❤️ MAPENZI SI MANENO TU, NI MOYO ❤️
Mapenzi si "nakupenda" tu kila siku.
Mapenzi ni kukaa kimya lakini moyo wako ukimpigania mtu ambaye hata hajui unajitoa kiasi gani kwa ajili yake.
Mapenzi ni kuvumilia tabia, hali, na makosa ya mtu wako kwa sababu unajua hakuna aliye mkamilifu, na bado unamchagua yeye kila siku.
Mapenzi ya kweli hayaangalii urembo wala hela, yanaangalia moyo.
Ni pale unapoona mtu hana kitu, lakini roho yako inatulia naye.
Ni pale unapoona wengine wa kuvutia, lakini bado macho yako yamefungwa kwa mmoja tu.
Ni pale unapoambiwa aachane na wewe, lakini anakataa kwa sababu amekuona kama maisha yake.
💬 Mapenzi ya kweli yanaumiza, yanajaribu, lakini mwisho wake ni ushindi.
Ni safari ya wawili waliopoa, waliovumilia, waliopigania… hadi wakashinda.
Siku moja utampata mtu ambaye hata ukiwa kimya, moyo wako utasikika kwake. Na hilo ni penzi, sio mchezo..