Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

MY CRAZY HOUSE GIRL 8

21st Aug, 2025 Views 39


Vanessa alisimama katikati ya sebleni, akishikilia ile karatasi kwa nguvu kana kwamba ilikuwa silaha ya kujitetea.
Damian alimsogelea kwa kasi ili amnyang’anye lakini Vanessa alimsukuma kwa mkono mmoja nyuma.
" Khaaaa Vanessa umenisukuma?
"Usinijaribu Damian!" alisema Vanessa kwa hasira.

Alifungua bahasha na kuanza kusoma.
Midomo yake ilianza kutetemeka alipoona jina la hospitali, tarehe, na kipengele kilichoandikwa kwa maandishi makubwa:
“POSITIVE PREGNANCY TEST.”
Aligeuza macho na kumtazama Alisha ambaye sasa alikuwa amekaa, amejikunja kama mtu aliyekata tamaa kabisa.
"Mimba? Damian unahusika na hii , hii mimba ni yako?"
Damian alishindwa kujibu, akashika kichwa kama mtu aliyechanganyikiwa.
"Vanessa tafadhali, usiingilie hii ishu, haina uhusiano na wewe," alisema kwa sauti ya kuomba.
Vanessa alicheka kicheko cha dharau.
"Ha! Haina uhusiano na mimi? hii ina kuhusu sana tu kumbe ulikua unamchezea mwanafunzi?"

Damian alifungua mdomo kutaka kuongea, lakini Vanessa alimkatisha kwa sauti ya juu.
"Shut up, Damian! Shut up!"
Alimgeukia Alisha, macho yake sasa yakiwa yamejaa mchanganyiko wa huruma na hasira.
"Wewe ni mjamzito na bado unatembea usiku kwenda kwa mwanaume ambaye anakutaka utoe mimba yake?"
Alisha aliinamisha kichwa chini, machozi yakimdondoka kimya kimya.
Vanessa alitembea mpaka alipoketi Alisha na kupiga magoti mbele yake.
"Alisha, usimsikilize huu mjinga. Hiyo ni damu ya mtoto asiyokuwa na kosa. Ni dhambi kubwa sana kuuwa kiumbe kisichokuwa na hatua kumbuka ukitoa hiyo mimba roho ya huyo mtoto haitaacha kujuandama mpaka na wewe utakapoingia kaburini.
Maneno ya Vanessa yalianza kumpa uwoga alisha.
" wewe , wewe Vanessa una kiherehere sana sijui kwanini unapenda kuingilia maisha yangu ? Sasa nasema hivi mimi nimemaliza hela ya kutoa mimba hiyo ilipotoa usirudi hapa na huyu kichaa ndio atakusaidia kwenye malezi ya huyo mtoto.
Damian aliondoka mbele yao na kurudi chumbani kwa hasira, akipiga mlango kwa nguvu.

Vanessa alimsogelea Alisha na kusema kwa sauti ya upole,
"Simama twende chumbani kwangu upumzike. Hapa hauna hifadhi tena."
Alisha alimuona Vanessa ana roho ya utu sana .
" Hapana dada mimi nitaondoka, nashukuru sana kwa ukarimu uliyonionyesha.
" Sawa lakini huyo mtoto ni furaha yako ya badae usije ukamdhurumu.
" Nimekuelewa dada hata hivyo nilikuja tu kumwambia ajue . Nilikuwa najua hawezi kukubali sababu Damiani ni mtu anayependa sana starehe na ni mtu anayependa sana wanawake nineshagombana na wanawake watatu kwaajili yake na hazikutosha alimchukua rafiki yangu Tausi . Bado hajamaliza ujana.
" Ni vizuri umemjia hicho alichokuachia ni zawadi yako jifunze vizuri.
Vanessa akimsindikiza Alisha mpaka nje . Baada ya Alisha kuondoka alirudi ndani kwenda kulala.

Wakati huo huo, Damian akiwa chumbani kwake, amekaa kitandani akiwa ameshika simu yake kwa hasira. Alitaka kumpigia rafiki yake wa karibu Romani ili amsaidie kuongea na Alisha. Lakini kila alipotaka kupiga, alisitisha.
Moyo wake ulianza kupata wasiwasi. Kilichokuwa rahisi awali sasa kilionekana kuwa ndoto mbaya.
"Mbona Vanessa anaingilia mambo ya watu? Hii mimba italeta balaa," alisema kwa sauti ya chini.Kesho yake Damiani aliamka akiwa kasirika alikaa chumbani kwake akiwa anatafakari jinsi ya kumaliza tatizo la Alisha mara simu yake iliingiza ujumbe.
" Damiani kama umeamua kuikataa hii mimba basi sawa ila mimi sitatoa hii mimba nitazaa mtoto wangu. Nakupa nafasi ya wiki moja kwaajili ya kufikiria mara mbili mbili ikiwa unataka hii mimba pamoja milango iko wazi na kama utakaa kimnya mpaka hiyo wiki moja ikapita basi utapoteza haki ya kuwa baba wa huyu mtoto.
Damian alipomaliza kusoma alitoa tabasamu lenye dharau na kusema.
" Sina haya ya kuwa baba hilo ni jukumu lako Alisha nakutakiwa kila la kheri kwenye safari ya ulezi wa mimba hatimae mtoto.
Mara mlango wa chumba cha Damiani uligongwa .
" Karibu ingia.
Mlango ulifunguliwa akaingia Vanessa.
" Habari za asubuhi Boss!
Damian alimkata jicho Vanessa kisha akafyonza.
" Umeamka na kisiwani eee.
" Unataka nini wewe cha umbea?
Vanessa alitabasamu alafu akasema.
" Nimekuja kukuangalia kama upo salama maana sio kawaida yako kuchelewa kuamka.
Damian akamuangalia
" Wewe mtoto wa kike mambo yangu hayakuhusu naomba utoke chumbani kwangu na siku nyingine ukiingilia kwenye mambo yangu nakuapia humu ndani utaondoka hii nyumba utakiona paa tu.
" Kwa kosa lipi lakini?
" Hujui kosa? Sasa endelea na ushilawadu wako utaona nitakachofanya.
" Acha makadirio bwana kwenye ukweli lazima tuseme, kwani wewe ni nani mpaka usiambiwe ukweli . Nenda kaoge alafu uje sebleni nimeshakuandalia kifungua kinywa.
Vanessa alifungua mlango akatoka huku Damiani akimsindikiza kwa macho na kujisikitikia maana safari hii amepata house girl kiboko

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MY CRAZY HOUSE GIRL 8  >>> https://gonga94.com/semajambo/my-crazy-house-girl-8

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest