Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:06

24th Aug, 2025 Views 4


Nakumbuka sana, nakumbuka usiku huu sasa tulienda fungate hotel kubwa sana hapo ni tunalala usiku huo na kesho ni safari kuelekea Zanzibar sehemu pekee ambayo mimi nilipendekeza badala ya Dubai, sikuona haja ya kwenda kote huko kutumia pesa wakati ninayo mambo mengi ingawa pia kwa Gabriella haikuwa rahisi kumshawishi.

Tulifika mpaka hotel, tulipofika sasa mke wangu, alinikumbatia na kusema “sasa ni mke halali wa Ricky, mpenzi wangu nakupenda sana, Wewe ni kila kitu nataka kukamilisha ulimwengu wangu. Wewe ukianguka tunaanguka wote, na ukiinuka tupo pamoja mpenzi wangu. Ricky mimi hapa mwenzako nakupenda si unajua babaaa eenh, na mtoto wetu akija atajivunia sana kuwa na baba na mama kama mimi. Nakupenda Ricky wangu.”

Nilimtazama na kutabasamu, halafu nilimwambia “Wifey, nakupenda unajua hilo.”
Alitabasamu na kusema, “I know bedmate, nakupenda.”
Nilitabasamu, akauma mdomo wake wa chini na kisha aliniambia “bedmate leo nataka kuufanya huu usiku kuwa usiku wa kipekee sana, usiku wetu wa kwanza, hatujuani ndiyo tunakutana hapa. Nataka usiku huu unikumbuke kila mahali yaani. Ukiwa kazini, matembezini, barabarani, popote pale mpaka kwenye vikao unikumbuke mimi.”

Nilitabasamu na kisha nilimtazama nikisema “waooo una maanisha?”
Alitabasamu na kusema “Yes, kabisa bedmate naenda kuoga twende wote basi mpenzi.”
Nilimtazama na kusema “tangulia, nakuja.”
Alitabasamu.

Mke wangu huyu alipoingia bafuni, mimi nilibaki pale kitandani nimechoka. Sina hata hamu na mke wangu kiukweli kabisa. Hii fungate natamani iishie leo kesho mimi nirudi zangu kumtafuta yule msichana walau nimuone tena. Kuna kitu kimenikaa tu hapa, natamani kumuona mrembo yule tena na tena, natamani yeye ndiyo angekuwa hapa, ningekuwa na yeye hapa.

INAENDELEA..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:06  >>> https://gonga94.com/semajambo/loml-love-of-my-life-06

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Ratiba ya Simulizi

  • PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA TATU. 25-08-2025 05:55

Ratiba ya Simulizi

  • PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA SABA 25-08-2025 07:00

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest