KWANINI NI VIGUMU SANA KUISHI NA MWANAMKE AMBAYE AMEUMIZWA SANA KWENYE MAHUSIANO YA ZAMANI?
Ni vigumu sana kumshawishi Mwanamke ambaye ameumizwa sana kwenye mahusiano/ndoa ya zamani kuwa kuna wanaume wazuri ambao wanaweza kumjali, kumthamini, kumpenda na kumpa heshima kisha Mwanamke huyohuyo akubali kumheshimu,kutii mamlaka ya mwanaume wakati huohuo mwanamke huyo ametoka kuumizwa sana hisia zake kwenye mahusiano/ ndoa ya zamani.
Wanawake wengi baada ya kuumizwa sana hujenga chuki dhidi ya kila mwanaume mpaka kufikia hatua ya kuwaita wanaume wote ulimwenguni kuwa ni "mbwa" au "nguruwe".
Chuki, kinyongo, wivu uliopindukia na hisia za kisasi dhidi ya wanaume husababisha mwanamke anakuwa mkali kupitiliza,anakuwa mbabe,anakuwa mbishi, anakuwa haambiliki, hashauriki, anakuwa mjuaji, anakuwa na misimamo mikali sana,anakuwa anaishi kwa kujiamulia lolote bila hofu maisha yake.
Wanaume wenye upendo, huruma, uvumilivu,wanaume wenye malengo ya kudumu na kujenga familia imara huteswa sana kwenye mahusiano/ndoa kwa sababu Mwanamke haitaji kuwa na mwanaume maishani mwake huku mwanaume yeye anakuwa king'ang'anizi anataka waishi pamoja na kulea watoto.
MWANAMKE HUUMIZWA SANA KIHISIA KWA NJIA ZIFUATAZO
Kila Mwanamke ambaye amebeba chuki, kinyongo, upweke kupitiliza, hisia za kisasi dhidi ya wanaume anakuwa amepitia matukio yafuatayo
1.MAHUSIANO YA NYUMA
Matukio ya zamani kwenye mahusiano/ ndoa yenye kumfanya mwanamke anajenga chuki, kinyongo, upweke kupitiliza,hisia za kisasi dhidi ya wanaume ni
~Fumanizi za mara kwa mara,vipigo, matusi, kudhalilishwa, kuingiliwa kinyume na maumbile, kuingiliwa kinguvu, kunyimwa unyumba kwa makusudi kwa muda mrefu sana, kufukuzwa nyumbani usiku wa manane, kulazwa nje,
~Kupokonywa mali, kudhulumiwa mali zake ambazo amenunua bila msaada wa mwanaume
~Kuachwa ghafla baada ya kuachishwa kazi au masomo kwa ahadi ya kufunguliwa biashara au kuolewa
~Kutelekezwa na ujauzito au watoto
~Kuachwa ghafla siku ya harusi yaani ex wake anasubiri pale watu wapo ukumbini anakaa kimya,anazima simu haipatikani kisha anatokomea kusikojulikana
~Kifo cha ghafla cha ex wake
~kuambukizwa ugonjwa usiokuwa na tiba kama UKIMWI kisha anatelekezwa ghafla
~Kushawishiwa afanye mapenzi kinyume na maumbile kisha baada ya njia ya haja kubwa kuharibika anatelekezwa ghafla
~Kuachwa ghafla na ex wake baada ya kumchukulia mkopo, kumsomesha, kumpa mtaji, kuwajengea wazazi wa mwanaume, kumkabidhi ATM card yake, kumuuguza sana ex wake.
2.MALEZI YA UTOTONI
Mwanamke anaweza kujenga chuki, kinyongo, wivu wa mapenzi kupindukia dhidi ya wanaume kwa sababu ya malezi ya utotoni kama ifuatayo
~Binti kuona mama yake mzazi anapigwa, kubamizwa ukutani, kupokonywa mali, kutelekezwa na ujauzito au watoto
~kubakwa au kulawitiwa
~kuona mama yake mzazi anafukuzwa nyumbani kwao usiku wa manane
~kuona baba yake mzazi anaingiza mahawara zake kwenye kitanda alichokuwa analala mama yake kisha mama yake mzazi analazimishwa kulala chumba cha watoto au nje.
haya yapo ndani ya kitabu cha JINSI YA KUPONA MAUMIVU MAKALI SANA MOYONI.
#Spirit_Warrior
#Wounded_Healer
π€Ίπ€Ί
Kama tatizo lako ni kubwa zaidi tunaweza kuwasiliana kwa ajili ya Counselling session na ufafanuzi wa kilichoandikwa hapo juu na utaona mabadiliko na kujisikia nafuu ndani ya muda mfupi baada ya mazungumzo.(Counseling kwa njia ya simu gharama Tshs 30000 , kuonana uso kwa uso Tshs 40000
Kwa wapenzi wa kusoma vitabu unaweza kupata nakala zangu orodha ipo chini π
Kupata kitabu cha
1.JINSI YA KUPONA MAUMIVU MAKALI SANA MOYONI - (Softcopy Tsh 30000)
2.UTULIVU WA AKILI KIPINDI KIGUMU (Softcopy)
3.FIKRA ZAKO FURAHA YAKO (softcopy)
4.TIBA YA MSONGO WA MAWAZO (by & Softcopy)
5.MALEZI YA UBONGO KISAYANSI( hardcopy & softcopy)
6.TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA (Hardcopy & softcopy)
7.MISINGI 10 YA FURAHA SIKU ZOTE (hardcopy &softcopy)
8.BADILI FIKRA ZAKO BADILI MAISHA YAKO
BEI Kitabu kimoja softcopy 5000 isipokuwa kitabu namba 1 bei yake ni Tsh 30000, hardcopy moja 10000
Mawasiliano
+255766862579
+255622414991
Imeandikwa na Psychologist
Said Kasege
Temeke,Dar es salaam.