Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:10

24th Aug, 2025 Views 6


Tulielekea kula, tulipofika kula mke wangu sasa anapiga picha kila kitu, mara nipige picha. Mimi tena ndiyo mpiga picha, chakula kinapigwa picha mpaka nachukia na ni muda wa kula. Alipomaliza alitabasamu na kusema “tule sasa Hubby.”

Nilishusha pumzi tu, alichukua uma wangu na kunilisha. Kisha aliendelea kula huku akiwa anazungumzia ndoa yetu namna imeenda viral, watu wanazungumzia, marafiki zake na zawadi.

Mimi nilikuwa nakula, namuwaza yule binti niliyemuona kanisani. Kisha nilikuwa nashindwa kabisa kujizuia kutabasamu. Nilijikuta natabasamu tena tabasamu pana kabisa. Mke wangu alinitazama na kuniita kwa Jina langu “Ricky!!”

Mimi nikaendelea tabasamu, akaniita tena “Ricky!!”
Nilimtazama na kusema “Naam!!”
Aliniuliza kwa kunishangaa “unatabasamu!!.”
Nikatabasamu tena na kumuuliza “kwani vibaya kutabasamu na mke wangu?”

Na yeye alitabasamu na kusema “kumbe nakufanya utabasamu, napenda hiyo mume wangu.”
Nilimtazama tu nikitabasamu kumbe mimi uzuri wa msichana yule ndiyo unafanya natabasamu na wala sio yeye. Moyo wa mtu kichaka. Tukiwa na hali hiyo mara simu ya mke wangu iliita. Aliitazama na kunitazama, nikamuuliza “kuna nini tena?”

Alishusha pumzi na kusema “ni mama, sijui anataka kusema nini?”
Nilimtazama nikisema “pokea, labda wanakusalimia tu.”
Ndipo mke wangu alipokea simu, alipopokea tu nikaona uso wa mke wangu unapoteza furaha, nikamuuliza “kuna nini?”
Mke wangu aliendelea kusikiliza simu huku akinitazama kwa hofu, na kisha alikata simu na kusema “ 😂😂😂sa itakuaje🤦‍♀️🤦‍♀️🤦‍♀️

INAENDELEA..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:10  >>> https://gonga94.com/semajambo/loml-love-of-my-life-10

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Ratiba ya Simulizi

  • PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA TATU. 25-08-2025 05:55

Ratiba ya Simulizi

  • PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA SABA 25-08-2025 07:00

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest