Kadri siku zilivyokuwa zinasonga mbele Suzan alianza kuzoea akaendelea na maisha yake . Taratibu alianza kumtoa Victor akilini kwake japokuwa haikuwa rahisi.
Aliamua kuachana kabisa na swala la mapenzi na kuamua kubaki mwenyewe.
Hakuwa na haraka tena na wala hakuruhusu mtu yeyote kuvunja moyo wake. Lakini James hakuacha kumuonyesha kuwa bado yupo karibu pia alionesha kuwa alitaka warudishe penzi lao .
" Suzan naomba unipe nafasi niwe mafriji wako .
" Hapana James sitaki tena mapenzi , sitaki kuumizwa wala kuvunjwa moyo niache nisimame mwenyewe.
" Sawa lakini bado sijakata tamaa , acha nikupe muda itafakari zaidi.
" Sidhani kama moyo wangu utaweza.
" Nakupa muda .
Hatimae ikipita miezi sita na suzan akawa amemaliza chuo akawa anajichanganya mtaani kutafuta kazi.
Siku moja alipokuwa anatoka kwenye ofisi moja simu yake iliita alipoangalia ilikuwa ni namba mpya . Alipokea haraka akihisi huenda anapigiwa simu baada ya kufanya usajili kwenye baadhi ya makampuni.
" Hallow...
" Hallow suzan.
Baada ya kusikia hiyo sauti moyo wake ulianza kudunda kwa nguvu. Alishindwa kuendelea kuongea alitoa simu yake sikioni aliangalia screen na kuzisoma zile namba kwa makini aligundua kuwa ni yeye Victor.
Alikata simu na kuondoka taratibu huku akijiuliza.
" Atakuwa amerudi? Kwanini ananipiga baada ya kukaa kimnya kwa muda mrefu? Anataka kunichezea tena michezo yake ya kijinga? Safari hii siwezi kumpa nafasi hata kidogo kwanza sitaki kuonana nae.
Dakika chache baadaye, meseji iliingia.
"Suzan, naomba unisamehe. Kuna mambo unahitaji kujua. Tafadhali, kama utakuwa tayari naomba kesho tuonane nikueleze kila kitu.
Victor
Suzan alikaa kimya kwa muda mrefu huku akiangalia na kusoma hiyo messege mara mbilimbili.
" Hapana suzan usikubali huu ni mtego mwingine ameona sijaterereka anataka kuja na njia nyingine.
Suzan akafuta meseji ile, bila hata kujibu. Hakutaka tena kuonana na Victor.
Siku iliyofuata jioni, Suzan alikuwa anakunywa juisi kwenye mgahawa mdogo, Akiwa pale, gari jeupe lilisimama Mlango ukafunguliwa na Victor akatoka.
Alionekana mwili wake umepungua, uso wake ulichoka, lakini bado alikuwa na tabasamu usoni mwake baada ya kumuona suzan. Wakati huo suzan aliona kama katiba shetani.
mapigo ya moyo wa Suzan yaliongezeka, lakini alipokumbuka kilichitokea hapo nyuma alitulia kama hakuona .
Victor alisogea hadi alipo.
" Mambo.
Suzan hakuitikia
"Naomba dakika tano tu tuzungumze. alisema Victor kwa sauti ya upole.
Suzan alimuangalia kisha akavuta pumzi.
"Victor si unajua muda ni gharama ?
"Najua, na sipo hapa kujitetea. Nipo hapa kwa sababu nahitaji kukuambia ukweli wote. Niliondoka kwa sababu maisha yangu yalikuwa hatarini."
Suzan alicheka kwa kejeli. "Hatarini? Hii sinema mbona kama inataka kuendelea kweli.
Ni kweli maisha yangu na familia yangu yalikuwa hatarini kuna watu waliokuwa wakinifuatilia na kutaka kuniuwa.
" Nani alitaka kukuuwa wewe mtu wa drama?
"familia ya mpenzi wangu wa zamani aliyefariki kwenye ajali ya gari tukiwa wote. Walinilaumu kwa kifo chake."
Aliongea Victor halafu akaweka bahasha mezani.
" Fungua hiyo bahasha uangalie.
Suzan alichukua bahasha taratibu, akafungua kulikuwa na picha pamoja na makaratasi.
Alichukua picha moja moja akawa anaiangalia
kulikuwa na picha za gari lililoharibika vibaya, kwa ajali . Picha ya maiti iliyokuwa umefunikwa pembeni ya barabara na picha nyingine ilikuwa niya Victor akiwa ametumia vibaya anavuja damu. Pia kulikuwa na ujumbe wa vitisho, na hata jalada la kesi.
" Hii imetokea lini?
" Miaka 3 iliyopita. Siku ile usiku nilipokuacha pale nyumbani nilikuwa nimechanganyikiwa mama yangu mzazi alivamiwa na kupigwa risasi hali yake ilikuwa mbaya sana ndio maana nikiondoa bila kitu chochote kwaajili ya kumuwahi.
Usiku uleule tulipata doctor , tukakodisha ndege na kuondoka tukampeleka Afrika kusini.
" Ninaamini vipi kama mama yako anaumwa au ndio giacyako mpya ya kutaka kuniumiza kwa mara nyingine?
"Ninajua siwezi kuomba urudi maishani mwangu, lakini nilihitaji uujue ukweli huu. Na leo, narudi mahakamani kwa ajili ya kesi ya mwisho. Kama nitashinda, nitaondoka nchi hii kwa muda. Nilikuja kukuaga vizuri kwa mara ya mwisho.
Victor hakusubiri jibu alisimama na kuondoka.
Suzan alibaki amekaa akishika bahasha alimsundikiza kwa macho mtu aliyemvunja vunja moyo lakini pia aliyemfundisha maana ya kusamehe.
" Inamaana anataka kuondoka hawezi tena kuwa na mimi? Suzan alijiuliza moyo wake ulikuwa bado anatamani sana kumpa nafasi nyingine Victor.
Victor alienda kupanda kwenye gari akiwa mnyonge.
" Vipi amekuelewa?
" Hajasema chochote inaonekana hawezi kumsamehe.
Aliongea Victor huku chizi likimtoka lakini alifuta haraka .
.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments