Baada ya Suzan kutoka sebuleni kuelekea alielekea jikoni ,Victor alivyobaki chumbani alinyanyuka na kwenda kusimama dirishani akiangalia nje kwa mbali kichwa chake kikiwaza.
βHuyu msichana kweli anaweza kuwa tofauti? Anaweza kuwa mke wangu?β
Alikumbuka siku za mwanzo, Suzan alipokuwa akijibu shaba nae na kumkataa kabisa Ilimlazimu kutumia nguvu nyingi kuwa karibu naye. Lakini sasa Suzan amekuwa mtu mpole na anamsindikiza bila hata kubishana
βKama huu huruma hii haitoki moyoni kwa Suzan basi mimi si Victor.
Akiwa bado kwenye mawazo hayo, mlango wa chumba uligongwa akarudi kitandani haraka na kuitikia .
" Ingia
Suzan alifungua mlango alirudi na kikombe cha uji mikononi, akasogea taratibu na kitanda.
"Hebu amka ujaribu huu uji. Victor alipouona ile uju akifanya anataka kutapika.
" Hapana siwezi.
" Hapana jaribu hata kidogo tu utapata nafuu huo uchovu unaotokana na kutokula .
" Asante suzan lakini siwezi.
Suzan alimwangalia kwa macho ya upole, hakusema chochote, alikaa kitandani kisha akachukua kikombe na kijiko, akichota uji kwa kijiji na kupuliza kwa mdomo wake kisha akapeleka mdomoni kwa Victor. Hili tukio lilimfanya Victor wapate msisimko na hisia flan hapo ndipo alipoamini suzan ndio mwanamke anaemfaa.
Alifungua mdomo wake akawa uji.
Baada ya kunywa vijiko kadhaa Victor alimwangalia Suzan.
" Asante suzan kidogo naona nafuu.
" Sawa hata hivyo kujitahidi umekubwa nusu ya kikombe huu mwingine utakunywa baadae.
Suzan alichukua kitambaa cha maji akamfutafuta vizuri mdomoni kisha akarudisha kikombe jikoni alafu akarudi chumbani na kukaa pembeni.
Victor aliweja mziki wa selin dion wa my love will go on. Walitulia na kusikiliza maneno ya ule muziki huku Victor hakumuangalia sana usoni. Alishindwa kujizuia alinyoosha mkono wake taratibu na kuushika mkono wa Suzan, Suzan aligeuka kumuangalia
"Unaonekana tofauti leo.
" Kivipi?
" Kwa kila kitu, umependeza pia unajali sana leo. Suzan alitabasamu alafu akasema
"Sijui labda ni kwa sababu naona unateseka. Sipendi kuona mtu anayejaliwa na Mungu anateseka hivi.
Suzan alisema kwa sauti ya pole.
Maneno ya suzan yaoigonga moyo wa Victor na kufanya nae aachiwe tabasamu.
"Una maanisha unanijali, na mimi ni mtu wa maana kwako?
"Kwa namna fulani, ndio. Sio rahisi usiku huu mimi kutoka nyumbani na kuwa hapa.
Victor alitabasamu, akamshika mkono Suzan.
"Suzanβ¦"
"Abee..."
"Ukiambiwa kuwa mgonjwa huyu sio mgonjwa wa kweli, utajisikiaje?
Suzan alimtazama kwa mshangao.
"Unamaanisha nini?
"Namaanisha mimi.....
Suzan alisimama kwa ghafla.
"Victor usiniambie huumwi ulikuwa unanichezea akili yangu.
Victor alisimama na kumsogelea kwa utulivu.
"Ndiyo, Suzan. Sikuwa mgonjwa. Nilihitaji tu kuona kama unanijali, sio kwa sababu nililazimika uwe karibu na mimi, si kwa sababu nina pesa, si kwa sababu nimekuzoea ila kwa sababu ya moyo wako.
Suzan alitazama chini, akiwa haamini kilichotokea.
"Kwa hiyo huu wote ulikuwa ni mtihani?"
Victor alishika mikono yake.
"Mtihani wa mwisho. Nataka mwanamke wa maisha yangu, Suzan. Nilipoanza na wewe sikujua kama utabadilika, lakini leo nakuona tofauti.
Suzan alinyamaza kisha akashusha pumzi ndefu.
Victor aliendelea, " kama huna jibu usijibu sasa hivi. Fikiria. Lakini nitakwambia ukweli mmoja, leo umeonyesha kile ambacho sikuwahi kukiona ndani yako.
Suzan alitabasamu kwa aibu.
"Victor⦠sijui kama ni mapenzi, au huruma, au vyote viwili. Lakini ukweli nimeuona tangia muda tu .
Victor alimsogelea taratibu, akaweka kiganja cha mkono wake kwenye shavu la Suzan.
"Ukweli gani uliouona?
" Kuwa unanipenda na unanihitaji haikuwa kunikomoa kama nilivyokuwa nadhani mwanzo lakini sijajua kama unanitania kwaajili ya kutimiza haja zako au unanipenda kwa muda na sina makazi ya milele kwenye chumba cha moyo wako?
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments