Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

MALIPO YA BUSU BALAA!πŸ’‹* *__________________________________* *SEHEMU YA KUMI NA MOJA*

10th Sep, 2025 Views 21



Suzan alijikaza kitandani akawa anakumbuka matukio ya hotelini, alikumbuka jinsi jinsi Victor alivyomnyanyua na alikuwa akisikia karadhi yake mazuri, akamweka kitandani na jinsi alivyokuwa anaogopa akajikuta anacheka huku akiona aibu.
" Kweli nimekuta futa na nimeliona na haya yote ni malipo ya nusu la hadharani aiseeeee nimekoma.

Kwa upande wa Victor alionekana kuwa na wasiwasi sana alihisi kuna kitu hakipo sawa kwa upande wa suzan alijitahidi sana kupiga simu lakini haikupatikana.

Kesho yake Victor hakwenda kumchukua suzan alipanda pikipiki mpaka chuo .
Wakati anaelekea darasani alikutana na James .
" Mambo
" Safi.
" Mbona jana hukujubu messege zangu na inaonyesha ulisoma?
" Sina cha kujibu James.
" Jana ulienda wapi na yule jamaa?
" Alinieleza nyumbani.
" Daaah unamaana mpaka nyumbani kwenu wanamjua?
" Sijamaanisha hivyo.
" Suzy unapendana na yule jamaa? Suzan alikuwa kimnya hakuongea
"Sasa kwanini haukusema mapema ukaniacha nimejipa matumaini ya kuwa na wewe? Nikakupa moyo wangu nikiwa naamini ipo siku tutafika mbali kumbe unaniona bonge la fala sababu sina kitu si ndio?
" James huna unachojua na sijui nikwambie nini ili unielewe.
" Sawa bwana acha mimi niache mashindano siwezi kugombania na mtu mwenye pesa.
Suzan aliumia sana lakini hakuongea chochote maana aliamini James hawezi kumuelewa.
" Nakutakiwa kila la heri kwenye mahusiano yako mapya. Alisema James kisha akaondoka.
" Kwahiyo ndio unaniacha hivyo?
" Ndio suzan moyo wangu umekinahi, siwezi kuwa na wewe tena wewe ni malaya Suzan huna tofauti na wanawake wengine wa hapa chuoni wanaofanya miili yao mitaji.
" James tafadhali usinitukane.
" Lazima nikwambie ukweli.
" Ukweli upo unaokuwa wewe? Huna unachojua James yule mwanaume sio mwanaume wangu.
" Sitaki kuendelea kudanganywa na kuanzia sasa its over.
" Poa.
Kuanzia siku hiyo Suzan na James waliachana.

Jioni kama kawaida Victor walifika chuo kwenda kumchukua Suzan.
" Kwanini jana ulizima simu ?
" Sikuwa nataka usumbufu.
" Kwahiyo ulikuwa unataka kuichanganya akili yangu.
" Mimi ndio nachanganyikiwa zaidi yako , unanisababishia matatizo kila kona. Hakika najutia sana ile siku ya busu.

Siku zilizidi kwenda na Victor alizidi kumganda Suzan ilifikia hatua alikuwa akitoa amri ya kutaka kuonana hata usiku maana kuna muda Victor alikuwa Bize siku nzima hivyo alimwambia dereva afuate chuo au alituma pesa kwa Suzan kwaajili ya usafiri.
Siku moja majira ya saa mbili usiku Victor alipiga simu.
" Nipo nje kwenu naomba utoke.
" Siwezi kutoka wewe ondoka tu.
" Suzan unanijua akili yangu haiwezi kuwa sawa bila kukuona na siwezi kulala bila busu lako.
" Kama hilo litasababisha ufe bora uende ukate ili uache kunisumbua.
" Huko ndio jibu lako kweli?
" Ndio unataka je kwani?
" Sawa dakika mbili nitakuwa hapo ndani kwenu.
Victor alikata simu na suzan aliweka simu pembeni akaendelea na kazi nyingine.
" Yani huyu anataka kunifanya toy kila siku kunitishia.
Baada ya sekunde walisikia geti linagongwa. Suzan alishituka .
" Mmmh huyo amegonga saizi ni nani?
" Suzy nenda kafungue geti.
Ilikuwa ni sauti ya mama yake na Suzy alinyanyuka haraka akaenda kufungua geti.
Alibaki mdomo wazi alipokutana na sura ya Victor.
" Khaaaaaa wewe unataka nini?
" Hakutaka wewe suzan.
Suzan aliangalia nyuma kama kuna mtu anawaona kisha akatoka na kufunga geti na kumvutia Victor pembeni.
" Ulifikiri natania?
" Wewe kweli ni kichaa ujue baba na mama wapo ndani?
" Ndio nilitaka kuonana nao.
" Alafu...
" Niwaambie nakuhitaji.
" Sikiliza naomba uende tutaonana kesho.
" Sawa lakini nusu kwanza.
" Khaaaa kwani wewe umekuwa na busu?
" Tangia siku ya kwanza ulinitega na kile busu.
Suzan aliamua amalize mzozo alintandika busu kisha akarudi ndani.

Mara kwa mara suzan na Victor walionekana kuwa pamoja watu wengi walijua suzan anatokna kijana tajiri na mtu maarufu, hata mtaani maneno yalianza kusambaa maana Victor hakuangalia muda wa kufika mtaani na mara kwa mara walionekana wakiwa wote kuna wakati walitoka pamoja wakaenda hotelini walikaa na Victor alikuwa alimbusu na kuushika mwili wake baada ya hapo alimuacha aondoke hakutaka kumlazimisha wafanye kitu ambacho hakuwa tayari.
Taratibu suzan alianza kumzomea Victor .
Ikipita siku bila kumuona alijikuta ana miss

Zikipita kama siku kadhaa hawajaonana suzan alikuwa hana amani kwenye moyo wake alichukua simu akaandika messege.
" Upo salama ? Aliandika huo ujumbe ilibakia kugusa kitufe cha tuma lakini alijikuta anasita.
Alifuta ile messege aliyoandika akaweka simu pembeni.
" Hapana siwezi kutulia . Alichukua tena simu yake na kupiga namba ya Victor. Iliita mara mbili kisha akakata, muda huo huo simu yake iliita Victor alikuwa anapiga.

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MALIPO YA BUSU BALAA!πŸ’‹* *__________________________________* *SEHEMU YA KUMI NA MOJA*  >>> https://gonga94.com/semajambo/malipo-ya-busu-balaa-__________________________________-sehemu-ya-kumi-na-moja

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest