Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

MALIPO YA BUSU BALAA! πŸ’‹15

14th Sep, 2025 Views 37


Suzan alirudi nyumbani kwao akiwa hana furaha alirudi kanyongonyea kama mgonjwa mpaka mama yake aligundua kuwa hayupo sawa.
"Suzan mbona upo hivyo?
" Nipo sawa mama ni uchovu tu , naomba nikapumzike kidogo.
" Sawa.
Suzan alienda chumbani lakini alishindwa kabisa kutulia alikuwa akimtafuta Victor pamoja na D bado wakawa hawajapatikana.

Siku ya pili ilipofika, Suzan aliendelea kuwa kwenye wakati mgumu simu zilikuwa hazipatikani.
Alijaribu kupiga simu ya Victor tena na tena bado haikupatikana.
Aliamua kurudi kule nyumbani kwa Victor kwa matumaini huenda amerudi. Alipofika, alimkuta mlinzi yule yule alikuwa getini jana
" Karibu madam.
" Nimekuta Victor?
" Hapana jaribu kumtafuta kwenye simu.
" Sipati na sina taarifa za Victor, kwani hajarudi?
" Hajarudi.
Mlinzi alimtazama kwa dakika kadhaa kisha akasema .
" Lakini D yupo ndani.
" Nataka kuonana nae.
" Sawa.
Suzan aliingia ndani akamkuta D akifanya usafi kwenye gari.
" D , Victor yuko wapi?
" Boss aliondoka usiku wa manane alienda uwanja wa ndege, alipata Safari ya ghafla .
Suzan aliduwaa.
" Safari ya ghafla? Mbona hakuniambia na usiku kucha nilikuwa nae?
" Hata mimi nilishangaa maana ilikuwa ghafla sana . Suzan alishangaa akawa haelewi

D aliingia kwenye gari akatoa karatasi ndogo yenye ujumbe
akampatia Suzan.
" Aliniachia hii nikupe .
Ujumbe huo mdogo uliandikwa kwa mwandiko wa Victor:

*Suzan kabla ya yote naomba nitangukize samahani kwa kukuacha bila kuaga na kukueleza chochote ila mimi nimesafiri.
Safari hii haikuwa mipango yangu, lakini nimeilazimika. Nimepelekwa mahali ambapo maisha yangu yanahitaji utulivu .
Kama utanisubiri, nitashukuru. Kama hutoweza nitakuelewa pia.
Victor*

Suzan alimaliza kusoma, akaangalia juu angani. Machozi yakaanza kumlengalenga.
"Victor kwanini kila kitu kwako ni ghafla? Kwanini maisha yako ni kama fumbo lisiloweza kutafsiriwa? Nataka kukuelewa, lakini kila hatua yako inanifanya nipoteze tumaini.
" Usijali atarudi kwajili yako.
" Sawa D acha niondoke. Suzan aliondoka akiwa mnyonge mpaka D akamuona huruma.
Suzan alikuwa kwenye wakati mgumu sana sababu alikuwa kashsmzoea sana Victor na alijua wanaenda kuanza safari yao yenye mapenzi ya furaha lakini ameishiwa kuachwa na huzuni, taratibu alianza kupoteza matumaini ya kuonana tena na Victor hata chuo walianza kumuongelea kuwa ameachwa sasa karudi kwenye ndoto.
" Hawa masponsa sio watu wa maana kabisa na ukizingatia kila siku warembo wapya wanazaliwa jamaa kashajipatia mtoto mdogo anakula zake maisha.
Maneno ya watu yakizidi kumuuliza suzan .
Siku moja aliamua kwenda kukaa mwenyewe kwenye limbwata akitafakari mambo yake , akiwa mbali kimawazo alishitukia kumuona James amekaa pembeni yake , James anamkabidhi chupa ya soda ya fanta.
" Asante.
" Vipi mbona imekaa kwa huzuni?
" Mbona nipo kawaida.
" Najua haupo sawa , ni kweli jamaa kakuacha?
Suzan hakutaka kujionesha mnyonge alijikaza na kucheka.
" Kumbe hata wewe una amini hilo ?
" Ndio naamini.
" James yule mtu hakuwa mwanaume wangu ila alikuwa ni mwanaume ambae alikuwa akilipita kisasi chake kwangu.
" Kivipi?
Suzan alimuelezea James kila kitu kuhusu Victor.
" Daaah kwahiyo jamaa alikuwa anacheza na akili yako?
" Ndio, naona sasa moyo wake uko na amani ndio maana ameamua kutulia zake.
" Kwanini hukuniam ila hilo mapema?
" Ningeanzia wapi ikiwa hukutana kujua ukweli ulikuwa ukinishutumu tu.
" Pole .
" Nimeshapoa.

Kila ilipofika usiku suzan alikuwa chumbani kwake akiangalia picha walizokuwa wanapiga wakiwa na Victor zilimkumbusha mambo mengi sana mpaka akajikuta machozi yanatoka.
" Sio kweli huyu mwanaume alikuwa hanipendi hata kidogo , kwanza mwanaume gani hakuwa na hisia hata za kutaka kuujua mwili wangu zaidi yeye alinichezea kama mdoli na kumuacha tu hata siku ile nimelala pembe yake mpaka asubuhi lakini alishindwa kabisa kufanya chochote. Hii sio kawaida Victor hakuwa na chembe ya upendo kwangu alikuwa yupo kwaajili ya kisasi na kuniumiza kihisia na sasa amefanikiwa.
Nakuchukia Victor, tabasamu lako lilinifanya niwe kipofu na maneno yako yalinipumbaza kumbe ulikuwa muongo moyo wako ilibeba chuki ya kisasi.
Palepale suzan aliamua kufuta kila kitu kwenye simu yake ambacho kilimkumbusha Victor. Hata baadhi ya vitu alivyomnunulia alivikusanya na kugawa hakutaka kubakisha alama ya Victor alipania kufuta kila kitu ili aanze upya maisha yake.

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MALIPO YA BUSU BALAA! πŸ’‹15  >>> https://gonga94.com/semajambo/malipo-ya-busu-balaa-15

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest