Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:01

24th Aug, 2025 Views 29


Leo nataka niwape hadithi ya maisha yangu, hadithi ambayo mtanitumia mimi kama mfano na kuishi mazuri yangu na kuachana na mabaya yangu ambayo nitakuwa nimeyafanya katika maisha yangu.

Jina langu ni Rodrick, mimi naitwa Rodrick. Sitaki kukuzungusha sana, nitaenda moja kwa moja na mengine tutajua hapahapa nitajitahidi sana uelewe kila kitu.

Nataka tu nianzie pale maisha yangu yalipoanza kuonesha upande wa pili wa dunia yangu. Na hapa ndiyo niliamini kuwa hakuna kitu hutokea bahati mbaya kwa maisha ya mwanadamu, kila kitu kina sababu, iwe nzuri au mbaya lakini tayari ni sababu na sababu hiyo itakupeleka mahali. Na hii ndiyo ilinitokea na mimi.

Mimi kwenye maisha yangu ninaye mchumba ambaye sasa nalazimika kumuoa kwasababu ana mimba yangu. Ninampenda, ndiyo nilikuwa naona hivyo, lakini kumuoa sikuwa tayari lakini familia yangu, na familia ya mpenzi wangu Gabriela zilikuwa zinasisitiza sana juu ya ndoa yetu kwasababu ya hadhi na heshima zao watawezaje kuficha hili hivyo ni lazima tuoane.

Hata yeye mwenyewe mpenzi wangu G, aliniambia kwa kudeka “eenh Rodrick, sasa mpenzi, nina mimba, tuoane au hunipendi babe eenh, niambie nijue.”
Nilimtazama na kusema kwa upole “G unajua sana kuwa mimi nakupenda unajua hilo, lakini kuhusu kuoa nilikuwa bado.”

G alinitazama na kusema “hofu yako ni nini sasa, tuna kila kitu Ricky, kila kitu tunacho sasa sijui unataka nini?, au mwenzangu hunipendi kama ninavyokupenda, kama hunipendi niambie, tell me.”

INAENDELEA..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:01  >>> https://gonga94.com/semajambo/loml-love-of-my-life-01

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Ratiba ya Simulizi

  • PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA TATU. 25-08-2025 05:55

Ratiba ya Simulizi

  • PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA SABA 25-08-2025 07:00

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest