Akiwa kwenye ujinga wake, mlio wa risasi ukasikika, apo akili ikarudi, akanikumbatia vizuri mda huo tumelaliana chini ya meza, apo natetemeka vibaya mno, bahati ikawa upande wetu, ving'ora vya polisi vikawa vimewahi kufika, tukanusurika ila mlinzi mmoja alilambwa shaba akawahishwa hosptal, sisi tukahama kabisa pale, lakini akili yangu haikuwa sawa, Teacher ni Doctor aliewewa nini napitia, alitafuta namna ya kuniweka sawa ndio tukarudi nyumbani lakini hatukuwa tumefikia muafaka...
Teacher aliondoka, Rose alikuja na kuanza kugomba, akawa analalamika nimemuibia bwana ake, mama alishangaa, akaanza kuhoji, mama Rose nae akapanic nakuchukia mno, Ronard alikuwa ananitazama uku analia, akaamua kuvunja ukimya nakusema, mimi nimemsalit, akatoa picha za kule nyuma siku ya graduation kama ushaidi, yani kelele iliyotokea hapo mmh,nilijaribu kujieleza lakini haikusaidia kitu, Dada pia alitoa ufafanuzi lakini hawakuelewa, Rose akasema kama nahitaji ugomvi uishe, basi niolewe na Ronard ili nimuachie mtu wake...
Niligoma wakasema watanionyesha, nimekula pesa za kaka ake saiv namkataa, nilipe nilipata hasira uzuri pesa zote sikuwa nimezitumia kabisa, nilichukua nakuwaletea, waligoma kuchukua, Ronard akawa anaomba nisimfanyle ivo nimpe nafasi, alipiga adi magoti, mama ake akawa anamzuia hataki mkamwana asie na status hana ramani, Lakini Ronard hakusikia, mama alimuonea huruma akamuinua nakumwambia saiv nimepanic tujipe muda, Ronard alikubali nakuingia chumbani kwake...
Upande wangu mama alijua kabisa tayari kuna tatizo sijui itakuwaje, hasa chuo nyumba yetu imeshaisha, kimbembe wakigoma na mkopo nimesoma shule ya kulipia kuna hatari ya kukosa mkopо па тата hawezi kuaford gharama ya chuo, alianza kupata mashaka, dada alimtia moyo nakumwambia atapambana nitasoma tu, japo ata yeye hana uchumi mzuri lakini hawezi shindwa kunilipia ata chuo cha kawaida afu nitajiendeleza walishauriana na kuona kukikucha ni vyema tuondoke kwanza ili kutulie...
Kweli asubuhi tuliondoke bila kuaga, nilianza kuishi na madam, nyumbani mama alianza kuishi kwa tabu, ilifika atua ikawa ni hatari mno, nilikuja kujua siku moja nimempigia mama alionekana kuumwa sauti iko chini, akawa kasahau kukata simu baada ya kuitwa nikasikia anaambiwa aoshe upya madrisha hayajatakata, na nguo afue, tena haraka,awaishe na chakula, akaomba leo aende hosptal hali yake sio nzuri lakini wakagoma, "kama unaenda hosptal hakikisha unaenda mazima...
Aisee niliumia, na dada alikuwepo, nilimuona machozi pia yanamtoka, aliniambia kazi ziko nyingi, mama aache hio kazi tutafute biashara, ilibidi mimi nirudi kumuuguza mama, hatukuwa. na ujanja, nilifunga safari bila kumwambia,apo na matokeo yalikuwa yametoka tayari, Rose alifeli mimi nilifaulu, nilifika jioni, nikakuta mama amedondoka chini Ronard ndo anahangaika nae, nilichanganyikiwa, aliwasha gari tukamkimbiza hosptal...
Tulifika akawahishwa kwenye matibabu, apo Ronard akawa ananituliza nisijali mama atakuwa sawa, baada ya muda mama alipata fahamu nilienda kumuona apo macho yamevimba vibaya mno, Ronard alipigiwa simu nyumbani akaniomba no, ili tuwasiliane kwa emergency yoyote, nilimpatia, alivyoondoka, nikarudi kwa mama, nakuta Doctor anaemtibu mama kamletea adi chakula, kumcheki vizuri ni Golden...
Alimhudumia mama nakusema natakiwa kuwa makini na mama kwa sasa kazi ngumu sio salama kwake, ameumia sana mgongo lakini pia amekutwa na homa ya muda mrefu, tulilazwa kwa siku 5,Bili yote ililipwa na G, Ronard alisafiri kikazi na baba ake hivyo hakuwahi kurudi akawa anatujulia hali kwenye simu, aliniomba bill alipie nilikataa nikamwambia tayari akasema anatuma ya matunda nilikataa, nilishaogopa pesa zake, lakini alilazimisha, akawa akituma narudisha muamala, na yeye anatuma tena, nikaamua kuacha akizitaka nitamrudishia....
Itaendelea....
Full 1000
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments