Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

MALIPO YA BUSU BALAA!πŸ’‹12 Suzan alijikuta moyo wake unadunda kwa kasi hakujua akipokea

11th Sep, 2025 Views 48

simu ataongea nini, simu iliita mwisho ikakata lakini baada ya muda simu ilianza kuita tena, alibonyeza kitufe cha kupokea akapokea .
" Hallow. Suzani alipokea na kuongea kwa sauti ya chini
" Suzan...
" Abeee
" Umenipigia?
" Aaa.. nadhani simu ilijipiga.
" Sawa, unaendeleaje?
" Naendelea vizuri .
" Uko wapi?
" Nipo nyumbani, sijakuona upo sawa kweli?
" Hali yangu sio nzuri naumwa.
" Ndio maana sauti yako haipo sawa, unaumwa nini?
" Ni homa ya kawaida.
" Pole.
" Asante.
Baada ya hapo kulipiza kimnya kila mmoja alinyamaza kusikiliza mwenzie ataongea nini.
" Nataka kukuona. Victor alivunja ukimya
" Utakuja nyumbani?
" Hata wewe unaweza kuja kwangu.
" Sijui unakaa wapi.
" Upo tayari D aje kukuchukua?
" Sawa mwambie aje akifika mtaa wa pili dukani kwa mama Tunu anipigie simu .
" Sawa baada ya muda mchache atakuwa hapo.

Baada ya kukata simu suzan alitoka chumbani kwake akamfuata mama yake.
" Mama, veen amenipigia simu Kaniomba nikusindikize kwenye sherehe ya ndugu yake.
" Unapenda mambo ya usiku wewe. Sasa usiku nani atakurudisha nyumbani?
Nitawahi kurudi
" Mmmmm mambo ya sherehe nayajua kama ukiona amechelewa kurudi bora ulale hukohuko kwakina Veen sitaki kulia mimi hii dunia imeharibika.
Suzan alifurahi maana alipewa uhuru wa kuongea na Victor mpaka atakapotisheka na kama atachelewa ataenda kulala kwa Veen kesho ndio arudi kwao.

Alienda chumbani kwake alichukua kigauni chake kizuri ambacho alivaa anapendeza na kila mtu huwa anamsaidia kuwa kapendeza. Akisimama kwenye kioo cha dressing akachsna nywele zake vizuri na kuzibana kisha akavaa nguo yake . Uso wake aliupamba kwa vipodozi na midomo yake aliitaka lipstick nyekundu .
Akiwa anamalizia kujiandaa simu yake iliita D alikuwa anapiga.
" Madam nipo dukani kwa mama Tunu.
" Sawa nakuja sasa hivi.
Alivaa viatu vyake kisha akatoka . Alifika dukani kwa mama Tunu akaona gari imesimama pembeni alienda akapanda na safari ya kuelekea nyumbani kwa Victor ilianza.
Baada ya dakika 20 walifika kwenye mtaa uliokuwa umetulia na kulikuwa na mijengo ya maana , hakukuwa na fujo wala kelele hali ya hewa ilikuwa safi . Waliingia kwenye moja ya jumba moja la kifahari.
" Karibu madam suzan.dereva alimkaribisha baada ya kumfungulia na suzan akashuka.
" Asante. Suzan alishuka huku akishangaa mazingira na mandhari ya pale.
" Boss yupo ndani karibu.
Dereva alimuongoza mpaka sebleni.
Suzan aliendelea kushangaa vitu vya thamani vilivyokuwa vimepamba sebule.
" Yupo chumbani nifuate huku.
" Chumbani? Kwani hawezi kuja huku?
" Tangia ameanza kuibwa hajawahi kutoka amekuwa mtu wa chumbani.
Suzan alipandisha ngazi wakaelekea chumbani kwa Victor alifunguliwa mlango akaingia.
Alimkuta Victor akiwa amekaa kitandani huku akiangalia movie kwenye TV yake kubwa iliyokuwa kwenye ukikuta wa chumba.
" Mmmmh kweli kuna watu wanaishi bwana ona kile kitanda . Suzan alijisemea
" Karibu Suzan.
Suzan alisogea karibu na kitanda alimuangalia Victor usoni kweli alionekana hayupo sawa uso wake ulimpauka na midomo ilikuwa mikavu.
" Pole sana.
"Asante , kaa karibu yangu huwenda nitapata nafuu.
" Afadhali madam umekuja unaweza kumshawishi aweze kula maana ni siku ya pili hajatoa kitu tumboni.
" Hii sio sawa kwani mnampa chakula gani?
" Pizza, baga, juice...
" Hivyo sio vyakula vya kula mgonjwa jamani hebu kaniinyeshe jikobnimuandakie hata uji mwepesi .
" Sawa madam.
" Usijisumbue suzan sina hamu ya kula .
" Huwezi kupona bila kula.
Suzan alinyanyuka akatoka huku nyuma dereva na Victor walikonyezana kumbe Victor hakuwa anaumwa sasa nia yake ilikuwa ni nini kusingizia ni mgonjwa?

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MALIPO YA BUSU BALAA!πŸ’‹12 Suzan alijikuta moyo wake unadunda kwa kasi hakujua akipokea  >>> https://gonga94.com/semajambo/malipo-ya-busu-balaa-12-suzan-alijikuta-moyo-wake-unadunda-kwa-kasi-hakujua-akipokea

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - Mc Shabby Tatizo Moyo
Mc Shabby Tatizo Moyo
Mc Shabby Tatizo Moyo

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest