Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

IBAKI STORY πŸ’”πŸ’”01

9th Sep, 2025 Views 21



Jack ndio jina langu ni binti wa miaka 21 ktk harakati zangu za kutafuta mkate wa Kila siku kwaajili ya kukidhi mahitaji kadha wa kadha.Nikakutana na kijana mmoja aitwaye Bernad eeebwana story ikawa Ivo
Bernad: Habari mdada mzuri
Mimi: nzuri tuu
Bernad: sorry nimekua nikiwa mteja wako karibia Kila siku lakin umekua busy Sana naomba inisaidie no yako Nina shida na ww pengine ninaweza kua nakupigia kwaajili ya biashara
Mie Tena mtoto wa kichaga ninavyo ipenda biashara yangu chap nikaanza mtajia no 0766.........90
Bernad:: owky Asante sana dada mzuri nisave jina gani mamy!
Mie: naitwa jack hata ukisave dada j inatosha .....
*******
Akaondoka zake nami nikawa busy kufuta futa vumbi bidhaa zingine..biashara yangu ni kuuza duka la vipodozi
Nikaendelea na biashara mpaka mda wa kufunga duka ukafika nikafungua duka nikaanza safari ya kuelekea makoroboi kwaajili ya kupanda gar kuelekea nyumbani pasias MwanzaπŸ˜‹πŸ˜‹
Baada ya kufika nyumbani nikamkuta baba na mama yaani bwana na Bibi nelyson wamekaa sebureni wakitizama Tv taarifa ya habari ITV nikawasalim Kisha nikaingia chumbani kwaajili ya kuoga
*****
Nilianza kupunguza nguo moja baada ya nyingine mwilini mwangu na kuingia bafuni.Nilioga nikamaliza nikachukua tushert nikavaa na kitenge kuelekea sebureni kupata chakula
*********
Tulikula tukamaliza baba na mama wakanyanyuka kwenda kulala mie nikabakia sebureni na mdada wa kazi tukiangalia maludio ya BEKI TATU maana mda huo ndio kulikua na maludio na mie ndio mpenzi wa BEKI TATU
Mda kidogo sim yangu ikaingia ujumbe mfupi uliossomeka hivi "" hellow dada mzuri!! Uko vizuri! Pole na uchovu wa kazi ninaomba kuzungumza na wewe""
Mie Sasa nilisha nogewa na vituko vya koku na mulii.Nikaipotezea msg iyo nikawa busy kweli yaani huwa sitaki hata nukta inipite kabisa
Nikaangalia mpaka ikaisha woiiii nikawa nimejichokea Sasa nikaona usingizi unabisha hodi nikaanza kujinyanyua kuelekea chumbani....ikaingia sms nyingine " mamy sorry kwa usumbufu nikutakie usiku mwema """ nikajisemea moyoni duh uyu mbona kama anakihele hele sijamjibu anakazana tuu na si mjibu mfyuuuuu

Nikajifanya kauzu na malingo yangu Sasa mda kidogo sim ikaita no ile ile inapiga nikasema ngoja nipokee nimtkane kwanini ananipigia mda huu nataka nilale
Hallo nikapokee kikauzu Sasa🀣🀣🀣
Upande wa pili hallo dada mzuri!! Samahani kwa usumbufu
Yaani ile samahani ikakata pozi la kut😜kana ikabidi nitulie kimya nijibu bila samahani
Upande wa pili...Mimi Bernad
Mimi Sasa:: oooh jamani nikajikuta Sasa naanza kusema samahani ulinitext nilikua nakula hata sijaulizwa nyie nyie🀣🀣🀣
Bernad: pole nimekusumbua samahani....jack kiukweli nimetokea kukupenda Sana yaani tangu nikuone siku ya kwanza mpaka Leo natamani niwe nakuona Kila mda....yr so beautiful ❀️ yaani ni mwanamke mpambanaji,mpole sikujui Sana ila ivyo tuuu nakupenda mama nisamehe kama nakosea kukueleza haya yote
Mimi; ujakosea Asante lakin nahitaji kupumzika nimechoka Sana na kazi naomba tutazungumza kwa wakati mwingine
Bernad:: owky sawa lala mama usisahau kusali
Nikamjibu tu haya nikakataa sim
*******
Dakika mbili nyingi akatuma Tena sms dada mzuri usinichukie nakupenda nisamehe nifikirie vizuri Nina Nia njema na wewe❀️
Sikumjibu Nikauchapa usingizi mpaka asubui nikakulupuka nimesha chelewa nikaanza kukimbizana kujiandaa...nikatoka njee nikamkuta baba kaisha amka nikamuakia,shikamooo baba!! Nikawa natoka kama nakimbizwa maana nimechelewa mnooo adi kijua kimeanza kutokeza
Basi bwana mpaka nikafika dukani nikafungua nikaanza kufanya usafi nikamaliza nikatulia Sasa kuanza kuhudumia wateja

Majira ya saa nne na nusu asubui ikaingia sms kutoka kwa Bernad: mambo! Umeamkaje
Nikamjibu Niko poa,,akatuma ten sms nyingine vipi umeisha kunywa chai!!
Mimi,nikamjibu Bado nilikua busy
Bernad: unajiskia kula Nini!
Sasa nazani mnajua ukutane na sms kama iyo woiii nikasema hapa sijibu kitu ataniona Mimi na tamaaa nikaa kimya weee mpaka akaipiga sim
Hallo jack!
Mie: yes
Bernad; Aujanijibi unataka kula Nini
Mie; nipo busy Sana Leo nitakula mchana
Bernad: hapana kula nakutumia kiasi hapo utakula unacho taka
Mimi: nikazuga,hapana acha tuu huku moyoni najisemea weee nitumie tuu nikasuke nakusukaπŸ€£πŸ€£πŸ™ˆπŸ™ˆakakata sim

Mda wote nikawa naitolea macho sim mhhhh😲😲😲😲toba ikaingia sms imethibitishwa umepokea kiasi Cha sh,laki moja na elfu 5 woiiiiiii😲😲😲nyie wamama hamkuniona vile nilishangilia sio kwamba sikua na pesa ila mtanisameh ndugu zangu jinsi pesa tunavyo ipenda chaga girl msinune vipenzi vyangu πŸ™ˆπŸ€£πŸ€£yaani kabla sijaitoa nikaanza kuzipiga hesabu ya harka harak kusuka 25 alafu nyingine ya hissa jumapili🀣🀣🀣
Nikasema hapa lazima nizuge ajue Niko busy sijaona msg nikauchuna kweli mpaka jioni nimeinama zangu nacheck clip TikTok mara uyo hapo dukan kwanguπŸ™ˆπŸ™ˆniliona aibu sikusema Asante alafu kanikuta Niko na sim pili sikua busyπŸ™ˆπŸ™ˆnilijibalagua apo mie Tena

Bernad; vip jack umekula?
Mie; Ndio nimekula Asante yaani nilikua busy kweli yaani saivi ndio nashika sim naona na sms yako jamani yaani wewe🀣🀣🀣kumbe ulinitumia na pesa πŸ€£πŸ€£πŸ™ˆπŸ™ˆAsante jamani
Bernad ; owky sawa usijali nimetoka kazini nimeona nipite nakucheck
Ndio nikapata na mda wa kumuuliza kwani mwenzangu unafanya kazi wapi!!
Bernad; nafanya kazi apo access Bank 🏧
😲😲😲😲
Nikalitoa jicho
Moyoni nikajisemea mme si ndio huyu kwanza handsome pili ana mgari mzuri ma uwakika wa kula upo mbona shoga yangu Jane atanikoma🀣🀣🀣
******
Nikaitika owky sawa mie Bado nipo nipo mpaka saa mbili ndio nafunga
Bernad; Haya ngoja niwai om and then niende gym ikifika saa mbili nimetoka gym nitakufata nikupeleke om
Mie : sawa
Huyooo akaondoka zake,Mimi nikabakia TikTok
Nimekaa dukani mpaka majira ya kufunga Bernad akanipigia sim nakufata nikamjibu sawa
Nikajipulizia spray mle ili ninukie vizuri vizuri jamani tunao uza maduka ya vipodozi ni ngum kunuka jasho wakat spray tunaziuza ni mwendo wa kujaribia tuu kwenye nguo🀣🀣🀣🀣
Mie uyoo na komwe langu

ITAENDELEA

.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

IBAKI STORY πŸ’”πŸ’”01  >>> https://gonga94.com/semajambo/ibaki-story-01

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - Mc Shabby Tatizo Moyo
Mc Shabby Tatizo Moyo
Mc Shabby Tatizo Moyo

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest