"Shahid umetoka wapi na vichaa? Mmoja wa
marafiki zake aliuliza
Kichaa nae mtu Acha niwaache tutaonana wakati mwingine. Shahidi alinyanyuka akamshika mkono Shania wakawa wanaondoka. huku watu waliokuwepo kwenye ile sehemu
wakiwaangalia.
Na kila mmoja alifikiria kivyake pia kuna wengine walisema anamtuma vibaya Shania lakini Shahid hakuwa wa kujali watu wanachosema pia alizingatia sana maamuzi na misimamo yake. Umekula? Shahidi alimuuliza huku wakiwa
wanatembea,
Nilikuwa ugali saileeee.
Sasa hivi njaa ina kuuma?
Ndio inauma sanaaaa
Sasa unataka kula nini? "Kuku. Alijibu Shania haraka haraka
"Sawa twende.
Walienda kupanda kwenye gari Shania alifurahi sana kupanda kwenye gari ni kama kilikuwa kitu kigeni kwake.
wakaelekea sehemu ya fukwe wa bahari.
Walipofika Shahid alienda kununua Chipsi kuku kisha wakaenda kukaa sehemu na kuanza kula. Rafiki mshike mtoto mimi nile kwanza nikishika
nitannyonyesha Shahid aliushika yule mdoli wakaendelea kula.
Shania nyumbani kwenu ni wapi? Kule... Aliongea huku alinyoosha kidole.
Leo unanipeleka nyumbani kwenu nikapajue. Shania aliitikia kwa kichwa huku akiendelea
kula.
Baada ya kushiba alimchukua mdoli wake na kutoa ziwa lake kisha akamsogeza mdoli kifuani kwake ikawa kama mama anamnyonyesha
mtoto wake
Shahidi alipoona ziwa la Shania alishituka na kugeukia pembeni ziwa lililokuwa bado la binti mbichi, lilikuwa bado limesimama yani Chuchu
saa sita na licha ya kuwa mchafu usoni na
sehemu nyingine lakini kifua chake kilikuwa cheupe na ngozi yake ilionekana kuwa nyororo, Kwa kiasi flan Shahid alihisi damu zinakimbia. mwilini mwake, aligeuka tena kuangalia Shania
hakuwa anajali, haraka Shahid aligeuza macho yake na kuangalia pembeni. Wewe niangalie Ilham ananyonya, anapenda
kunyonya huyu Shahidi hakugeuka, Angalia basi huku mwenzio niliumia hapa.
Shahidi alitupia jicho kuangalia mara moja na kurudi kuangalia pembeni
Hahaha Unaogopa eeeee... Unaogopa
kuangalia kidonda.
Masikini Shania hakujua kama anamuweka kijana wawatu kwenye wakati mgumu kwa kuona ziwa lake.
Shahidi akiwa bado anaangalia pembeni shania alisimama na kumpiga kibao kidogo begani. Kidalipo Kalale nacho....alisema shania huku
akiwa anakimbua na kutokomea huku Shahid
akiwa anamsindikiza kwa macho.. Huu sasa mtihani hakuaogopa hata kunifunulia mwili wake.
Taratibu Shahidi alinyanyuka na kufuata gari lake na kuelekea nyumbani kwake. Alipofika nyumbani kwake alipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwake alivua nguo na
kwenda bafuni kuoga. Akiwa amesimama kwenye bomba Maji yakimwagika mwilini mwake mawazo yake yote yalikuwa kwa Shania,
alikuwa akifikiria kifua chake alichokiona.
Aaaah sijui kwanini huyu shetani ananiweka kwenye kumbukumbu mbaya kiasi hiki. Shania ni mtu asiwe kuejielewa sitakiwi kumfikiria na kumuweka kichwani kwa kile nilichokiona.
Kesho yake Shahid akiwa ofisini kwake simu yake ya mkononi iliita, aliekuwa anapiga alikuwa ni mlinzi.
Hallow
Boss yule kichaa yupo hapa kama ulivyosema akija nikwambie.
"Sawa nakuja.
Shahidi alikata simu kisha akaweka vizuri faili lililokuwa akilipitia alafu akatoka. Alimkuta Shania akiwa kasimama nje ya geti
alichungulia ndani, alipomuona Shahid anaenda alianza kucheka huku alinyanyua mdoli wake na kumuonyesha kwa Shahid.
"Ilham baba yule anakuja Mlinzi na wanaume wawili waliokuwa wamesimama pale getini walicheka kimnya.
kimnya, Shahid aliwaona lakini hakujali.
Toka hapa anacheka nini sasa. Shania aliwafokea kisha akarudisha macho kumuangalia Shahid.
Shahidi alipofika karibu Shania akamuita. "Baba Ilhamu naomba mia mbili.
Sawa nakupa uende ukale.
Haya na Ilham nae atakula.
Sawa. Shahidi alitoa hela na kumpatia Shania alifurahi akawa anaondoka huku akiangalia ile hela ya noti.
Bye, Ilham muage baba, Shania aliushika mkono wa mdoli wake huku akiwa anafanya
kama anamuaga na Shahid alimpigia mkono. Wakati anageuka ili arudi ofisini kwake akakutana uso kwa uso na Rashidi.
"Hiki ni kitu gani unaleta hapa Shahid? Kwani vipi? Huyu kichaa umemzoeshs kuja hapa huoni
kama inaleta picha mbaya kwako?
Sijali alafu haina madhara yeye kuja hapa sababu nachukulia kama mtu wa kawaida. mwenye kutaka msaada kwangu.
Mmmh mtu wa kawaida wakati chupa
Inapooza ile. Acha dharau kumbuka kabla haujafa. haujaumbika.
Sawa lakini hapana kuwa na ukaribu na mtu ambae dishi limeyumba ni kujishushia heshima yako kwanza jiangalie wewe ni nani.
Mimi ni mtu na yeye ni mtu. Alijibu shahidi kisha akaondoka. Rashidi alimuangalia kisha akacheka kidogo na kutingisha kichwa.
Daaaah na imeshapewa jina baba Ilham kweli dunia inaenda kasi sana. Mama Ilham kaka. kumtembelea baba Ilham, kaka kuchukua hela ya matumizi. Baba Ilham uwe unaacha pesa ya
matumizi kabla ya kuja kazini
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Maoni