Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

MOYO WANGU KWA MSELA πŸ«€ 01 Mimi naitwa Rena,nimelelewa na babangu mzazi pamoja na mama wa kambo

17th Sep, 2025 Views 19

lakini alikuwa ananipenda huyo maana yeye hakubahatika kuwa na mtoto hali iliyopelekea babangu kutafuta mwanamke mwingine kuzaa nae ambaye ni mamangu mzazi lakini mamangu hakuwahi nilea ni kama walimtumia tu awazalie wakamlipa kwa kumjengea nyumba kubwa tu na ata sikuruhusiwaga kwenda kwa mama kabisa niliwahi kwenda mara moja tu wakati nipo darasa la kwanza sikukanyaga tena lakini mama alikuwa anakuja kuniona angalau kwa mwaka mara moja na alikuwa anapokelewa vizuri tu kwakweli,na akiondoka pia walikuwa wanamfungashia zawad mbalimbali arudi nazo kwake akawa kama ndugu kwao

Mamangu pia alikuwa na watoto wengine wawili lakini sikuwahi kujuana nao kivile nawaona ona tu wakija na mama , walikuwa wakike na wakiume.....maisha yangu yaliendelea kwa babangu huku nikiwasiliana na mama angu mzazi maana nilikuwa nimeruhusiwa😜mamangu wa kambo alikuwa ananidekeza hatari kwanza watu walikuwa hawajui kuwa hajanizaa yeye,miaka ilisonga mwisho nilimaliza kidato cha nne mwenyewe nilirud nyumbani maana nilikuwa nasoma boarding

Basi nilipanda basi kurudi nyumbani nilifika jioni nikawa namsubiri mama anifate nilingoja mpaka kigiza kikaanza ingia ndo akafika wow mwanangu apo nimenuna hatarπŸ˜’jamani usimnunie mama basi eti mziwanda wanguπŸ«‚sitak mimi nimekaa apa njaa inaniuma😞sorry my dear ni foleni tu mwanangu usikasirike bas akanichukua tukarudi nyumbani apo nimenuna hatari ananiongelesha sitakπŸ™ˆ tulifika nyumbani tukamkuta baba nilimkumbatiaje utasema sijamuona siku kibao wakati imepita kama wiki 3 tu walikuja shule kwenye graduation nmekumiss sana binti angu kwanza pole na hongera kwa mitihani asante daddy ila tu mama kaniudhi jamani mimi kanigandisha stendi njaa inauma bado unayo tu jamani nawee ndio kwanza nile maana nitazimia kwa njaa nikaenda kupakua chakula nile baba akanambia yaani mwanangu nna habar njema apa nimeona hii likizo ukisubiri matokeo uende ukamsalimie mamako(mzazi) pamoja na ndugu wengine maana ata uwajui kweli daddy? kabisa lini? siku yoyote utayopenda sawa basi acha nikaekae ata wiki kwanza nipumzike sawa,nilikaa baada ya wiki mama mzaz alikuja kunifata twende uko kwake sasa nikawajue na ndugu wengine😜 niliandaa vitu vyangu vizuri na baba akanipa mtonyo niweze kununua chochote pia akanambia ntakaa mwezi ila nikiona vip nirud sawa daddy mama alikuja niliwaaga vzur mama(mzaz) akanambia yaani watafurah nyumban bibi ako,na ndugu wengine ata Mimi natamani sana niwajue usijal mwanangu ndo tunaenda tulisafiri tukawa tumefika mida ya saa10 jion moro tukitokea dar mama akakodi boda mbili kwenda uko nyumban ila hakukuwa mbali tukawa tumefika ,yaani kufika tu apo nyumbani kwenyewe tukakuta ugomvi msichana na mvulana makamo yangu wanazichapaπŸ‘ŠπŸ»πŸ˜€

niliishia kuganda mama buana akaenda kuwapiga makofi wajing nyiee kila siku makelele tu wakaachiana uyo mvulana akaondoka uku analalamika dogo usinichezee yaani nitakuzimisha msichana nae abaki nyuma anamjibu mama akamwambia nawe kelele msichana mzima hujiheshimu nae akaondoka ndani kanuna balaa kulikuwa na wengine wanashangilia et walikuwa wasichana wawili mvulana mmoja🀨wawili ndo niliwajua ni wadogo zangu ambaye ni msichana na mvulana lakini wale walokuwa wanapigana na msichana mwingine sikuwajua kabisa mama aliwacharua kweli yaan mnashangilia ugomv yaan mnapenda mikelele nyumba hii kutwa vimbwanga( mieee nikajiuliza moyoni kutwa vimbwanga??πŸ™„) basi kale kavulana ambae ni mdogo wangu alikuja nikimbilia kunipokea dada uyo karibu asante mdogo wangu akanisaidia bag wale wengine ata hawana mudaπŸ€”nikakaribia ndani mama akanipeleka chumban kwake utakuwa unalala umu na mimi sawa mama akamuulizia yule mdogo wangu anaitwa amani bibi ako yuko wapi kafate bamia shamba sawa upumzike ushafika nyumban asante mama ngoja mimi nitafute cha kupika nilimpigia mama mlezi kumwambia nimeshafika sawa mwanangu tutakua tunawasiliana sawa sawa basi kiusingizi kikanipitia😴 nkaja amshwa na mama ukaoge uje kula usiku ushaingia na uje umsalimie bibi ako sawa mama nilitoka kwenda kumsalimia bibi nikaoga tukaenda kula baada ya kula mama akaanza nitambulisha mwanangu uyu najua utakuwa unamkumbuka ni bibi ako ndio mama na hawa wadogo zako unawajua amani na asha usiowajua kabisa ni hawa wawili pamoja na yule mvulana ambaye tuliwakuta wanapigana na uyu (akamuonyesha kidole msichana mmoja) uyu na alokuwa wanapigana nae ni mapacha uyu kulwa yule mvulana ni doto(nikasema mmmh sa mbona yule mvulana alikuwa anamuita kulwa wake dogoπŸ˜„)

Hawa ni watoto wa anko wako pamoja na huyu mwingine nae anaitwa Zahara nae ni mtoto wa anko wako ana watoto watatu anko wako na aunt Yako wamesafiri kidogo wakirud nao utawaona sawa mama nyiee uyu ni ndugu yenu mwanangu kabisa Nadhani mnamkumbuka Na mmemsikia sana sawa tumemuona ila naomba uwe makini na yule doto akili zake sio nzuri nami nikajisemea nahis anavuta bangi maana smuelewi yupo kama mhuni ivi kwanza ana virastaπŸ˜‘basi tulienda kulala na mama wale wengine wakalala chumba kingine mamangu alikuwa hana mume wakat uo waliachana asubuhi niliamka mama akanambia nimtume asha au aman akaninunulie mswaki nilitoka chumbani nikakuta wenzangu kibarazani niliwasalimia mambo zenu? poa tu hawakuwa na story nying na mimi wala niniπŸ˜‚

Wakaendelea kupiga story zao nikamtuma amani mswak na dawa maana ndo niliona ana kaukaribu na mimi bibi nae akaamka tukamsalimia akaniuliza umeamkaje? kulwa alidakia wengine hatuulizwi tumeamkaje jamani mbona kazi..! ebu kelele wewee muone macho yake kama mchinaπŸ˜‘mropokaji ropokaji tu bibi alimcharua wenzie asha na Zahara wacha wacheke mimi nilijikaza sikucheka🀭kwanza badala mfanye usafi mmekaa vikao mnapiga story sasa bibi ata ujatuuliza tumeamkaje labda tunaumwa jeee huo usafi tutaufanyaje wee mtoto wewe endelea kuleta mdomo tu bibi uyu mngemrudisha mkoleni hajakoma ujeuri asha alidakia nae nawewe kelele si nakushauri tu jamani ungeanza kujishauri wewe kuchana nywele zako hizo zilizo timu timu kama umetoka kufufuka nilishindwa kujizuia jamani tulicheka wote mpaka basi🀣🀣🀣🀣

Amani akawa ameniletea mswaki na dawa akanambia dada basi nitoe mia mbili nikampa mia tano ilobak chenji maana nilimpa elfu mbili aninunulie mswak mia5 na dawa elfu 1 basi kina kulwa wapo watu na dada zao maboss ila na nyieee dada achana nao hawa nilienda zangu kuoga nawaza hii nyumba jamani mbona vituko sasa mimi sijazoea makelele atiii😟 nilivyotoka kuoga nikamwambia mama umu Kuna vtuko akasema ujacheka bado na Kuna maudhi sana tena wakikukera usiwachekee ila tunaishi Kwa upendo tu usijali,ila doto tu ndo uwe nae makini Hawa wengine wasikushughulishe ni wanajichetua tu

ITAENDELEAAA

FULL STORY
Whatsapp 0657171961
KWETU Morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MOYO WANGU KWA MSELA πŸ«€ 01 Mimi naitwa Rena,nimelelewa na babangu mzazi pamoja na mama wa kambo  >>> https://gonga94.com/semajambo/moyo-wangu-kwa-msela-01-mimi-naitwa-rena-nimelelewa-na-babangu-mzazi-pamoja-na-mama-wa-kambo

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - Mc Shabby Tatizo Moyo
Mc Shabby Tatizo Moyo
Mc Shabby Tatizo Moyo

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest