Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

MTOTO WA MAID ACHIA MOYO WANGU❤ 3--4

11th Sep, 2025 Views 16


Chapter 3

Vipindi viliendelea, ulifika muda wa kipindi chake. kila mtu alikaa kimtego darasani tukabaki wawili tu, ambao tulikuwa kawaida, wengine wote waliacha mapaja wazi, Teacher aliingia. akawapuuza tu, alifundisha, ila kuna namna akawa anatazama sana upande wa Rozi, baada ya kumaliza kufundisha akaomba darasa tujitambulishe, tukawa tunajitambukisha kwa majina kila mtu, tulijitambulisha, akashukuru na kuondoka, baada ya muda akaomba saa moja ya kila mtu kujitambulisha, in deep, sio tu majina, watu wote walikubali kwa furaha, tuliombwa tujadili kisha majibu tumpe kiongozi wa darasa ampelekee, tulijadili, wakatoa muda upi tumpe mwalimu, nikatakiwa kupeleka Rozi akaomba yeye apeleke, watu darasani wakagoma wakaanza vita, ikabidi waelewane niende mimi mwenyewe....

Nilienda nikagonga nikaruhisiwa kuingia, nilimpa mda, nikawa nataka kuondoka akanizuia, akainuka kwenye kiti, nilikuwa muoga, muda wote naongea sijamtizama, na huenda ata angekuwa mwingine ata nisingejua, alivyoanza kusogea ndio nikainua macho kumtizama, nilivyomtizana tu, akasimama akafumba macho nakuniomba niende, nikaondoka huku najiuliza alinisimamisha ili iweje, au alitaka kuniuliza kuhusu Rose, make toka mda namuona anatizama upande wetu sana, nikajua tu, huyu kampenda Rose, nilitabasamu nakurudi darasani...

Nilifika kila mtu anauliza kasemaje, niliwatizama kwa kuwahurumia tu, nikawaambia kasema tu tujiandae,basi kila mtu akarudi kwenye dawati lake kusubiri, ila mida ilivyokaribia, robotatu ya darasa, walichomoka kumbe wameenda kujipodoa,kila mtu akawa anarudi kapodoka, adi Rose na Sara, nilibaki tu natabasamu jinsi wanavyohangaika aisee, muda ulifika kwanza Teacher kaingia anashangaa watu wako tofauti, hakufumbia macho, akaamua kusema, naona mmependeza wenyewe, wakafurahi kusikia. wamesifiwa...

Tulianza kujieleza tunakotoka, idadi ya familia, kila mtu akajieleza adi kazi za wazazi, mimi pia sikuficha nilijieleza, sikuona aibu coz darasa zima linajua, kuna siku nilimkera Rose akaamua kutangaza, sikuchukia nilichukulia kawaida tu,make ni kweli mama angu ni house maid, tulijitambulisha wote tukamaliza, mtoto wa kapuku nilikuwa peke yangu, wengine wote wana toka familia nzito, ata Rose cha mtoto...

Alishukuru nakutupa wosia,na nikama alikuwa anatoa onyo kijanja ili wasimuandame, alikuwa akihusia maisha na kuwazuia mahusiano kwa wakati huu sio salama tujitahidi sana tumalize kwanza shule, angalau huko chuo, aliongea kwa upana sana, kisha akaondoka, kila mtu akawa anahisi, kaambiwa yeye, watu walinywea kwa muda kulipoa make muda wakujitambulisha watu walijimaliza mno...

Siku iliisha, hatimae wakaanza kumzoea japo kuna ambao hawakusikia hasa Rose, alitoroka usiku na kwenda kwa Teacher, alihisi kabisa Teacher anampenda make kila akiingia darasani jicho huwa huu upande wetu, na aliamini kabisa siwezi kuwa mimi, make yeye ni mzuri kunizidi mimi, alitoka kwa wizi akampa pesa mlinzi akachomoka, alivyofika kwanza Teacher alishangaa, alimuwasha kofi kisha akamweka chini nakumshauri asifanye huu ujinga tena sio tu kwake hata kwa walimu wengine...

Alimpa wosia na kumtaka arudi Rose aligoma nakuomba tu angalau akubaliwe, Aliwekwa kofi jingine nakutimuliwa, akasema atapiga kelele watu waje, akaambia sawa piga, Rose alishindwa akaamua kuondoka lakini akiwa na hasira. mno, alifika Bwenini akaniamsha, akaanza kunililia na kujieleza kwangu, akanisimulia kila kitu, dah nilimuhurumia nikamshauri ajifanye nae kukaza huenda, Teacher kuna kitu anaogopa, au huenda, anasubiri umalize shule, tuliamini hii ndio sababu tukakubaliana kumpa mda Teacher, kulikucha vipindi vikaendelea, ila leo kukawa na jipya tena yani la motooooo...

Itaendelea....

*SEHEMU YA NNE*

Waliingia walimu wakataita majina ya wanafunzi tukabaki watu 7 tu, wengine wote walituhumiwa. kwenda usiku kwa Teacher G na mlinzi aliepokea. rushwa walitembezewa fimbo zakutosha, na mlinzi akafukuzwa kazi, yani hawakuamini, kila mtu alienda kwa muda wake, wamekuja kuumbuliwa mbele ya darasa, tena fimbol ziliwakuta kama mvua, na wazazi wakaitwa, wakapewa onyo, apo kukawa kumetulia, yani walipoa wakawa na adabu sio kawaida, Rose pia alikuwa miongoni mwao....

Vipindi viliendelea likizo ya mwezi wa nne ikafika, apo mwezi wa 5 4m 6 wahitim tupande tulirudi likizo, tukakuta kaka zake Rose waliokuwa nje kimasomo pia wamerudi, na kuna mmoja Ronard, kaka mkubwa alikuwa ananimendea sana, hasa hii likizo nilijitahidi sana kukaa nae mbali adi muda wa shule kufungua ukafika, akaomba yeye ndo atupeleke, Boss hakukataa, na hivi mmewe pia alikuwa likizo ndo kabisaaa....

Akaona kapata furusa yakubaki na mme wake, Ronard, alitupeleka shule lakini njiani akaanza kunipiga mistali uku mdogo wake anamkuwadia, nilikuwa kimya nikaomba wanipe muda lengo nifike tu shule salama, sikuwa na imani nao kabisa, sikuwa nataka kupenda kabisa,historia. ya mama angu ilikuwa inazunguka sana kichwani kwangu, apa kichwani nina nywele ndefu sana kila wiki lazima nizipunguze, ilinibidi kujifunza kujishave mwenyewe na wembe kichwani, ili kuficha urefu nilirithi nywele za baba angu asiejulikana, nachojua tu ni mzungu wa

Canada....

Walikubali na kutuwaisha shule, kaka Ronard akatoa pesa nyingi akatugawanisha, nilikataa wakanibembeleza, huku wanasema mbona kama unatukwepa, nilijikaza nikapokea ilikuwa pesa nyingi kwangu, kwasababu mama angu hunipatia pesa ya matumizi ama emergence elf 15 ama 20, na tayari ameshanipatia, hii aliyonipa kaka Ronard ni laki moja na nusu, ilinipa wasiwasi mno ata kuipokea, nilijikaza tu, ili yaishe...

Nilipokea akafurahi, nakusema nakupenda sana Gift nakuahidi ukimaliza tu masomo yako mimi navuta jiko aisee, sitaweza kusubiri zaidi, nilitabasamu tu bila kujibu chochote, alitaka kunikimbatia nikakimbia, wakahisi naona albu, Rose akafurahi nakuanza kuniita wifi,mimi kimya sikulipenda kabisa hilo jina, leo tunafika tunatambilishwa, madam mpya na Teacher sasa huyu alikuwa kiboko acha nyie nyie, kwanza uyu mzuri afu anasauti fulani ivi huchoki kusikiliza dah..

Ila toka watu wachapwe wakawa makini apo unatamani kimya kimya,na madam nae hakuwa haba mrembo atari, na alifanana sana na Teacher G, na alikuwa na jina kama langu, alitokea kunipenda adi mwenyewe nikajua yani kila kitu utasikia somo fanya hivi, mara peleka hiki au atakuja na chakula ataniita nikale nae, alikuwa makini ata kunikazia kwenye masomo mno, adi nikampenda, nikajihisi nimepata dada. na mimi, kuzaliwa bila ndugu inauma nyie unakuwa unatamani upate ata mtu tu wakumuita dada, kaka, mdogo wako yani sijawai ata kupata wakucheza nae, mama angu alikuwa ananiacha anaenda kazini na ivi ni ndani ya geti nikawa nacheza tu peke yangu...

Sitakiwi kuchangamana na watoto wa boss,

mama aliweka mipaka ili asilete kelele, nilizoea

nikawa namsubiri akirudi nakula nacheza

mwenyewe nilivyoanza shule ndo ikawa angalau, ata kuongea nimeanza kujua nikiwa na miaka 7 sikuwa na mtu wa kuongea nae mara kwa mara ikapelekea kutokujua kuongea, nilivyopelekwa shule ndo nikaanza kujua nilipata amani sana, nikajikuta nasoma kwa bidii ili nisimualbishe dada G, sijawai kushika no moja lakini awamu hii nilishika, kila mtu hakuamini, mimi huwa ni 8,9 sijawai kuwazidi leo nimekuwa wa kwanza kama utani, wakaanza majungu, Madam. ananipendelea, na Teacher mpya alianza kutembea na Rose, lakini kumbe alikuwa pia ananitaka, alikuwa anapambana nimuelewe. nikagoma, akawa anatembea na wanafunzi kama 5, afu wakajuana, kila siku nikupigana, afu mwenzao yuko bze hajali, ile kitu ilijilikana. mwalimu akafukuzwa apo tumeingia 4m 6....

Rose alijikuta hachomoki kwa teacher

aliefukuzwa akaendeleza mahusiano, akawa anatumia simu ya magendo, nilivyotaka kumshauri akawa mkali nakudai namuonea wivu, kanipa kaka angu sijaridhika, nikashangaa mbona mambo kayakuza sana, niliamua kumuacha afanye anachokitaka, siku hazigandi hatimae tulihitimu, siku ya graduation, Mama alinipigia simu nakusema hatoweza kufika hamna mtu wakubaki nyumbani, ila boss atakuja nisihuzunike, ukweli hii iliniuma mno, nilijikaza kulia nikashindwa kabisa, nilitoka nikajibana sehemu nakuanza kulia, nilitamani mama angu

ahudhurie ata kama ni maskini...

Mama ni mama tu, niliumia mno, nilijikaza kumbe wakati nalia Madam Gift alikuwa nyuma. yangu, alinikumbatia, akaniambia lia machungu yote yaishe bado hujalia, nikama aliniambia lia kwa nguvu, nililia sana, nilivyotosheka nikanyamaza, akaniambia anaomba yeye ndie awe ndugu yangu, anatamani awe na ndugu lakini hakupata hio bahati na kalelewa na baba tu, tuliunganisha undugu nakupena no na namna yakupatana, na hata majina mtandaoni tukakubaliana majina yakuandika incase tukapotezana basi mtandaoni itakuwa sehemu. yakupatana kwa hayo majina ya tuliyokubaliana tutatumia....

Madam aliniaga akajiandae yeye ni dada sasa, tulifurahi kwa pamoja na kuagana, kesho yake ilikuwa graduation wazazi walifika, na sheree ikaanza, muda wa keki, ya pamoja mzazi aliekuja kunilisha keki alikuwa ni Madam G, mama Rose alijisahau, akawa katoka muda naitwa alikuwa anaongea na cameraman, nilimlisha madam na yeye akanilisha na taji aliandaa, na Muda wa vyeti pia alijitokeza na vyeti nilichukua vingi kwakweli...

Ilifika muda wa kukaa na familia sasa, Boss alikuja na keki moja ya Rose, niliumia ila nikawaza nakuona nakosea sana, sipaswi kukasirika hii iko sawa, mama alitakiwa aandae yani wanilipie ada bado na mambo madogo madogo niwasumbue hii nakosea, nitakuwa sina. shukrani, hili walilonitendea nikubwa mno kuliko hio keki, nilivyowaza tu ivo nikapata amani kabisa nakufurahi pamoja na wao, kumbe Madam aliandaa keki kwa ajili yangu, alileta keki tukaungana na Mama Rose, nilijikuta nalia kwa furaha mno, nilipewa zawadi na keki tukakata zote, na kula juu...

Nilimshukuru sana dada angu wa hiyari,

niliomba kuongea na mama kupitia simu ya dada angu, nilimtambulisha kwa Dada angu wa hiyari na kumsimulia aliyonitendea mama alifurahi adi akalia, waliongea nakupongezana, tukawa ndugu, nilipiga picha za kutosha, Rose aliniita na kunambia, kaka ake ananiita kule nyuma, nilisita sana, nyuma tena nilimwambia naogopa kwenda peke yangu, alicheka nakuniambia niache uoga, alisema nimfate anisindikize, nilikuwa naogopa mno...

Nilienda nikakuta kuna cameraman, keki ya jina langu, па zawadi, Ronard alivyoniona alitabasamu nakuomba tukate upya keki, kaandaa mwenyewe kwa ajili yangu, nilisogea Itaendelea...

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MTOTO WA MAID ACHIA MOYO WANGU❤ 3--4  >>> https://gonga94.com/semajambo/mtoto-wa-maid-achia-moyo-wangu-3-4

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Tangazo - PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest