, ikiwa ni upanuzi mkubwa wa marufuku ya usafiri iliyotangazwa na utawala wa Trump mapema mwezi huu, kulingana na nyaraka ya Wizara ya Mambo ya Nje iliyopitiwa na gazeti la The Washington Post.
Miongoni mwa nchi mpya kwenye orodha yawezaokumbwa na marufuku ya viza au vikwazo vingine ni mataifa 25 ya Afrika, ikiwa ni pamoja na washirika muhimu wa Marekani kama vile Misri na Djibouti, pamoja na nchi za Karibiani, Asia ya Kati na visiwa kadhaa vya Pasifiki.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje alisema taasisi hiyo haitatoa maoni juu ya mashauriano ya ndani au mawasiliano. Ikulu ya White House haikujibu mara moja ombi la kutoa maoni.
Hatua hiyo ingeashiria kuongezeka kwa hatua za ukali zinazochukuliwa na utawala wa Trump dhidi ya wahamiaji.
Barua hiyo, iliyosainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio na kutumwa Jumamosi kwa wanadiplomasia wa Marekani wanaofanya kazi na nchi hizo, ilisema kuwa serikali za mataifa yaliyotajwa zinapewa siku 60 kutimiza viwango vipya vilivyowekwa na Wizara hiyo. Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha mpango wa awali wa kuchukua hatua ilikuwa ni saa 2:00 asubuhi siku ya Jumatano.
Nyaraka hiyo ilitaja sababu mbalimbali ambazo, kwa mujibu wa utawala huo, zinahusiana na mapungufu ya nchi hizo. Baadhi ya nchi hazina mamlaka kuu ya serikali iliyo na uwezo wa kutoa nyaraka za utambulisho au nyaraka nyingine za kiraia zilizo sahihi, au zinakabiliwa na “udanganyifu mkubwa serikalini.” Nyingine zina idadi kubwa ya raia wanaoishi Marekani kwa kukiuka muda wa viza zao, barua hiyo ilisema.
Haikufahamika mara moja ni lini vikwazo hivyo vya usafiri vinaweza kuanza kutekelezwa iwapo masharti hayatatimizwa.
Nchi zinazotajwa katika nyaraka hiyo ni, Angola, Antigua, Barbuda, Benin, Bhutan, Burkina Faso, Cape Verde, Cambodia, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Djibouti, Dominica, Ethiopia, Misri, Gabon, Gambia, Ghana, Ivory Coast (Côte d’Ivoire), Kyrgyzstan, Liberia, Malawi, Mauritania, Niger, Nigeria, Saint Kitts na Nevis, Saint Lucia, Sao Tome na Principe, Senegal, Sudan Kusini, Syria, Tanzania, Tonga, Tuvalu, Uganda, Vanuatu, Zambia na Zimbabwe.
#KitengeUpdates.