Na. Mwandishi Mkandarasi
WhatsApp. 0672493994
==================
MIAKA 33 ILIYOPITA
UZAZI ulimpiga kofi Tukae, kiasi cha kumchukua miaka therathini na tatu bila mtoto. Huwezi hisi kwa namna alivyonyong’onyea moyoni, mwilini hadi rohoni. Hakuamini kabisa katika miujiza wala watalaamu ambao wasichana wa lika lake, waliwapa sikio. Yeye alimini kuwa, Mwenyezi Mungu anampango na yeye, na siku yoyote ile anaweza kushusha mapacha.
Mwezi huu ulikuwa mbaya sana kwake, kiasi cha kutetelesha ndoa yake mpya anayodumu kwa miaka sita sasa, ukiachana na ile ya mwanzo ya aliyoachika baada ya miaka mitatu.
Yeye alikuwa na uvumilivu wa kusubiri mtoto, lakini sio kwa wengine, hasa walioshikanama upande wa mumewe. Maswali ya lini uta-muheshimisha mwanaume wetu, yalikuwa mengi sana, haswa katika kipindi hiki, kiasi cha Tukae kuvunja Imani yake.
Shetani alipoona Tukae ametikisika baada ya kumtishia ndoa yake nyingine itavunjika, akapata nafasi ya kumtawala Tukae, na kumpa wazo la kutega sikio kusikia ya walimwengu kuhusu ulimwengu wa giza na maajabu ya wataalamu.
Rafikiye, kwa jina la Zubeda, akawa sikio na jicho la Tukae. Akampa Tukae hadithi ya kutoshika mimba kwa miaka kumi na nane, na kisha akapata mtoto kwenye mwaka wa kumi na tisa.
“Nisaidie Rafiki yangu! Nakwenda kuaibika…” Tukae aliomba akiifunga mikono yake huku akiteleza kwa magoti hadi chini, pindi tu alipoyasikia mafanikio ya Zubeda kwa kupata mtoto.
“Hakuna haja ya kuniomba kwa namna hiyo. Ni wajibu wangu kukusaidia” Zubeda alisema.
“Nitashukuru sana!”
Zubeda alikunjua tabasamu. “Hata hivyo umechelewa shoga’angu, ungenipa sikio mapema, ndoa yako isingefikia hatarini” Akasema. Akisahau kuwa hata yeye alihangaika miaka mingi tena zaidi ya Tukae.
Siku iliyofuata ilikuwa ni fasiri baina yao, waliekea hadi kwa mganga mmoja wa jadi ambaye alisifika kwa kutoa huduma nzuri bila ghalama kubwa, na kama ni kafara, basi ni mbuzi au kuku, kikubwa tu, kafara iwe katika mazingira rafiki inayopatikana mteja wake.
Mganga Mitimingi, alishasoma maswahibu ya Tukae bila hata kuelezwa. Alipoishika tu mikono ya Tukae na kuitaza kupitia macho yake ya kiganga, alithibitisha kuwa Tukae amelaliwa na Wachawi.
“Kuna mmoja wa ndugu zako, hajapenda kabisa wewe kuolewa maishani mwako. Ameamua kukuziba uzazi” Mitomingi alisema bila kupepesa macho.
“Naweza kuumjua?” Tukae alipandisha presha. Akauma meno kwa nguvu na kuapiza kwa Mungu wake kuwa, hatamfumbia macho.
“Umefika kwa lengo la kutafuta uzazi, na sio shari!” Mitimingi alikoroma.
Tukae akawa mtulivu kama amemwagiwa maji ya baridi.
Basi wakapewa tarehe ya kurejea tena. Ni baada ya wiki moja, wanatakiwa kuja tena kwa Mitimingi, wakiwa na uhakika kuwa watasaidiwa na mizimu, na Tukae atajifungua salama kupitia nguvu ya mizimu anayoiabudu Mitimingi.
___________
Kama ulivyo usiku wa deni. Zubeda alimuongoza tena Tukae hadi kwa Mganga Mitomingi, na safari hii hawakukaa kabisa kilengeni. Mitimingi alitoka na Tukae, huku Zubeda akiachwa katika nyumba ya Mitimingi kusubiri majibu ya mizimu huko walikokwenda.
Walitembea kwa miguu, Mitimingi akiwa mwongoza njia akiwa na begi dogo mgongoni, na kofia ya mviringo iliyovikwa matete kichwani. Walitembea polepole bila kuongea neno hadi waliofika upande wa kusini mwa Mto Malindi, ambapo wakazi wake wameutosheleza sifa kwa kuita bahari.
Kabla ya chochote hakijatendeka, Mitimingi aliweka chini vifaa vyake na kulifungua begi lake, kisha akatoka na kitu kilichovirigwa mkononi.
“Nitakuwa mwongozaji, nawe utaikia kadiri ya imani yako itakavyokutuma, huku ombi lako la mtoto likiwa mbele zaidi” Mitimingi alisema.
“Sawa” Tukae aliitika, aibu ya uoga ikimshika kila akimwangalia Mitimingi.
“Utavaa hili vazi. Tunakwenda chini ya maji!” Mitomingi alisema.
“Ee!” Tukae alishituka.
“Huwezi kufa! Ndipo tiba inapopatikana! Tunaingia wote” Mitimingi alisema. Akijaribu kuongea na Tukae aliyeguza mwili mzima kuangalia bahari. “Vaa, tusipoteze muda hapa!” Mitimingi alisisitiza.
Tukae aligeuka na kukutana na Kanga juu ya mkono wa kushoto wa Mitimingi. Akaipokea na kuikunjua. Akajitaharisha tayari kwa kuivaa…
“Unaivaa juu ya nguo?" Mitimingi alionesha kushangaa. Ni kutokana na Tukae kutojua utaratibu" Hilo ni vazi la wakuu! Hupaswi kuvaa ukiwa na rosali, bangili, pete, cheni, saa, kibanio, shati, sketi hata chupi. Ni Kanga tu!” Mitomingi alisema kwa sauti ya ukali yenye shibe.
Muda ukapita kwa ukimya!
Ni kama Tukae hakukubaliana na masharti haya nafuu kutoka kwa Mitimingi. Inakuaje avue vitu vyake vyote mpaka kufuli na kuvaa Kanga tu kisha kuzamia majini na mwanaume?
“Baada ya dakika tatu kupita bila kujiandaa, nasitisha msaada!” Mitimngi alitishia. Kisha akamega hatua kutoka eneo hilo kumpisha Tukae aendelee kujiandaa kwa uhuru.
Dakika mbili zote alizitumia kutafakari. Fikira zake zilimzomea kwa kukabali ushauri kutoka kwa rafiki yake Zubeda. Lakini sasa ameshayavilia nguo maji, hana budi kuyaoga. Aliitumia dakika moja kujiandaa kwa haraka haraka, na hata Mitimingi alivyojitokeza, alimkuta Tukae anamaliza kuzikunja nguo alizovua na kuziweka pembeni ya mti lilipo begi na kofia ya Mitimingi.
“Ondoa mashaka. Sitakugusa!” Mitimingi alisema kwa upole, akiipoteza kabisa sura yake ya ukali. Uso wake ulimaanisha! Hakuwa na chembe yoyote yenye dalili za kongopa.
Alimaanisha!
Mitimingi akiwa na tumbo wazi, msuli pekee ukimsetiri maungo yake ya chini, aliongoza njia kuielekea bahari, na hakukuwa na mtu mwingine yoyote kwa upande huo aliyekuwa anashuhudia tukio hilo, isipokuwa wao wawili.
Tukae na Mganga Mitimingi.
Hao wanaelekea zao chini ya Bahari
.
.
.
Season ya Pili Kila Mtu Asome....
Imeanzia Mbali Kidogo. Kama ukifanikiwa Kusoma Vipande 10 vya mwanzo, nadhani tunakwenda Pamoja.
@highlight.