Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

MUME WANGU ALIVYONIOLEA MKE WA PİLİ SEHEMU YA : 04

10th Sep, 2025 Views 81



Nilinyanyuka nikiwa na hasira sana lakini pia usoni mwangu nililowana machozi tu.

“Ni nini hiki mume wangu ??”

Nilimuuliza uku nikikausha machozi yaliyoko usoni mwangu.

“Nini kuhusu nini, nakuongelesha hapa unajifanya unisikii we mjinga nini, hivi Shamsa hii dharau unaniletea mimi kipindi hiki umetoa wapi ? Nakuona unajitaidi sana kuonesha Kuwa unanimudu unataka Khadija anichukuliaje Mimi “

“Hamad umeharibu swala
Yangu ujue “

“Hapa ni msikitini au ? Shamsa hapa ni Nyumbani kwangu na Nina haki ya kufanya chochote kile, mambo ya swala Sijui ujinga gani gani uko kwa baba yako wa kimasikini na sio Nyumbani kwangu “

“Nitukane uwezavyo lakini achana na familia yangu, zungumza uwezavyo lakini achana na baba yangu, hamad umebadilika sana mume wangu sijakuzoea hivi Mimi “

“Yaani wewe Bwana 😂 shida yako ni kwamba umechelewa kunijua tu, anyway sijaja hapa kwaajili ya hizi Kelele zako Nimekuja kufata haki yangu kama mume kwako “

“Uko serious??”

“Kwani Mimi na wewe tunautani tangu lini, shamsa chojoa hizo nguo zako za kizee haraka “

Alizungumza mume wangu na muda huo huo akanivuta nguo zangu na kuanza kuzilalua Kana kwamba ni mtu ambaye amepanga kubaka.

Kwa Mara ya kwanza naweza kusema Kuwa nimebakwa na mume wangu Mwenyewe 🥹 hamad alitumia nguvu nyingi sana juu yangu lakini pia hakukuwa ata na kuandaana alichojali ni yeye kukizi haja ya mwili wake pasi na kujali Kuwa nilikuwa nikipata maumivu makali sana.

Baada ya kumaliza kila kitu alinyanyuka na kuingia bafuni akaoga na kuja kujitupia kitandani na baada ya muda usingizi Mzito ukamchukua.

Kwa upande wangu Walahi nilikuwa na maumivu makali sana Nikabaki nikimlilia Mungu wangu na kulalamika kimoyo moyo.

“Kama Mungu ulijua Kuwa Hamad sio sehemu sahihi kwenye maisha yangu Kwanini umenifanya niwe mke wake ? Kwanini umenifanya Niharibu maisha yangu kwaajili yake 😫 ni kweli nilikuwa mkaidi kiasi kwamba ukuweza kunikomboa kwenye manyanyaso Makubwa kiasi hiki ? Kama ndoa ni baraka hii yangu ni nini Mungu ? Sijakataa Kuwa na mke mwenzangu lakini Kwanini iwe kwa njia ngumu kiasi hiki ? Mungu Kama maisha yangu ni hivi Basi nichukue mapema Mimi “

Eeeh nilijikuta nikianza kukufuru sasa maana ni Kama Mungu anioni hivi licha ya mateso makali sana ninayopitia juu ya huyu mwanaume 🥹.

********

Majila ya saa 11 alfajiri hamad aliamka zake na pasi na kuzungumza chochote akanivamia Tena mwilini na kupata cha asubuhi.

“Utaanda kifungua kinywa kizuri kwaajili yetu “

Alizungumza hamad pale tu alipomaliza kutua Mzigo wake wa asubuhi.

Sikuweza kujibu kitu zaidi nilibaki nikimuangalia na kujiuliza maswali Mengi sana juu yake,
Kiukweli huyu sio hamad wangu, huyu sio hamad ambaye Mimi Niliachia kila kitu kwaajili yake, sikujali chochote kile zaidi ya penzi lake.

“Umenisikia ??”

Hamad aliniuliza baada ya kuona Kuwa Nipo kimya.

“Haya sio maisha mume wangu “

Nilimwambia.

“Maisha yapo Nyumbani kwenu kule ambapo watu wanalala mpaka sebuleni si ndio ?”

Aliniuliza hamad kwa dharau ya hali ya juu.

Kwa unyonge wa hali ya juu nikanyanyuka na kwenda bafuni kwangu na kuanza kuoga, baada ya kujiweka mwili wangu safi moja kwa moja nikaenda kuweka Nyumba yangu safi lakini pia kuandaana kifungua kinywa cha familia nzima.

Sawa mambo yalikuwa magumu sana kwangu lakini hakuna kitu kilinizuia mimi kufanya majukumu yangu, nilihakikisha Kuwa natekeleza majukumu yangu Kama mke lakini pia mama wa watoto wawili.

“Napenda nguvu yako kwenye kujituma as a wife material “

Alizungumza Khadija ambaye aliingia jikoni na kunikuta nikiweka vitu Sawa kwenye fliji langu, kWa upole nikageuka na kumtazama kisha nikamsalimia.

“Za Asubuhi Khadija “

“Salama, aaaah nilikuwa Naomba mayai ya kukaanga tu maana naona mezani umeweka mayai ya kuchemsha na Mimi uwa Situmii“

Alizungumza Khadija na kutaka kuondoka, kWa haraka nikamjibu.

“Mayai yameisha Ila nitaenda sokoni leo mchana “

Khadija akanitazama kWa macho yake ya dharau kisha akaniuliza .

“Kwahiyo asubuhi hii nisile au nini maana yako ? “

“Maana yangu ni kwamba Tumia kilichokuwepo kWa sasa, unaweza ukatumia sausage nimeweka pale, lakini pia ata nyama nimeweka “

Nilimjibu kwa utulivu wa hali ya juu maana niliona ni Kama yeye amejipanga na bifu hivi.

“Usinipangie nini cha kula nimekuabia nataka mayai ya kukaanga”


Kabla sijaweka neno muda huo huo mume wangu akaingia jikoni na moja kwa moja akamkumbatia Khadija kwa nyuma.

“Nilikuwa nakutafuta uko Kote laazizi wangu “

Alizungumza hamad kWa sauti ya mahaba uku akipapasa shingo ya Hadija.

“Aaaah nilikuja kumfuata Dada Shamsa ili tuungane kwenye kifungua kinywa “

Alizungumza Khadija.

“Ndio maana nakupenda sana Khadija wewe ni mwanamke wa kipekee sana iliyejawa na upendo “

Alizungumza hamad pasi na kujua Kuwa anamsifia mtu ambaye atakiwi kabisa kupata hizo sifa.

“Twende mke wangu “

Nilibaki nikiwaangalia tu wakitoka nje, Kiukweli niliona Kuwa Nina maadui tu Ndani kwangu na sio kitu kingine, sikuwa ata na nguvu ya kwenda kuungana nao kwenye meza ya chakula nilibaki kuendelea na kazi zangu.

*******

Maisha yaliendelea kusonga ingawa ilikuwa ni kazi kubwa sana kwangu lakini nilihakikisha Kuwa nakuwa İmara kwaajili yangu lakini pia kwaajili ya watoto wangu.

Siku moja niliamka nikiwa siko Sawa kabisa na kila mtu alipotoka Nyumbani nikafunga safari na kwenda hospital.

Nilifika hospital na kufanya vipimo vyote na baada ya hapo Nikabaki nikisubilia majibu kutoka kWa daktari.

Nikiwa nimekaa kwenye sehemu ya kusubili majibu gafla akaja msichana ambaye ata sikuwa namfahamu lakini akanisogelea Karibu zaidi na kuniambia

“Samahani, wewe ni Shamsa au nakufananisha ??”

Kwanza nilimuangalia kwa muda uku nikivuta kumbukumbu kwamba niliwai kumuona wapi lakini sikuweza kabisa kukumbuka kisha nikamjibu.

“Ni Mimi wewe ni Naani ??”

Pasi na kujibu swali langu msichana huyo akajikumbatia kWa nguvu sana na kuniambia.

“I miss you twinie, Nimekuwa nikikuulizia sana sana jamani “

Msichana huyo alionekana kunijua sana na alikuwa so emotional kwa kukutana na Mimi maana adi machozi vilikiwa vikimlenga lenga.

“Wewe ni Nani kwani ??”

Nilimuuliza Tena maana aliniweka njia panda.

“Me NEHA jamani Neha your best friend “
Nyieeeeeh nilijikuta nikimkumbatia kwa nguvu sana jamani, Yaani kwa nguvu kuliko kawaida.

Iko hivi jamani, huyu Neha ni Rafiki yangu ambaye nimesoma nae shule ya msingi na tukapotezana tulipoanza sekondary, yaaani huyu ndio Yule Rafiki yangu wa toka nitoke Walahi, yaaani tunapendana kuliko maelezo.

Kabla hatujazungumza kitu chochote kile Jina langu likaitwa na Mimi chap nikawai si unajua watu wengi wanataka huduma.

“Aaah Shamsa, pole kWa hali yako lakini ni habari njema tu Wala si ugonjwa Bali unakaribia Kuwa mama kWa Mara nyingine Tena shemeji yangu “


Alizungumza dokta huyo ambaye ni Rafiki wa Karibu sana na mume wangu.

Ila nyieeeh 🥹 haya ni majaribu gani jamani, Yaani kWa jinsi ambavyo maisha yapo hovyo kWa upande wangu bado naenda kumuongezea Mtoto huyu mwanaume 😫💔 eeeh Mungu nisaidie….

.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MUME WANGU ALIVYONIOLEA MKE WA PİLİ SEHEMU YA : 04  >>> https://gonga94.com/semajambo/mume-wangu-alivyoniolea-mke-wa-pl-sehemu-ya-04

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE
PROMOTE YOUR BUSINESS FOR FREE

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest