Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:03

24th Aug, 2025 Views 4


Alicheka akisema “si unaniona na shemeji yako?, sisi tupo tutumieni ili kuweka mambo sawa ndiyo maana ni walezi wenu. Hatupo hapa kusimama tu ina maana sana.”

Tukacheka na kukumbatiana. Baada ya hapa, watu walianza ingia kwa magari, na G sasa ananifuata na maringo yake ya kudeka “Ooh baby lets go, twende Mine Man.”

Hapo tayari yupo mwilini, hata msimamizi ananitazama anacheka akisema “unaona mambo hayo, haya tangulieni kwa gari na mimi nimfuate babygirl wangu.”
Tulicheka tu.

Sasa nikiwa ndani ya gari, hapo mpenzi G na simu kila muda picha mpaka natamani kumwambia pumzika kidogo nipate hata kupumua nakasirika na la kufanya sina. Nikawa natazama tu dirishani, sielewi hata nifanye nini nipumzishe fuvu langu maana G ana hekaheka.

Si unajua wale wasichana kila kitu ni kuonyesha na wengine wajue anacho basi ndiyo G wangu. Ana maisha safi, msomi, pesa kwake sio shida ila kujisikia, na kujiona yeye ndiyo yeye hayo ndiyo maisha yake.

Basi akawa ananilazimisha ni tabasamu, nicheke ili mradi tu apate picha ambazo yeye anataka kwaajili ya matumizi yake. Nikawa sasa nimechoka. Wakati nikiwa natazama dirishani, upande wa pili kutoka pale tulipokuwa, nilimuona msichana mzuri sana, ninarudia tena, msichana mzuri sana sana sana.

Amevaa lubega, halafu mikononi ana fimbo sijui ni ya kazi gani ila alikuwa na fimbo. Na hiyo Lubega sio kwamba yupo wazi juu hapana inaonekana amevalia gauni kwa ndani sasa sijui sababu ya Lubega.

Jinsi alivyo tu nilijikuta natabasamu, na ilivyo ajabu nilikuwa nahisi kama ana tabasamu na mimi hata na mimi nikawa natabasamu kıla nikimtazama. Huyu mwanamke ni mzuri sana.

INAENDELEA.
.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:03  >>> https://gonga94.com/semajambo/loml-love-of-my-life-03

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Ratiba ya Simulizi

  • PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA TATU. 25-08-2025 05:55

Ratiba ya Simulizi

  • PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA SABA 25-08-2025 07:00

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest