Niliwaza haraka haraka nikasema huenda hizi ni njia Mungu anatufungulia za kutupatia ada sisi yatima wakeπ₯Ήπ₯Ή..
Nilimwambia Hemed it's okay kwa hiko chakula kitakuwa cha watu wangapi???
Akasema ni chake yeye tu atakuwa anapitia anaenda kula nyumbani then anarudisha vyombo asubuhiπππ...
Sawa basi nimekuelewa... na chakula kitakuwa cha aina gani maana hicho cha mtu mmoja si itatakiwa niwe napika chakula unachojisikia kulaπ..
Hemed aliniambia ni kweli but mimi nitakutajia tu vyakula ninavovipenda then nitakuwa nakupa pesa ya mahemez ya week nzima then wewe utakuwa unapangilia kipi cha kupika..
Okay sawa basi Hemed naomba nikutakie usiku mwemaππtuliagana hivo huku pembeni kadogo kangu kakawa kanacheka cheka tuπ³π³
Unacheka nini wewe badala ujisomeeπ³π³ hahahaa dada mbona huyo kaka alikuwa anakuongelesha hivoπππ ni kama vile anakupenda π
Hivi huyu ni chizi eehπ³π anawaza upuuzi ila simlaumu maana ndo yuko kwenye ule umri wa foolish ageπππnilimpiga kakibao kadogo kichwani nikamwambia soma huko uache upuuziπ
Tuliendelea kusoma mpaka saa sita za usiku tukaingia kulalaπ₯°π₯°π₯°siku iliyofuata kama kawaida tuliamka mapema tukaenda sokoni tukahemea makolo kolo ya mgahawani then tukaenda kuandaa chakula
Tulipika chai na vitafunwa tukapeleka kule site kwa Boss Hemed yeye hakuwepo walikuwepo mafundi tuππ
Siku hiyo nimefika pale mambo yalikuwa tofauti na janaπ³π³π³ yani siku hiyo mafundi walinionesha heshima fulani hivi mmmhhh nikabaki nashangaa..
Jana tu walikuwa wananitania tania wengine mpaka wananiita mama watoto wengine wakaanza kuniomba namba ila siku hiyo nikaanza kuitwa miss mara madame hahaaa haya ni maajabuπ
Niliwapa chai then nikakaa pembeni kusubilia vyombo wakati nasubilia vyombo hee mara nikaona gari ya Hemed πππ alafu akaja kupark pale nilipokaaa nyieeeπ
Alitelemka kwenye gari akanipa hi alikuwa ananiangalia kuliko kawaida ila sikumzingatiaππ alipoona nampotezea akasimama pembeni akawa ananiangalia kwa macho ya kuibiaππ
Mimi wala sikuwa na time naye hahahaaa nilikuwa bize tu nawaza majukumu mimi ndo mama mimi ndo baba kwangu na kwa mdogo wangu sina nafasi ya kuwaza ujinga hata kidogoππ..
Nilikuwa nawaza mbali sana mpaka akili ikawa haiko tena pale siteπ nilikuja shituka kwa badae mafundi wanakonyezana tu mmhhh nini kinaendelea
Si ndo ikabidi nigeuke kumwangalia Hemed nikakuta mkaka wa watu kaganda jicho liko kwangu...
Kwa vile mafundi walishamaliza kula nilikwenda kuchukua vyombo vyangu niondoke Hemed akaniita akaniuliza kama chai ipo nikamwambia niliyoleta pale site imeisha ila ofisini ipoo..
Aliomba twende wote ili akanywe chaiπππnikamwambia sawa twende..
Alifungua mlango wa gari nipande nikamwambia siyo mbali tutembee tu..
Please Bella panda kwenye gari please ππ ilibidi nikubali kupanda tukaondoka kuelekea pale mgawahani kwetu..
Nilikwenda nikamuwekea chai chapati na maharage akaanza kunywaπ₯°π₯° alipomaliza akaniambia chakula ni kitamu sana naomba namimi uwe unaniwekea chai nitakuwa nakuja kunywa hapaπ
Poppy kwa pembeni ni kukenua tuπππnilimwambia sawa Hemed hakuna shida..
Aliomba Bill nikampatia yake na mafundi akanilipa... baada ya hapo kuna kikaratasi alinipatia kilikuwa kimeandikwa vile vyakula anavokula yeye..
Alinipatia na hiyo pesa ya mahemezi ya week nzima na ya kwangu ya upishi nyieeeeee mbona ananipa pesa zote hiziππ
poppy alinikonyeza dada chukua mbona unakuwa mshamba hivo weweπ€
Nilichukua zile pesa baada ya hapo Hemed aliondokaπ jioni ilipofika nilikwenda kuhemeaππ
Siku hiyo nilipanga kumpikia samaki na ndizi pamoja na juice ya embe na passion πππ...
Niliingia jikoni mtoto wa kitanga mapishi nayajua si kitotoπππnilikaangizaaaaaππ
Hiyo juice nikaisaga nikaitia kwa fridge ipoeeππΌππΌππΌ usiku mida ya saa mbili ndo nikapigiwa simu na Boss Hemed anaomba nimwelekeze home aje kuchukua chakulaπ
Mmmmh nyumbani tenaaaa
Nini kitafuata???.. itaendelea..
Full 2000
Whatsapp 0657171961
KWETU Morogoro.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments