Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

MTOTO WA MAID ACHIA MOYO WANGU* *1---2*

10th Sep, 2025 Views


*_________________________________________*

*SEHEMU YA KWANZA*

"Binti yangu,najua sijakuhemelea vitu vyote lakini nitajitajidi awamu ijayo uende na mahitaji yote, mama jamani ata usijali, vilivyopelea nivichache nitajibana kila kitu kitaenda sawa,mama angu alinikumbatia kwa furaha, nilikuwa kwenye maandalizi ya kwenda Advance, na kwa bahati nzuri boss alitoa ofa ya kunisomesha private na chuo pia kwa gharama zake, mama angu ni house maid, alipata mimba yangu akiwa mdogo sana, amenizaa akiwa na miaka 16....

Baba angu alikuja kutalii, akawa kamrubuni mama angu, kutoka kituo cha kulelea yatima. akampangia nyumba, nakuanza kuishi nae, walitoka mbali na mkoa aliokuwa anaishi mama wakahamia Iringa, mama angu alivyopata ujauzito,baba angu aliondoka na kuahidi anaenda kufanya utaratibu wa visa, ili waondoke wote, lakini baba angu hakurudi mpaka mama akajifungua, kodi ikawa imeisha, akaanza kufua nguo kwenye nyumba za watu apate nauli arudi Kituo kilichomlea, alifanikiwa na kurudi, lakini maisha bado yalikuwa magumu waligoma kumpokea, wakampa hifadhi kwa muda, bahati nzuri kabla ya muda kuisha akawa amepata kazi za ndani, na walikubali aishi na mimi, wakampa chumba kimoja cha nje na ndio tunaishi adi leo, na mpaka leo tuko hapa hapa, kila pesa inayopatikana mama anaogopa kuitumua kwa ajili kunilipia chuo...

Lakini Boss alivyojitolea kunisomesha, tulimshukuru sana Mungu kwa ajili ya boss, pesa tuliyohifadhi tuliamua kuanza ujenzi wa nyumba, tulikaa na mama tukajadili na kushauliana tukaona mtu sahihi wa kutupa nyumba nzuri na kwa usahihi ni Jirani yetu mmoja tuliezoea kumuita kaka Benny, ni fundi mzuri sana na alifahamika kwa ujenzi wake mzuri, tulimtafuta japo maisha yetu ya chini, mwanzo tulipata hofu kumtafuta kwa uchumi wetu lakini tukajikaza tukampigia jamani alituhudumia kama watu fian hivi, mpaka tukasahau kama kajumba ketu ni ka kawaida, kwanza kaka anajua huyu acheni nyumba imenyooka ukicheki renta zake aisee utapenda rula ikasome, alitujari nakutupa ushauri mzuri sana na kutupa msaada nini tufanye kwa bajet. yetu ili tupate kitu kizuri na bora, tulifata ushauri wake na kumpa tenda, basi kaakiba kote tukakapeleka kwenye nyumba, uku mimi nasoma Advance, na nilikuwa na soma shule moja na mtoto wa boss, tulilala asubuhi mapema mama aliniamsha, ili nijiandae. nisijekuachwa tunapelekwa mapema sana,ili boss awahi kurudi, nilijiandaa haraka tukatoka na mwenzangu alikuwa amekwishajiandaa, tulitoka nikasalimia na kumuaga mama angu, safari ikaanza na wosia kama wote, mimi naitwa Gift, na mtoto wa boss anaitwa Rose, ni binti poa tu, sema anaongea sana tofauti na mimi, angezaliwa uswahilini mmh ingekuwa hatari....

Tulienda shule moja iko Dodoma, tukaachwa apo ilikuwa ni ya wasichana tupu, na hapa ilikuwa ni term ya pili hivyo tunauenyeji, tulifika nakuingia room tunaishi room moja, na tunapendana sana, japo huwa naonekana kama napelekeshwa na Rose lakini kwangu huwa ni kawaida tu sioni ajabu make natambua hajui ata kufua nguo huwa namsaidia alikosomea alikuwa analipa watu wakumfulia, ata mimi aliomba awe ananilipa lakini sikutaka, alichokifanya mzazi wake kwangu ni kikubwa hivyo nikaona nifanye kama shukran...

Nikifua namfuria nabrash viatu vyake na hata kitanda nikawa namtandikia hawezi kabisa, nilitamani kumfundisha lakini hapendi ukimwambia anahisi umemchoka, nikaamua kuacha kuwa mwalim, nifanye kwa moyo tu,leo tulivyokuwa darasan aliingia mwalim mpya, aisee mzuri jamani mmmh, mkaka anavutia uyo, niligundua ni kila mtu kamuelewa teacher, tena bora mimi kuliko wenzangu, walionekana kupotea kabisa kwenye ramani, nilipuuza na kuendelea na ratiba, Teacher alijitambulisha. Anaitwa Teacher Golden, atakuwa na sisi kwa muda, watu walikuwa wamezubaa nikajikuta napiga makofi peke yangu, nikaona aibu mno, Teacher akaomba tukae lakini darasa zima tulikaa watatu tu, wengine hol, Ilibidi apite kila dawati agonge, kuna watu Mungu alitulia haswaa kuwaumba jamani mmh, mkaka mzuri kuliko wadada....

Mimi mwenyewe niliinua mikono apa Mungu alitulia aisee, kipindi kiliendelea, baada ya kipindi mimi ndie nilikuwa kiongozi wa darasa, nilitakiwa kupeleka class journal niliinuka III nipeleke teacher akasaini, nikashangaa, Rose kanidaka nakuomba apeleke, sikukataa wala kuchukia nilimpatia, alipeleka lakini akawa haelewi ni wapi Teacher anatakiwa asain akampa sehemu so Teacher akamuuliza wewe ni kiongozi wa darasa, akawa anajikanyaga, Teacher akaomba muhusika apite mbele, nilienda uku natetemeka nisije kupigwa, nilifika akaomba maelekezo ikabidi nifunue nakumuonesha, akasain nakusepa, Rose alishusha pumzi kwa nguvu, akaomba nimuelekeze kila kinapokuja kipindi cha huyo Teacher, nilikubali make mimi ata sikuwa nawaza mapenzi kabisa...

Wanafunzi walianza kumjadili, kila mtu sasa ni Teacher G Teacher G, mda wa uji adi 4m 6, nao mada ikawa ni Teacher niliona kama wanawaza ujinga sana, nilifata uji wangu na Rose nikampelekea alikuwa pia na marafiki wengine, wakati tunakunywa uji wakaanzisha mada, Rose akasema yeye kamuwahi Teacher G ni wake, walizozana sana mimi kimya, sikutaka kuingilia kabisa, mpaka wakaelewana atakae wini basi asimuingilie mwenzake, wakanigeukia mimi, 'na wewe vipi mbona mwenzetu huchangii? Nikashangaa nakusema nichangle nini?..

"Heee usinambie mwenzetu ata Teacher G pia hajakuvutia? Nilicheka nikawaambia tu mimi na wanaume ni kama petrol na moto na salvi nawaza kitabu ata hio nguvu ya kuwaza suruali sina, maisha yangu yananibana kusoma sana," Hee Gift umezidi ivi mshipa wa hisia kweli unao mwenzetu? Nikitabasamu nakujibu na kama ungekuwepo ningehakikisha nauvunja, ili usiweo so ni bora sina, nilijibu huku nainuka, walicheka nakusema tu we kiboko sitaki kuamini mwenzetu hujashtuka kabisa, Sara akajibu hata akishtuka anajua kabisa hawezi kumpata, wote walikaa kimya....

Upande wa Teacher alikuwa ofen nikama kuna hali alikuwa anaituliza hivi kwa kuilazimisha sana, mpaka anafumba macho, anafumbua, akaona kama joto sana, akaamua kufungua kabisa dirisha, na sisi tulikuwa jirani na dirisha, alituona akarudi haraka kukaa, huku anapumu utazani katoka kukimbizwa na jitu la kutisha.....

Itaendelea....

Chapter 2

Muda uliisha tukarudi kwenye vipindi, walimu waliingia, mpaka vipindi vikaisha,tulitoka, nikafua nakudeki, nikaingia kujisomea, upande wa Teacher alikuwa anawaza, aliamua kumpigia Baba ake, Dady uku sio salama, naomba utafute mwalimu wa hawa watoto wako mapema, nilikwambia tayari nimeshaanza kupata wakati mgumu kibaya zaidi sasa awamu hii sio wao tu na mimi nataka kuingia kwenye tatizo, "Golden usinambie hatimae umependa mwanangu wataacha kukuita shoga, mzee aliongea hadi akalia...

Mzee ivi unajua unachokiongea lakini? Huyu ni mwanafunzi Baba natakiwa kukaa mbali nae mapema sana tusije kuharibu, Baba ndo msiri wangu kweli nimempenda, na naamini ni mtu sahihi sana lakini nahitaji mda,nahitaji kukaa mbali amalize masomo yake, sikutegemea kama nitapenda haraka hivi, sijui kama huyu nae hatoniacha tena Baba nahitaji muda

alionekana kutoka kwenye kisanga kizito sana, alikuwa na mchumba wake wa toka utotoni lakini mchumba alikuwa na mtu mwingine, amekuja kumuacha bila taarifa, anakutana na picha tu za ndoa tena kibaya zaidi na rafiki yake ndie aliemuoa, aliumia sana nakuhisi anakasoro, kila akiingia kwenye mahusiano hadum, na hajui shida nini, wengi wanamtaka lakini hawadumu nae...

Imefika hatua aliacha kupenda nakuamua sasa atadate na mtu yeyote anaemtaka, ila sio anaemtaka yeye, alifanya hivyi lakini bado aliachwa tena bila taarifa, hakuwa anaumia kama alivyoumia kwa yule wa kwanza kwa sababu hajawapenda, anadate nao tu kupima kama watadumu, na kila anaedate nae kelele na kumuhisi anachit muda wote, alikuwa anakosa kabisa amani, hakutaka apende sasa moyo moyo, hauna break umeshazama mahali tena kwa mwanafunzi...

Na hii ni shule ya baba ake, yeye sio Mwalim kaja tu kumsaidia Baba ake kwa sababu kulikuwa na upungufu wa Walimu hasa wa Chemistry akaamua kuja kujaza hio nafasi, kwa muda, yeye ana biashara zake zina usimamizi mzuri akaona sio mbaya, aje kupumzika kwa kufundisha, japo alijua kabisa wanafunzi watavutiwa nae hilo analijua,na alishazoea, ila anaepuka asipende, lakini Bahati imeangukia kwenye kupenda, alijikuta anawaza bila kutulia, kila akilala inakuja tabasamu ya binti anaemchanganya, anajikuta anakosa kabisa utulivu...

Alianza kufanya mazoezi usiku ili tu amsasahau uyo binti, lakini wapi,akaamua kuoga apo saa tisa tayari hajapata hata tone la usingizi, alijikuta anakesha, mpaka kunakucha...

Itaendelea.

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MTOTO WA MAID ACHIA MOYO WANGU* *1---2*  >>> https://gonga94.com/semajambo/mtoto-wa-maid-achia-moyo-wangu-1-2

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest