Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Zuchu Ft Diamond Platnumz - Inama

KICHAA NA MIMBA YA BOSS SEHEMU YA NANE*

10th Sep, 2025 Views 23



Doctor hakumuangalia mama Farida Jinsi alivyokuwa ametahayari na wakati huo Shania alikuwa haelewi chochote alitulia huku akiwa anaangalia mamcho pale ndani.

"Pole sana mama. Hili limeshatokea hauna budi kilipokea. Asante baba Mama Farida alimuangalia

Shania kwa jicho la huruma alitamani kuongea nae kitu lakini alijua ni kazi bure hataweza kupata majibu ya maswali yake. Alimshika mkono Shania wakatoka chumba cha daktari na kurudi nyumbani.

Walifika nyumbani wakafikia nje kwenye kimvuli cha mti.

"Vipi mama mbona imechoka hivyo?.

Farida mwanangu ni haki nichoke kwa hilo. lililonifika. Farida alitaka kukaa lakini mama yake akamzuia.

"Usikae kwanza, ingia ndani kaniletea maji ya kunywa nahisi kuna kitu kime nikwama kwenye kioo. Farida aliingia ndani akaenda kuchukua maji wakati huo mama Farida alikuwa akimuangalia sana Shania ambae alikuwa hana habari.

"Huyo mwanaume alianzaje kumbaka mtu kama huyu, kwani hakuona hali yake au ndio hawa wanaoamini mambo ya kishirikina?

Mara Farida alirudi akiwa na grass ya maji.

"Mama mbona unaongea mwenyewe?

"Dunia imenizonga Farida hii dunia sijui ina watu wa aina gani?

"Unamaana gani kusema hivyo mama? Aliuliza Farida huku akiwa anakaa na mama yake

alikunywa kwanza maji ndipo akatoa jibu. Shania ni mjamzito. Farida alishituka.

"Mama...

"Ndio hivyo, hata mimi nilishituka kama wewe. "Mmmh inawezekana vipi Shania kupata mimba

7

"Hujui kapataje? Wakati huko mitaani kuna watu. wa hivyo kabisa.

"Ni kweli, lakini kama alibakwa itakuwa sio

mwanaume mmoja alimshika na ingejulikana tu kuwa Kabaka hapa lazima kuna njia iliyotumika kumlaghai.

Kwanini unafikiria hivyo?

Mama Shania namjua vizuri sana huwal hapendi kujichanganya na wanaume tena

hapendi hata kuguswa. "Sasa unataka kuniambia hii mimba kapewa na

mwanamke? Sijamaanisha hivyo ila kwa hisia zangu nahisi kuna njia imetumika.

Achana na hizo hisia ndio imeshatolewa mwenzio ana kijusi huko tumboni kwake. "Masikini.

"Mwenzio naweza nitamdhibiti vipi na hiyo hali na mtu mwenyewe kama unavyojua hali yake. Mama kama Mungu ameamua apate huo ujauzito basi hawezi kuacha aadhalilike kila kitu kitakuwa sawa.

Siku chache badae Shahid akiwa amelala kitandani kwake na Aisha, Shahid alikuwa anaota ndoto huku akiweweseka na kulitaja jina la Shania na jasho jinginoilikuwa likimtoka.

Wakati huo Aisha alikuwa macho akimuangalia, Alimpiga piga shahidi bagani na Shahid alizinduka kutoka usingizini.

"Unaitwa hebu kaa tuongee.

Shahidi alichukua simu yake akaangalia saa. "Sasa hivi saa tisa usiku unataka tuongee nini?

"Nataka kukuuliza swali langu moja tu na kama utanijibu nikaridhika tutalimaliza mapema.

"Mmmh nakusikiliza

"Shania ni nani?

Shahidi aliposikia jina la shania alishituka lakini

akapoteza na kuuliza

"Sijaelewa swali lako Shania ni nani kivipi? Mara kwa mara umekuwa ukiweweseka na kulitaja jina la shania sasa nataka kujua ni nani?

Kama ni mwanamke wako nijue leo. "Hivi yote hayo yanatokana na wivu au kuna kitu gani hasa?

"Mmmh yani utaje jina la mwanamke mara kwa mara ukiwa usingizini alafu mimi nikae kimnya tu.

"Hata mimi simjui huyo Shani sijui nani na ninamuomba Aisha sitaki usumbufu na maswali

ambayo hayana maana Shahidi alimgeukia upande wa pili akajifunika shuka na kuendelea kulala.

Siku zilienda Shahid bado hajamtoa Shania kwenye kichwa chake mara nyingi alikuwa

akimkumbuka na kutamani sana kumuona. Siku moja baada ya kutoka kazini alienda ufukweni mwa bahari na kuanza kuzunguka huku akiwa na imani atamuona Shania.

Muda ulizidi kwenda lakini Shania hakutokea Aliamua kuondoka, alipofika sehemu alimuona

yule kijana muuza chips ambae alimpigia simu Farida na kumueleza kuwa Shania kaonekana. Shahidi aliamua kumfuata. "Mambo vipi?

Safi bro karibu.

"Asante, sijui unanikumbuka? Shahidi aliuliza na yule kijana alimuangalia kwa makini.

"Ndio, ndio nimekukumbuka kaka, karibu.

"Asante. Samahani hivi siku hizi Shania yuko wapi maana nina muda mrefu kidogo

sijamuona.

Aisee Shania sasa hivi huwa haki hapa maral

kwa mara na sijui ana shida gani ila yupo. "Ahaaa nilitaka kujua tu maana sisi ni binadamu na Shania alikuwa amenizoea sana.

Ni kweli ila kuwa na amani atakuwa yupo salama kama kungekuwa na tatizo tungesikia. Huenda Kapata Chimbo lingine huko.

"Poa, poa acha mimi niende. "Sawa bro karibu sana.

Shahidi aliondoka lakini alijisemea moyoni.

"Natakiwa kumuona Shania, nitafanya juu chini nimuone siwezi kuishi kwa amani bila kumuona.

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

KICHAA NA MIMBA YA BOSS SEHEMU YA NANE*  >>> https://gonga94.com/semajambo/kichaa-na-mimba-ya-boss-sehemu-ya-nane

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Zuchu Ft Diamond Platnumz - Inama
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest