba ingawa upasuaji huo haukuwa wa dharura ya haraka, ulikuwa muhimu ili kuondoa tatizo lililokuwa likimtesa kimya kimya kwa muda mrefu.
Zarina hakuwahi kuwa na usingizi mzuri kwa siku tatu mfululizo. Kila alipomwangalia Darren usiku, moyo wake ulikuwa unamwambia, asiache kumshika mkono hata sekunde moja.
Asubuhi hiyo, nyumba nzima ilikuwa na hali ya wasiwasi. Raveen alikuwa kimya zaidi ya kawaida, akihangaika kuhakikisha kila kitu kiko tayari. Wazazi wa Darren walifika wakawa wametulia huku wakimuomba mtoto wao.
Zarina alikuwa na Darren kwenye chumba cha mapumziko walikuwa wamekaa kitandani.
Darren amevaa shati jeupe la wagonjwa na suruali Uso wake ulikuwa na tabasamu dogo, lakini macho yake yalionyesha hofu iliyojificha.
“Hii ni siku nzito sana Zarina .Sikuwahi kufikiria kuwa nitakuwa kitandani badala ya kukulinda wewe.
Zarina alimshika mkono kwa nguvu.
“Hata shujaa anaweza kuhitaji kupumzika na kutibiwa. Leo kazi yangu ni kukulinda wewe, Darren. Hii vita tunapigana pamoja.
Mama na baba yake walipomaliza kuomba walienda kumuangalia.
" Darren mwanangu siku zote umekuwa shujaa kwa uwezo wa Mungu utavuka hili. Alisema baba yake huku akiwa ameshika begani. Na Darren alitabasamu.
" Mwanangu nakuombea utoke salama.
" Sawa mama . Baba , mama kama ikitokea bahati mbaya sijaamka naombeni munuangalie sana Zarina na mtoto wangu alietumboni. Mchukulieni Zarina kama mlivyokuwa mkinichukulia mimi . Nadhani nilishawaeleza kila kitu kuhusu yeye.
Wakiwa wanaendelea kuongea wauguzi walifika .
" Jamani tumekuja kumchukua mgonjwa wetu
Walimchukua Darren wakampeleka kwenye chumba cha maandalizi. Daktari alikuja na kumhakikisha kuwa kila kitu kiko sawa.
“Upasuaji utachukua saa manne hadi sita. Tunatarajia matokeo mazuri, MUNGU atusimamie kwenye kazi yetu.
" Amina.
Zarina alikuwa anaongea mwenyewe kwa sauti ya chini huku machozi yakimtoka . “Utarudi kwangu salama. Nitakusubiri hapa mlangoni.
Mlango wa chumba cha upasuaji ulifungwa taratibu. Zarina alibaki nje, akitembea huku na kule kama mtu aliyepoteza kitu cha thamani. Kila dakika ilionekana kama masaa kwake. Kila mtu alikaa kimnya akimuomba Mungu kwa anavyojua yeye.
Baada ya muda mrefu waliohisi kama umekaa miaka, daktari alitoka akiwa na tabasamu. “Upasuaji umefanikiwa. Tumemtoa kwenye chumba cha upasuaji, sasa yupo kwenye chumba cha uangalizi.”
Zarina alihisi miguu yake ikilegea kwa furaha.
" Tunaweza kwenda kumuona?
" Labda kwa mara moja tu maana bado hayupo sawa.
Zarina alikimbilia kumwona, na alipomkuta akiwa amelala kitandani, huku akiwa Kalala usingizi mzito na puani aliwekewa mashine ya kupumulia.
Baada ya dakika tatu doctor aliwaomba waondoke wamuache apumzike.
Baada ya siku mbili hali ya Darren ilikuwa nzuri japokuwa hakuwa ameimarika .
Siku hiyo Zarina alifika wodini akamkuta bado Kalala. Aliushika mkono wa Darren.
Darren alifumbua macho kidogo, akatabasamu kwa uchovu. “Nilikuambia nitarudi na sasa niko hapa, salama.”
Zarina alijifuta machozi, akiinamisha kichwa chake kifuani kwake. “Usinifanye nipitie hofu kama hii tena, Darren. Nakupenda sana.
" Nakupenda pia.
Raveen alisimama mlangoni,akiwa anatabasamu.
“Kaka, sasa unaweza kupumzika. Shemeji atahakikisha unapata kila unachohitaji.”
baada ya muda mrefu, Zarina alihisi kwamba sasa ilikuwa zamu yake kulinda moyo wa Darren, kama ambavyo yeye alivyomlinda mara zote.
Hatimae siku zilienda waliruhusiwa wakarudi nyumbani ila siku moja moja waliorudisha hospitali kwaajili ya kuangalia maendeleao yake. Zarina alikuwa alimuhudumia vizuri na kuhakikisha anakuwa salama.
Siku moja baba yake Zarina alienda nyumbani kwa Darren kumuangalia binti yake.
Zarina alipomuona baba yake alishituka sana na kuingiwa na hofu lakini mama Darren alimtuliza.
" Tulia binti yangu kila kitu kipo sawa.
Zarina alitulia lakini hakuwa na amani.
Zarina alienda chumbani na mama Darren wakawa acha wanaume sebleni wakiongea.
Najua unajiuliza baba yako kafikaje hapa.
" Ndio tangia nimeondoka hajawahi kujitafutia kujua nilipo.
" Labda kwasababu alijua upo sehemu salama.
" Alijuaje kama nipo sehemu salama?
" Baada ya wewe kuja hapa Darren alituambia ikabidi tumtafute baba yako, hatukuweza kumpata ila tulipata mawasiliano yake tulipiga simu na kumueleza kila kitu bahati nzuri alitueleza .
Baada ya Zarina kuongea na mama mkwe wake alienda kuongea na baba yake.
" Nisamehe baba , najua nimekosea kuja kukaa kwa mwanaume bila ndoa na mpaka ukapelekwa kubeba ujauzito.
" Usijali mwanangu kwa upande mwingine hata mimi nina makosa sikuweza kukutetea kwa yule mwanamke mbaguzi.
Mama zawadi akifanyia mengi mabaya lakini nashukuru kuna mtu aligundua unayopitia na kujitoa kwako.
Zarina nimeridhika mfungwa ndoa na Darren yeye ndio mwanaume anayekufaa.
Zarina alifurahi na kumkumbatia baba yake.
" Asante baba nashukuru baba kwa kuthamini furaha yangu.
Baada ya hapo mzee Mustapha walirudi nyumbani kwake.
" Ulisema unaenda kumchukua Zarina yuko wapi sasa?
" Mama zawadi naomba uachane na mambo ya Zarina nimeamua kumpa uhuru wa kuishi maisha yake.
" Uhuru upi uliompa?
" Akitegemewa huko , awe na furaha pamoja na amani hapa mwanangu alikuwa anateseka sana.
" Alikuwa anateseka na nani? Usitafute sababu wewe mzee . Sema umeamua kumpa uhuru mwanao wa kuishi na huyo mwanaume wake sasa ngoja tuone kama watafika mbali.
Mama zawadi na mwanae zawadi waliendelea kufuatilia maisha ya Zarina wakagundua kuwa anafanyiwa sherehe kubwa ya uchumba pia ni mjamzito.
" Haiwezekani Zarina hawezi kuolewa na boss wake
" Sasa tutafanyaje mama?
" Tutajua la kufanya siwezi kukubali kabisa , si bora ungeolewa wewe mwanangu.
" Alafu sijui nilifungua na nini unajua siku ile zilivyoenea kwenye sherehe yule kaka alikuwepo na niliwakuta wanaongea.
" Sasa kwanini usijitongozeshe kwake mambo yameanza kuwa magumu unaongea ujinga wako hapa.
Zawadi na mama yake walijaribu kufanya kila hira kumuharibia Zarina lakini juhudi zao ziligonga mwamba. Mambo ya Zarina yalinyooka kama rula na hatimae alipata ndoa . Walifunga ndoa na kufanya harusi kubwa sana iliyoteka vichwa vya habari kwenye mitandao.
Zarina aliishi maisha mazuri sana na mume wake pamoja na familia ya Darren hakika alipata familia mpya.
Pia alibarikiwa kupata mtoto mzuri wa kike ambae aliongeza furaha kwenye familia yao.
Mama zawadi na wanae walibaki na aibu .
Kweli mwisho wa ubaya ni aibu.
All the best.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments