Sijui maongezi yao mengine yalikuwa ya aina gani ila baada ya muda mama alikuja chumbani kwangu akaniomba nimpe album ya picha zangu..
Nilimpatia akaondoka nayo baada ya muda aliirudisha ila picha mbili hazikuwemo..
Mimi sikujua kilichofuata zaidi ila usiku ulipofika mama aliniletea simu niongee na mama mchungaji..
Nahisi mama alishamuelezea hali halisi na akamuomba amsaidie kunibembeleza๐๐
Mama mchungaji aliniambia Maya mimi ni mtumishi wa Mungu je una wasiwasi wowote juu yangu?..
Nikamwambia hapana mama sina wasiwasi wowote juu yako...
Unahisi naweza kukuletea mtu asiye sahihi kwenye maisha yako??? Nikakaa kimya๐๐๐..
Mama mchungaji aliniambia hii familia mimi naijua vizuri mnoooo ni watu wazito si kitoto na ni wacha Mungu๐๐hautojutia kuolewa pale..
Na usifikilie et ukiolewa ndo hauwezi kusoma tena no๐๐๐shule utaenda kama kawaida..
Mama mchungaji alinihusia mno mwisho akaniambia hata yeye alitamani angekuwa na mtoto wa kike yeye ndo angeolewa na Rouhy....
But kwa sababu ye hajajaaliwa mtoto wa kike basi hakutaka hiyo bahati iende mbali ndo maana ameamua anipe mimi...
Bado sikuwa tayari jamani kuolewa ni ishu ingine mjue๐คฃ๐คฃ๐คฃalafu mkaka mwenyewe alivo mzuri nahisi ana mkeka wa mademu๐๐..
Nilivyo kapole maskini kazi yangu itakuwa ni kulia lia tu huko kwenye ndoa๐คฃ๐คฃ๐คฃnilitamani wazazi wanielewe kwenye swala lile lakini ilishindikana..
Siku iliyofuata yule mama na mama mchungaji pamoja na baba mchungaji walirudi tena pale nyumbani kwetu kwa ajili ya kuongea na mimi..
Na awamu hii walikuja na kila kitu kinachotakiwa katika mahari yangu๐ฐ๐ฐndo naondoka hivo Mungu wangu๐ฅน๐ฅน bado nilikuwa siamini ninachokiona..
Mama Rouhy aliniambia kijana wake kuna kitengo nyeti sana amekabidhiwa serikalini na inatakiwa awe na mke haraka iwezekanavyo kabla hajaapishwa๐ฅบ๐ฅบ..
Mama Rouhy alinisihi sana nikubali ndoa na akanihakikishia sitojutia...
aliniambia ataenda kunilea na kunidekeza kama alivyokuwa ananidekeza mama yangu๐ฐ๐ฐ..
Kwa vile wazazi wameshaamua mimi wala sikuwa na kauli..
Wazazi walipewa kitita cha pesa nyingi sana kama mahari na visindikiza mahari na baada ya hapo walipewa pesa zingine kwa ajili ya kunifanyia maandalizi ya ndoa..
Ndoa yangu ni miongoni mwa ndoa zilizofanyika kwa haraka zaidi kuliko kawaida..
Yani baada ya mahari kutolewa siku iliyofuata nilienda kutafutiwa nguo na shopping ya vitu vingine....
Then jioni ilipofika wazazi wakaalika majirani na ndugu waje harusini kesho yake๐ฅน๐ฅน๐ฅนniliwanuniaaaa sana..
Kesho ilipofika niliandaliwa kwa ajili ya kuolewa imajini naolewa na mtu sijamtia hata machoni๐ฐ๐ฐ
Ni picha tu ndo nimeona naye akatumiwa zangu basi๐ฅน๐ฅนhata sauti yake tu sijaisikia...๐
Baada ya kuandaliwa tukakaa kidogo tukaambiwa Bwana harusi tayari ameshawasili hivo inatakiwa tuelekee kanisani..
Zile zile gari alizokuja nazo bwana harusi kutoka mjini ndo zilizokuja kutuchukua kutupeleka kanisani..
Nyieeeee tumefika kanisani nikatelemshwa kwenye gari tukaanza kumach kuingia kanisani๐๐๐
Wakati tunaendelea kusogea mbele pale alipo Rouhy nikawa najaribu kukodoa macho kiwizi wizi namwangalia naye macho yake yote alikuwa ananiangalia mimi๐...
Kichwani nilikuwa nawaza tu muda wa yale mambo mengine itakuwaje๐๐mkaka alivyojazia yule namimi nilivyo kadogo si ataniua mimi katoto ka watu๐ด๐ด๐ด
Hahahaaaaa sijui itakuwaje,??... nikusihi ujiunge nami katika sehemu inayofuata...
Itaendeleaaaaaaa
KWETU morogoro.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.