Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Pyar Ho Jane Dushman

MTEULE (The chosen one) 01

1st Aug, 2025 Views 26

Story………………...
Mtunzi……………..Simulizi Za Zooper
WhatsApp……....0613083801
Umri………………...18+

Mwanzo.......
Macho ya watu wote yalikuwa kwenye msafara wa familia ya kifalme, magari yenye hadhi yaliitawala barabara na idadi ya watu ilikuwa kubwa iliyokuwa ikishuhudia msafara huo.
Wengi walijipanga barabarani kutazama huku kila mtu akiongea lake, wapo waliousifu uongozi wa mfalme wao na wapo waliouponda uongozi wa mfalme wao, baadhi pia walilaumu kwa magari yao kuwekwa kando mpaka pale msafara wa familia ya kufalme upite kitu walichoona ni upotevu wa mda tu.

Msafara ulitembea taratibu na kwenye gari moja wapo alikuwa kapanda mwana wa mfalme, macho yake yaliangaza nje kuangalia watu waliokuwa wamejipanga barabarani wakiutazama msafara na alipotaka kuyageuza aliweza kumuona binti mmoja akiwa kasimama pembeni kabisa akiutazama msafara.
Macho yake hayakukoma kwa binti huyo na ghafra hisia za ajabu zilimshika zilizofanya moyo wake uanze kwenda mbio na kuongea kwa sauti.
"Simamisha gari!"
"Prince!?"
"Nimesema simamisha gari!"
Kwa umakini mkubwa Dereva aliisogeza gari pembeni na kusimamisha na magari yaliyokuwa upande wa nyuma na hata yale yaliyokuwa upande wa mbele yote yalisimama.
Mwana wa Mfalme alishuka haraka kwenye gari akifatiwa na walinzi wake na kuanza kuangaza sehemu aliyokuwa kasimama binti aliyemuona kwa mara ya kwanza lakini kwa bahati mbaya hakuweza kumuona na kwenye moja ya gari Mfalme mwenyewe alishuka akifatiwa na Malikia na wote wawili wakamsogelea kijana wao.
"Kuna jambo gani linaloendelea hapo!?, mbona umesimamisha msafara!?"
Prince hakujibu swali la Mfalme zaidi ya kuendelea kuangaza alipokuwa kasimama binti kama ataweza kumuona.
"Prince Hayden nini kinachoendelea mbona humjibu Mfalme!?, kumbuka tunatakiwa kuwahi haraka kwenda kukamilisha taratibu zote za uchumba wako?"
"Hamna kitu!"
Prince Hayden alijibu na kurudi ndani ya gari, Malikia na Mfalme walitazamana ila na wao waliamua kurudi ndani ya gari ili msafara uendelee.

Binti aliyekuwa akitaftwa na Prince Hayden alikuwa tayari ameshatoka maeneo hayo akiwa kabeba kichwani beseni la mboga mboga.
"Jipatie bonga kwa bei nafuu"
"Aaaaah wewe nawe na mboga zako kila siku mboga mboga huuzi hata nyama!?"
"Hahahahaha licha ya kunichamba ila najua utaniungisha tu Mama Najim!"
"Sikuwa na mpango wa kununua mboga mboga ila lete tu ninunue alafu nimesikia kuna msafara wa Mfalme Leo umeuona!?"
"Ndio nimeuona!"
"Mmmmh ila hii nchi yetu na yenyewe bado ipo kizamani jamani yaani mpaka leo tunaongozwa na Mfalme wakati wengine wanaongozwa na marais!?"
"Utafanyeje sasa ndiyo utaratibu ulivyo Mama Najim!?"
"Wanakera bhana ila vipi kuhusu lile ombi langu Sierra!?"
"Ombi gani Mama Najim!?"
"La kuolewa na kijana wangu!, unajua wewe ni binti mrembo sana ila kijana wangu ni mwoga na hawezi kukwambia mwenyewe!"
"Mmmmh nitafikiria kuhusu hilo!"
"Usinifanyie hivyo Sierra, mkubalie kijana wangu akuoe na ukija kuishi hapa utaishi maisha mazuri kama Malikia, hutakuwa tena ukitembeza mboga barabarani kama ufanyafavyo maana kijana wangu atakutunza inavyotakiwa!"
Ongea ya Mama Najim ilizidi kumweka njia panda Sierra lakini alibeba beseni lake la mboga mboga na kuliweka kichwani.
"Nitakupa jibu ndani ya mwezi huu!"
"Usiache basi mrembo wangu!"
Aliongea huku akiyapiga piga mashavu ya Sierra aliyoondoka na kitendo cha Sierra kuondoka kuna kijana aliyekuwa amejificha alitokeza na kumsogelea Mama Najim.
"Kasemaje Mama!?"
"Wewe nawe mwoga mno aaaaaah!, unashindwaje kumwambia mwenyewe kuwa unampenda na unahitaji kumuoa!?"
"Moyo wangu huwa unaenda mbio kila ninapomuona Sierra na kukoswa ujasiri wa kuongea naye, niambie basi mama alivyokwambia!"
"Kasema atanipa jibu ndani ya mwezi huu!"
"Uhuuuuuuuu!"
Najim aliruka kwa furaha.
"Kilichokufurahisha nini hapo!?"
"Naenda kumuoa Sierra mwanamke ninayempenda kuliko yoyote yule!"
Mama Najim alikunja sura yake baada ya kijana wake kuongea na kumuuliza.
"Heeee! inamaana mpaka mimi mama yako ninayekupigia debe hunipendi!?"
"Wote nawapenda!"
"Ukiambiwa uchague kuishi na mimi au Sierra utamchagua nani!?"
"Sierra!"
"Kumbe wewe litoto lijinga ivi!"
Mama Najim alianza kumkimbiza kijana wake akitaka kumpiga na Najim naye alianza kukimbia huku akizidi kumtania kuwa ataishi na Sierra na sio yeye.

Upande wa Sierra aliendelea na kazi yake ya kuzungusha mboga mboga akitembea karibu kila sehemu za mji na hakukawia kumaliza kutokana na yeye kuwa na wateja wengi, baada ya kumaliza alianza kujongea kwa ajili ya kurudi nyumbani kwao lakini tabasamu alilokuwa nalo lilipotea pale pale na hali ya hofu iliingia ndani mwake, alikuwa akitembea kama mtu aliyenyeshewa na mvua kwa hofu kubwa na dakika chache mbele alifika kwenye nyumba anayoishi na kusimama upande wa nje akiwaza namna ya kuingia ndani.

Mda huo huo mlango ulifunguliwa na binti mmoja na baada ya kumuona Sierra aliongea kwa sauti ya juu.
"Mama njoo uone!"
Haukupita mda mwanamke mnene alitoka nje na kumtazama Sierra kwa hasira.
"Kwanini umetumia mda mrefu kuuza mboga mboga!?"
Kigugumizi kilimshika Sierra na kujibu kwa hofu.
"Wateja walikuwa washida kuwapata!"
"Lete hapa hizo hela!"
Sierra alisogea taratibu na kutoa pesa kwa ajili ya kumpatia ila alishikwa mkono na kuanza kuvutiwa ndani.
"Leo utaniambia vizuri kwanini umechelewa na uhakika ulikuwa kwa wanaume wako huko!"
Sierra alianza kujitetea kwa Mwanamke huyo mnene ambaye ni Mama yake mkubwa lakini hakuweza kueleweka.

Alifikishwa kwenye chumba anacholala na kuanza kupigwa na fimbo iliyokuwa ndani ya chumba hicho na kubaki akilia tu akijaribu kujitetea mbele ya Mama yake mkubwa.
Karibu mwili mzima ulitapakaa alama za viboko na maumivu kutawala.
"Nyenyuka ukapike haraka!"
Haraka Sierra alinyenyuka na kutoka mbio kuelekea jikoni.
"Alaaa! sitaki umalaya mimi kwenye nyumba yangu na unasaa moja tu la kupika sasa ole wako ucheleweshe chakula!"
Baada ya kuongea alitoka na kwenda kujumuika na wanawe.

Sierra alikuwa akiishi ndani ya nyumba ya Mama yake mkubwa aliyekuwa na mabinti wanne lakini kazi zote zilikuwa zake toka aanze kuishi ndani ya nyumba hiyo, na yote ni baada ya wazazi wake kufariki na kuchukuliwa na Mama mkubwa wake akiamini atapata malezi yaliyo bora lakini mambo yalikuwa ndivyo sivyo kwani aligeuzwa na kuwa kijakazi wa ndani.
Sienna, Maya, Layla na Imelda binti wa mwisho wote ni watoto wa mama yake mkubwa na wao kazi yao ni kukaa tu na kumuachia kazi zote yeye.

Sierra alianza kupika haraka haraka kama alivyoambiwa akiogopa kuadhibiwa tena kwa mara nyingine na Mama yake mkubwa au mwite Mama Sienna.

***********************

Furaha ilitawala na vigelele vilisikika baada ya msafara wa kifalme kuwasili ndani ya nyumba moja ya kifahari, walipokelewa kwa heshima na kukaribishwa ndani lakini mambo yalikuwa tofauti kwa Prince Hayden, furaha aliyokuwa nayo mwanzo ilipotea kabisa baada tu ya kumkosa binti aliyekuwa hamfahamu.
"Inatakiwa uwe na furaha Prince hii ni siku yako mhimu!"
"Najua!"
Malikia alibaki kumtazama kijana wake aliyemjibu kiufupi na wote walienda kukaa na baada ya mda kuna binti aliletwa aliyepambwa na kuvutia kwenye macho ya kila mtu aliyekuwa maeneo yale, Mfalme Leo alipiga makofi akifatiwa na wengine akiwemo Malikia wake lakini haikuwa hivyo kwa Prince Hayden, yeye aligeuka na kutazama pembeni kabisa kitu kilichozidi kumshangaza Malikia aliyekuwa akifatilia mienendo ya kijana wao.......ITAENDELEA.

Full Tsh 1000, WhatsApp 0613083801

Namba za Malipo 👇👇👇👇

0613083801 HALOPESA JINA JOHN
0748697173 M-PESA JINA JOHN..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MTEULE (The chosen one) 01  >>> https://gonga94.com/semajambo/mteule-the-chosen-one-01
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Pyar Ho Jane Dushman
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest