Kwa jeuri aliongea kwamba kakataa milioni 30 za Yanga kwenda kutumbuiza kisa yeye ni shabiki wa Simba imani yake ilimwambia kwamba hakuna mtu atazuia yeye kutoimba kwenye Simba lakini mambo yamekuwa tofauti Simba wamemfungia vioo.
Kwenye hii dunia ukijifanya mfia timu kuna siku utadharirika na kupoteza fursa muhimu, nadhani kwasasa Tunda atakuwa anajiona ni mjinga kiasi gani kwa kukataa pesa ndefu kisa Simba anatakiwa ajifunze kwa wengine.
Alikiba ni shabiki wa Yanga lakini ilipokuja pesa ndefu kutoka Simba hakuiacha na anaifanya kazi ya Simba kwa weledi, Mbosso shabiki wa Simba lakini Yanga wameweka pesa mezani akaenda kutumbuiza kwenye tamasha la Yanga kisha karudi Simba na hakuna aliye mtukana lakin hata Diamond alifanya hivyo alifanya kazi na Simba kisha akaenda kufanya kazi na Yanga kakusanya pesa zake anakula maisha.
Huyu jamaa badala ya kuangalia kazi yeye akaweka ushabiki mbele labda kama hajui, Timu zinapoita msanii lengo sio kumuhamisha timu bali yeye kwenda kuburudisha mashabiki na mashabiki hawa wa hizi timu ndio mashabiki wa muziki pia. Leo hii Diamond, Alikiba, Mbosso na Zuchu wanajua kwamba kwenye hizi timu kuna mashabiki zao hivyo wanapaswa kuwaburudisha bila kujali timu zao na wakikataa kufanya hivyo maana yake wamewakatili mashabiki wao.
Haya leo katupwa na hajapewa hata shilingi angeichukua milioni 30 ya Yanga si ingemsiadia pakubwa? Kimuziki sasa hivi Tunda hana hata thamani ya kulipwa milioni 5 halafu timu inakupa milioni 30 unakataa kisa ushabiki huyu si hajielewi, haya wenzie wanakula pande zote wanapiga pesa zao wanatengeneza maisha yeye kabaki hana pa kwenda.
Kwenye hii dunia ukiendekeza ushabiki wa mipira na vyama unaweza jikuta unapoteza fursa ambazo zingebadilisha maisga yako na kukupa utajili?
#Mbosso #Diamondplatnumz #Alikiba #Zuchu.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments