Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:11

24th Aug, 2025 Views 6


“Dadie, ni mama, kazini mambo sio mazuri, tangu alfajiri baba anafuatulia na hakuna kitu anaweza kufanya sasa maana amechoka sana. Kuna kampuni tulikuwa tunafanya nayo kazi naona ina leta usumbufu na baba peke yake na meneja sidhani kama wataweza kama unavyojua mimi ndiyo nipo ofisini muda mwingi. Mume wangu, tunaweza kughairi hii safari kwa sasa then tutapanga upya walau sasa nimsaidie baba yangu?, tafadhali baby, please nakuomba.”

Nilitamani ajue namna nimefurahi, maana tu siku ya kwanza hii fungate ilikuwa imenichosha na kunipa mawazo sana kichwani. Nilikuwa sijaifurahia kabisa. Unaweza kuniona nina matatizo pengine au labda sina akili nzuri lakini niamini hivi ndiyo nilikuwa ninajisikia. Roho yangu juu ya mke wangu imeingia uzito sana. Nilikuwa naona kila kitu kibaya hapa.

Nilimshika mkono na kusema “poleni sana mke wangu, mimi sina neno kabisa kwasababu hili ni jambo muhimu sana. Unahitaji msaada wowote ule kutoka kwangu?”

Gabriella alinitazama na kuniambia “nashukuru sana mpenzi wangu, najua nimekatisha wakati wetu mzuri sana. Nakuahidi nitalipia wakati huu Dadie. Sasa wacha twende nyumbani wewe ukapumzike na mizigo niache hapo halafu baada ya hapo niingie kazini.”

Nilimtazama na kusema “hakuna tatizo kabisa, kama unahitaji nikupeleke kazini pia ndiyo nirudi nyumbani ni sawa, hata kama unahitaji nikae hapo kazini nikusubiri pia ni sawa.”

Mke wangu alicheka kidogo, lakini tayari ninamfahamu suala la kazi uso wake tayari haukuwa na raha.

Mke wangu na mimi tulianza kurudi chumbani. Sasa hapa ndiyo nilianza kumuona namna anakuwa na kazi zake. Ni muda wote simu, akitoka kuzungumza na huyu anaongea na huyu. Nilikuwa namtazama tu, yeye akinitazama anatabasamu lakini haachi kuzungumza na simu na wakati mwingine maagizo yenyewe anarudia. Wakati mwingine tena anarudi kwa mama yake na kumuelezea namna anaweka mambo sawa basi vile akisifiwa mke wangu mimi ndiyo mimi huku kwangu mambo yanazidi ni simu simu na yeye.

INAENDELEA..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:11  >>> https://gonga94.com/semajambo/loml-love-of-my-life-11

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Ratiba ya Simulizi

  • PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA TATU. 25-08-2025 05:55

Ratiba ya Simulizi

  • PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA SABA 25-08-2025 07:00

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest