Mtunzi:™ Simulizi za Abuu lion ✓
№0685086201
Yule dada akaweka kituo na kushusha (kilio) kizito, akasema, "Kaka, siwezi kuendelea kukusimulia, (naumia sana)..." Nilijikuta mpaka mimi nashusha machozi aisee.
Niliona nimsogelee karibu na kumbusu yule dada kwa upendo na kichwa chake nikakiweka begani kwangu huku akiwa amempakatia mtoto wake aliyekuwa mchanga, kisha nikamwambia, "tafadhali acha kulia na unisimulie ili niweze kukusaidia."
Yule dada alilia kwa dakika kadhaa kisha akaendelea kwa kusema, "baada ya kuambiwa na daktari kuwa mume wangu amenifanyia mambo ya (kikatiri) kiasi kile nililia sana na daktari akaniambia kuwa mume wangu hakuwa na lengo la kuniacha (hai) bali alitaka nipoteze maisha. Basi baada ya mambo yote hayo nilirudi nyumbani, hapo hospitali waliokuja kuniona ni majirani lakini ndugu wangu au wa ukweni hawakuja kuniona. Baada ya kufika nyumbani nilikuta watu wamejaa, na waliponiona walinijulia hali, lakini japokuwa mume wangu alinitendea ukatili wote huo sikusita kumuulizia yuko wapi baada ya kufika nyumbani, na jibu nililopatiwa niliambiwa kuwa baada ya kunifanyia ukatili ule mume wangu amepokea kipigo kizito kutoka kwa wananchi na kwa sasa yupo hospitali hali yake siyo nzuri. Baada ya taarifa ile nilishindwa kuvumilia maana sikuwa na mtu mwingine wa kuweza kunisaidia zaidi ya mume wangu, japo amenifanyia ukatili wa aina ile. Kina mama majirani waliguswa na tukio nililofanyiwa, hivyo walikuwa wakinipa msaada mara kwa mara hasa chakula pamoja na matibabu kama wanawake wenzangu.
Basi muda ulizidi kwenda na zilipita siku 3 mume wangu hakurudi nyumbani. Nilishindwa hata kwenda kumuona sababu sikuwa na uwezo wa kutembea, sehemu zangu za siri zilikuwa na kidonda kikubwa. Hata kurejea nyumbani nilipewa msaada tu na watu.
Siku ya tatu jioni taarifa ilikuja kuwa mume wangu amepoteza maisha — yaani (amefariki) dunia kutokana na kipigo kibaya alichopokea kutoka kwa wananchi wenye hasira kali. Msiba wa mume wangu uliniacha kwenye majanga makubwa. Kwanza nilikuwa nauguza kidonda, lakini pia nilikosa mtu wa muhimu katika maisha yangu. Isitoshe hata msibani walinipiga marufuku kwenda maana wakwe zangu hawakunipenda hata kidogo, hivyo mpaka mume wangu anazikwa mimi sikufika hata msibani kwake wala sikuweza kushuhudia maiti yake. Nilikuwa na wakati mgumu sana kaka yangu, kwani yule mwanaume ndiye alikuwa tegemeo langu.
Basi niliishi kwa maumivu makubwa, na mpaka nilipopona kidonda na kuendelea na shughuli zangu kiwandani, ajira yangu ilikuwa imeshaondoka sababu nilikaa nyumbani kwa mwezi mmoja na siku kadhaa, hivyo kiwandani waliniondoa kwenye nafasi za ajira.
Niliendelea kuhangaika huku na kule kutafuta ajira huku mimba yangu ikizidi kukua. Hatua ya mwisho, pale nilipokuwa nikiishi, kodi ya nyumba iliisha na mwenye nyumba alinifukuza kama mbwa. Hivyo niliondoka usiku wa saa 4 na dakika, na nilifika sehemu moja hivi nikiwa nimebeba mabegi yangu. Kaka yangu, kifupi tu, historia yangu ni ngumu mpaka kufikia kujifungua mtoto huyu salama.
Nilimtazama yule dada kwa huzuni sana, kisha nikamuuliza, "Sasa baada ya kufukuzwa na mwenye nyumba, ulienda wapi?"
Yule dada amebarikiwa busara sana, akasema, "Kaka, sikuzote Mungu huwa hamuachi mtu hata kama yupo kwenye magumu. Siku ambayo nilifukuzwa na mwenye nyumba nyumbani kwake, hiyo siku nilipitia magumu sana. Nikiwa nimejilaza chini ya uvungu wa gari bovu lililokuwa limepaki kwa muda mrefu, nilihisi mtu ananiita. Nilipogeuka kumtazama alikuwa mbaba mmoja hivi, alikuwa akiniita. Niliamka na kutoka chini ya uvungu, na yule baba aliniuliza sababu ya kuwa pale. Nilimuelezea kwa ufupi historia yangu, naye alinisihi kwa kusema, "Mwanangu nakusaidia sababu ya huyu mtoto wako sababu una mimba, hivyo nitakusaidia maana matapeli mmekuwa wengi sana."
Ndipo yule baba akanipa msaada na tukaongozana mpaka kwake. Alikuwa akiishi peke yake; mkewe alikwenda kujifungua kwao, na alikuwa na watoto wawili na wote walikuwa kwenye shule za bweni, hivyo pale nyumbani alibaki peke yake. Ndipo akanikaribisha, nikawa kama mtoto wa pale na kuishi kama nipo nyumbani.
Yule baba simsemi vibaya, alikuwa akinihudumia kama mwanae au mkewe. Kwa kila siku alikuwa akiniachia 10,000 shilingi za Kitanzania. Hivyo nilikuwa natumia 2,000 tu, kisha 8,000 naitunza. Nikikaa kwa yule mzee kwa amani sana kwa miezi hiyo ya mimba, maana mkewe baada ya kujifungua alikumbwa na matatizo ya uzazi, hivyo alichelewa kurudi. Na taarifa ya mimi kuwepo pale aliambiwa na mumewe.
Basi ilifikia siku ya kushikwa na uchungu na kwenda kujifungua. Ndiyo siku ambayo mke wa huyu baba naye alikuwa akirudi baada ya kujifungua. Na namshukuru Mungu nilijifungua salama, japo nilipoteza damu nyingi sana, na ilibidi yule baba afanye mpango niongezewe damu maana hali yangu haikuwa nzuri sana. Nilipatiwa matibabu mafupi, na mke wa yule baba aliyenisaidia naye alifika hospitalini na kufurahia sana kuniona mimi na mwanangu. Hakuwa na kinyongo hata kidogo.
Basi nilisalimiana naye kwa heshima sana, maana naishi nyumbani kwa mumewe kama nyumbani kwetu. Hivyo niliwachukulia kama familia yangu. Basi muda wa kurudi nyumbani ulifika, nilirudi salama. Na rafiki wa yule mama ambaye naishi kwake walikuja kunipa hongera. Lakini zaidi ya hao, hakuna mwingine aliye kuja kunijulia hali, maana nilikuwa nimetengwa na ndugu/jamaa.
Basi siku zilikwenda kama wiki moja hivi kupita baada ya kujifungua. Siku moja nikiwa bado na kidonda, nilitoka nje kupunga upepo nyuma ya nyumba — ila ni ndani ya geti maana ile nyumba ilikuwa kubwa sana, na pembeni yake ilikatiwa partition za nyumba kama 3 mle mle ndani.
Nikiwa nje naendelea kupunga upepo, nimempakatia mwanangu maana sikujua hata miko ya kumtoa mtoto nje akiwa mchanga, nilimsikia yule mama akiwa amerudi, na siyo kawaida yake akaanza kuniita. Lakini nilishindwa kuitika sababu sauti yangu haikuwa sawa, niliitika kwa sauti ya chini sana.
Yule mama hakuwa peke yake, alikuwa na rafiki yake. Nikamsikia akisema, "Yaani amejifungua juzi juzi tu lakini kutulia ndani hawezi, ila Husna (mjinga) sana huyu mtoto."
Niliona kawaida tu, sababu mama yoyote duniani huwa na maneno. Nilimalizia kumnyonyesha mwanangu na kusimama kuelekea huko alikokuwa mama. Nilipofika nilikuta viatu vipo nje, nikajua wameingia sebuleni.
Sasa kabla sijafungua mlango, nikamsikia yule rafiki aliye kuja na yule mama mwenye nyumba akisema, "We mama Danieli, huyu binti hayupo kweli? Tusije tukaropoka akatusikia."
Kisha mama mwenye nyumba akasema huku akifungua madirisha, "Ila kweli, ngoja nimuangalie kwanza."
Niliogopa sana. Yule mama akasimama na kuanza kuniita huku akielekea chumbani kwangu, na nilihisi anafungua mlango wa kutokea. Nikajificha kwenye tanki la maji lililokuwa karibu.
Yule mama akatoka nje kuhakikisha usalama kuwa nipo au sipo. Inaonekana kuna jambo wanataka kuteta, hivyo alitoka nje na kufungua mlango wa kutokea na kuanza kuizunguka nyumba yote.
Laiti kama angezunguka nyumba yote angeniona. Nashukuru Mungu aliizunguka nyumba kidogo na kurudi ndani.
"Huyu binti ametoka bana, na akirudi lazima afungue geti, hivyo tutamsikia tu. Na sijui kaenda wapi na mtoto mchanga," alisema yule mama mwenye nyumba.
Kisha yule rafiki akasema, "Tuachane na hayo. Sasa kama uwezekano upo, hakikisha leo tunapata huu mzigo, maana ni muhimu sana. Huyu binti tutampulizia dawa usiku alale fofofo, kisha tutaandaa vijana waje kumchukua mtoto wake. Wahakikishe wanavunja mlango ili ionekane mmelivamiwa. Kisha baada ya kumpata mtoto, tutampeleka kwenye kafara ya 13. Nadhani uchaguzi huu lazima upite shoga yangu, maana kinachohitajika ni (damu) ya mtoto mchanga."
Nilistuka na kukumbuka kuwa huyu mama mwenye nyumba ni mwanachama na anagombea ubunge. Hivyo wanataka kumtoa mwanangu (kafara).....
Itaendelea.
Kama unasoma simulizi hii, usisahau kulike na kutoa maoni yako. Asante..