Katika Qur-aan na Hadiyth kumetajwa moto kuonesha mazingira mabaya watakayoshukiwa watu waovu, Waliompinga Allaah na kuendesha maisha yao ya hapa duniani kinyume na kanuni na taratibu alizoziweka Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala).
Maisha ya motoni ni kinyume na maisha ya Peponi ambayo picha yake tumeshaiona. Tunafahamishwa katika Qur-aan kuwa motoni kuna Daraja au Milango saba, na kila mlango iko sehemu iliyogawanywa.
“Na bila shaka Jahannamu ndipo pahali pao walipoahidiwa wote. Ina milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu walio tengewa”. [Suratu-Al-Hijr:43-44].
Daraja hizi za moto zimepewa majina kama tusomavyo katika Qur-aan:
1️⃣ 𝗝𝗔𝗛𝗔𝗡𝗡𝗔𝗠:
Katika Aayah nyingi jina hili limetumiwa, Kama jina la ujumla la maisha ya Motoni. Kama katika baadhi ya Aayah hizi Allaah Aliyetukuka Anasema:
“Hakika nyinyi na hao mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu” [Al-Anbiyaa: 98].
“…kisha Tutawahudhurisha pembezoni mwa Jahannam, wapige magoti (hapo)” [Maryam: 68].
2️⃣ 𝗟𝗔𝗛𝗔𝗕: Moto wenye muwako mkubwa kabisa.
“Atauingia Moto wenye mwako”. [Suratul-Masad: 3].
3️⃣ 𝗛𝗨𝗧𝗪𝗔𝗠𝗔𝗛: Moto wa kuvunja vunja-Moto uliowashwa kwa ukali.
“Hasha! Atavurumishwa katika Hutwamah”. [Suratul-Humazah: 4].
4️⃣ 𝗦𝗔’𝗜𝗬𝗥𝗔: Moto mkali wa kuunguza.
“Basi wapo miongoni mwao waliyoyaamini, na wapo walioyakataa. Na Jahannam yatosha kuwa ni (Sa’iyra) moto wa kuwateketeza”. [Suratun-Nisaa: 55].
5️⃣ 𝗦𝗔𝗤𝗔𝗥𝗔: Moto unaobabua.
“Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar”. [Suratul-Mudaththir: 26].
6️⃣ 𝗝𝗔𝗛𝗜𝗬𝗠: Moto mkali.
”Na Jahiym itadhihirishwa kwa wapotovu”. [Suratush-Shu’araa: 91].
Basi bila ya shaka mtaiona Jahiym”. [Suratut-Takaathur: 6].
7️⃣ 𝗛𝗔𝗔𝗪𝗜𝗬𝗔𝗛: Moto uokwao kwa ukali.
“Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Haawiyah”. [Suratul-Qaari’ah: 9].
Wakosaji wataingia katika aina hizi za Moto kulingana na makosa yao. Kwa ujumla aina yoyote ya moto ulioandaliwa kwa ajili ya makafiri na wakosefu hata ukiwa na daraja ya chini namna gani, Utakuwa ni mkali usio na mfano na usiovumilika hata kwa muda mfupi sana kama Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anavyotufahamisha:
“Hakika hiyo (Jahannaam) ni kituo kibayana mahali (pabaya kabisa) pa kukaa (hata kwa muda mfupi.” [Suratul-Furqaan: 66]
Kiufupi maisha ya motoni yatakuwa magumu sana kwa wakazi wake. Chakula chao kitakuwa cha moto wa kuunguza kila kitu tumboni, Mavazi yao yatakuwa ya moto, Kinywaji chao cha moto kitakachochemsha matumbo yao kama maji yachemkavyo kwenye sufuria ya shaba.
Tunamuomba Allaah (Subhanahu wa Ta’ala) Atukinge na adhabu ya moto, sisi na vizazi vyetu na Waislam wote kwa ujumla, Aamiyn.
Kwa faida zaidi
𝗙𝗢𝗟𝗟𝗢𝗪 𝗙𝗕 𝗣𝗔𝗚𝗘 Naupenda Uislam
Wabillaahi at-Tawfiyq..