Niliendelea kumsaili huku moyoni nikisema “ni mwanamke anayevutia sana, amenivutia, ni mzuri sana.”
Sijui hata kama unanielewa, nimetoka kanisani na kwa Mara ya kwanza naona kabisa nimekutana na love of my life (LOML). Sijamaliza hata kumtazama huyu mwanamke dereva naye alikuwa anaondoa gari.
Nilikuwa hata nainamia, nataka kumuona yule mwanamke mzuri. Lakini nashindwa, nilichukia, nilitamani tu nishuke ila nawezaje.
Sasa hapo G ananiambia “Mine Ricky, upo ok?”
Nilimtazama, sio kwamba Gabriella ni mbaya, ana uzuri wake na si unajua mwenye pesa anajitunza vizuri ni mwanamke fulani hivi wa hadhi. Yule mwanamke ukimuona unajiuliza nimfuate au basi achana naye.
Ni mzuri ana jipenda sana. Lakinu sasa yule nimemuona ana uzuri wa asili na pale ndiyo maisha yake magumu. Ni kama malaika amenipa tu mwanamke siku ya ndoa yangu.
Aliniuliza tena akideka “Ricky wangu. Please dadie, niambie are you happy?”
Nilijikuta nina furaha sana nikisema “very happy, nina furaha sana G.”
G alitabasamu na kusema “nashukuru sana mume wangu, nakupenda sana mume wangu mzuri na asante kwa kukubali kuwa mume. Nakupenda.”
Nilimtazama na kusema “nakupenda mke wangu.”
Nilimkumbatia, lakini kumbato lote hili, akili yangu ipo kwa yule msichana ambaye hata jina lake silijui, lakini moyo wangu tayari umehisi uwepo wake, ni msichana wa aina yake.
Moyo wangu umemtambua na hisia zangu zimemwangukia, nahisi ninampenda sana yule mwanamke, mwanamke mgeni nisiye mjua na sijui hata wapi nitamuona tena.
INAENDELEA..
Maoni
Click here to login and comments